Quantcast
Channel: LEWIS MBONDE BLOG
Viewing all 7853 articles
Browse latest View live

HAWA NDIO WAREMBO WALIOUTIKISA LEO MTANDAO HUKO INSTA


TCAA yapiga marufuku kununua, kurusha ‘drones’ bila kibali maalum

$
0
0
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imepiga marufuku urushwaji angani wa vifaa vya kieletroniki visivyo na rubani (drones) bila kupata kibali maalum.

Kupitia tangazo lake kwa umma, TCAA imesema kuwa kwa taasisi au mtu binafsi kufanya majaribio au kurusha drones, ni lazima apate idhini ya Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mamlaka hiyo.

“Ifahamike kuwa kuanzia sasa, taasisi au mtu binafsi anayetaka kununua, kufanya majaribio au kurusha angani vifaa hivyo visivyotumia rubani anapaswa kupata idhidi ya Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na kibali kutoka TCAA,” imeeleza taarifa ya Mamlaka hiyo.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari imefafanua kuwa uendeshaji wa shughuli zote za anga nchini uko chini ya Mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.

Tangazo hilo linakuja wakati ambapo kumekuwa na urushwaji wa drones unaofanywa na watayarishaji wa video za muziki kwa lengo la kuchukua picha za juu, pamoja na taasisi mbalimbali zinazochukua matukio husika hasa yanapofanyika katika maeneo ya wazi.

Drones zilitumika zaidi katika uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo mikutano ya kampeni za wanasiasa ilikuwa ikipigwa picha za juu kuonesha umati uliohudhuria.

TAZAMA FOMU YA PESA ZA ESCROW ALIZORUDISHA NGELEJA

$
0
0
Fomu ya Benki ya CRDB inayoonyesha Mbunge wa Sengerema William Ngeleja kurudisha fedha za Escrow milioni 40.4 alizopewa na Rugemalira.

Sababu za Ngeleja Kurejesha Fedha zabainishwa

$
0
0


MBUNGE wa Jimbo la Sengerema, William Ngeleja amesema moja ya sababu za kurudisha fedha za mgawo wa kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni kugundua aliyempa fedha hizo, amehusishwa na kashfa ya kuzipata kinyume cha sheria.

Waziri huyo wa zamani wa Nishati na Madini, amerudisha serikalini kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Sh milioni 40.4 alizopewa kama msaada na mfanyabiashara James Rugemalira wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd ya Dar es Salaam. Aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwamba alipokea fedha hizo bila kujua kuwa zilikuwa zinahusishwa na kashfa ya Tegeta Escrow kama ilivyo sasa.

Alisema fedha hizo alizipokea kwa nia njema kama msaada au mchango ili zimsaidie katika kutimiza majukumu yake ya kibunge hususan kusaidiana na wananchi wa jimbo lake kutekeleza shughuli za kijamii ikiwemo kujenga misikiti, makanisa na kusaidia wanafunzi wasiojiweza na kusaidia miradi ya maendeleo ambayo haipo kwenye Bajeti ya Serikali.

“Fomu ya tamko langu kama kiongozi wa umma kuhusu rasilimali na madeni kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka 1995 kwa kipindi kilichoishia Desemba 31, 2014 niliyoiwasilisha ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Desemba 24, 2014 ilijumuisha msaada huu,” alieleza. Aidha, Ngeleja alisema Januari 15, 2015 alilipa kodi kwa TRA kiasi cha Sh 13,138,125 ikiwa ni sawa na asilimia 30 ya msaada huo aliopewa kama ilivyoelekezwa na TRA.

“Nilipokea msaada huu kama wapokeavyo wabunge wengine kwa nia njema, bila kujua kwamba Rugemalira baadaye angekuja kuhusishwa na kashfa ya fedha za akaunti ya Escrow kama ilivyo sasa,” alisema Ngeleja akirejea kufikishwa mahakamani mwezi uliopita kwa Rugemalira na mshirika wake wa kibiashara, Habinder Sethi wakihusishwa na utakatishaji wa fedha hizo zilizotokana na Akaunti ya Tegeta Escrow.

Alisema ameamua kurudisha fedha hizo, kwa kuwa imedhihirika kwamba aliyempa msaada anatuhumiwa kwenye kashfa ya akaunti ya Escrow, hivyo amepima na kutafakari na hatimaye kuamua kwa hiari yake kurejesha fedha hizo serikalini bila kujali kwamba alishazilipia kodi ya mapato. “Nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa tu, kwa vile hajathibitika kupatikana na hatia, kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya kashfa na tuhuma hizi,” alieleza mbunge huyo na kuongeza: “Nina zaidi ya miaka kumi na miwili nikiwa kiongozi wa umma na pia niliwahi kuitumikia Wizara ya Nishati na Madini… lakini sijawahi kukumbwa na kashfa ya rushwa au ufisadi.

Kwa hiyo nimesononeka na kufadhaika sana kuona kuwa msaada niliopewa sasa unahusishwa na tuhuma.” Ngeleja alisema, “nimerudisha fedha hizi ili kulinda heshima na maslahi ya nchi yangu, chama changu CCM, serikali yangu, jimbo langu la Sengerema, familia yangu na heshima yangu mwenyewe.” Alisema kupokea msaada ni jambo la kawaida, ila ikibainika msaada unaopewa una harufu ya uchafu hata kama haujathibitishwa na vyombo husika ni vyema kujiepusha nao.

Pia alimpongeza Rais John Magufuli kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya kwa maslahi ya Taifa na kwamba anaungana na Watanzania wazalendo kumuombea kwa Mungu na kuahidi kuendelea kumuunga mkono kwa kupigania maendeleo ya nchi. Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu suala la makinikia, alisema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kina kwa kuwa lipo katika uchunguzi kwa sasa.

Maswali 5 Tata Kwa Ngeleja Baada ya Kutangaza Kurudisha Pesa za Escrow

$
0
0

Nikupongeze kwa hatua uliyoamua kuichukua ya kurejesha huo mgao wa Escrow......Lakini naomba ujibu haya maswali...

1.Ulichukua huo mgao kwa kazi gani?
2.Wewe na aliyekupa mlikua na mahusiano gani?
3.Kilicho kufanya urejeshe hizo fedha ni kipi? a) ni mali ya umma. b) Ulipokea kimakosa?
4.Je hizo fedha utarejesha kwenye akaunti ya nani?
5.Kutokana na swali la 3 upo tayari kutoa ushahidi mahakamani?

Tazama Kichupa kipya cha Vanessa Mdee - Kisela | Official Video | Ft. Mr. P ( P-Square )

Magazeti ya Leo Tanzania Jumamosi ya July 15,2017

Mahakama Yakataa Ombi la Kigogo wa Escrow Harbinder Singh Seth Kutibiwa Nje ya Nchi

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa ombi la Mawakili wanaomtetea mfanyabiashara Harbinder Singh Seth la kumruhusu mteja wao kwenda nje ya nchi kutibiwa uvimbe uliopo tumboni na badala yake apatiwe tiba kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili. 

Wakili wa kujitegemea, Alex Balomi aliifahamisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana kuwa Harbinder Singh Sethi anaumwa, hali yake imeendelea kubadilika na hii  ni wiki ya nne sasa  hawezi kupata usingizi.

Wakili Balomi aliiambia mahakama hiyo kuwa Sethi anasumbuliwa na uvimbe tumboni ambao unahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari.

“Kutokana na hali yake kuwa mbaya hii ni wiki ya nne sasa hawezi kupata usingizi hivyo anahitaji  ungalizi wa karibu wa madaktari  na kwamba wamebahatika kupata nyaraka kadhaa kutoka kwa daktari,” Balomi  aliifahamisha mahakama. 

Balomi aliongeza kuwa hata siku aliyokamatwa alikuwa akienda kwenye matibabu Afrika Kusini.

Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Leonard Swai  alisema  nyaraka ambazo Wakili Balomi anataka kuziwasilisha mahakamani hapo kuhusiana na Sethi hazijakidhi vigezo vya kisheria  na kwamba alitegemea daktari ambaye anamtibu angefika mahakamani kueleza hali  halisi ya ugonjwa husika.

Kutokana na hoja hizo,  Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alisema suala la ugonjwa si la kufumbiwa macho, linapaswa kuchukuliwa kwa uzito na kuelekeza magereza kufanya kila linalowezekana kuhakikisha hali ya mshtakiwa huyo inabaki katika hali nzuri na inapobidi wawasiliane na wataalam wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kesi imeahirishwa hadi Julai 28, 2017 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Katika kesi hiyo, Sethi na James Rugemalira wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola 22, 198,544.60 sawa na Sh 309,461,300,158.27.

Rufaa Vyeti Feki: 600 Wagonga Mwamba, 450 Warudishwa Kazini

$
0
0
Watumishi wa umma 450 walioondolewa kazini kutokana na kudaiwa kutumia vyeti vya kughushi wamerudishwa kazini baada ya kushinda rufaa zao.
Baada ya kutangazwa kwa Orodha ya watumishi wenye vyeti feki, 1050 walikata Rufaa huku  8800 wakiridhika na matokeo hayo.

Mbali na hilo, Serikali imesitisha mishahara kwa watumishi wa umma ambao walitakiwa kuwasilisha vyeti vyao kwa uhakiki lakini mpaka sasa hawajafanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk.Laurean Ndumbalo alisema watumishi hao wameshinda rufaa zao hivyo wataandikiwa barua za kurudishwa katika utumishi wa umma.

Alisema katika rufaa hizo, wengi walikuwa wanawake walioolewa na kubadili majina yao kwa kutumia ya waume zao.

“Kuna baadhi walitumia majina mawili alipokuwa kidato cha nne baadaye alilazimika kutumia matatu na kusababisha mkanganyiko hivyo tumejiridhisha na wanarudishwa katika utumishi wa umma,” alisema Dk. Ndumbalo.

Alisema Serikali pia imesitisha mishahara kwa watumishi wa umma ambao walitakiwa kuwasilisha vyeti vyao kwa uhakiki lakini mpaka sasa hawajafanya hivyo.

“Serikali imesitisha mishahara ya watumishi wote ambao muundo wa utumishi wao uliwataka kuwa na sifa ya kufaulu kidato cha nne wakati wanaajiriwa lakini hawakuwasilisha vyeti vyao kuhakikiwa na Baraza la Mitihani.

“Tunasitisha mishahara yao kuanzia mwezi Julai hadi hapo watakapowasilisha vyeti vyao kuhakikiwa,” alisema Dk. Ndumbalo.

Dk. Ndumbalo aliongeza kuwa kwa watumishi walioajiriwa wakiwa darasa la saba kabla ya waraka wa Utumishi wa Umma namba moja wa mwaka 2004 uliowataka waajiriwa kuwa na sifa ya kidato cha nne, wataendelea na kazi mpaka watakapostaafu.

Alisema sera ya Menejimenti na Ajira katika utumishi wa umma toleo la mwaka 1998 lilianza kutekelezwa Mei 20, 2004 hivyo kwa walioajiriwa kabla ya hapo warudishwe kazini kama waliondolewa kimakosa.

“Nasisitiza kuwa watumishi wote wa umma walioajiriwa kwa sifa ya elimu ya darasa la saba kabla ya Mei 20 hawahusiki na uhakiki wa vyeti vya kufaulu mtihani wa kidato cha nne na wataendelea kuwa watumishi wa umma katika vyeo vyao mpaka watakapostaafu kazi,” alisema Dk.Ndumbalo.

Aidha alisema serikali inatangaza ajira mpya 10,184 katika sekta mbalimbali huku ikitoa ajira 3,172 kwa sekta ya afya.

Profesa Jay Afunguka Wema Sepetu Kuikacha Harusi yake

$
0
0
https://media-mpasho.s3.amazonaws.com/wp-content/uploads/2015/12/Wema-Sepetu-1ed.jpg?x91596
BAADA ya Jumamosi iliyopita Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’ kufunga ndoa na mchumba’ke wa kitambo, Grace Mgonjo katika Kanisa la Mtakatifu Joseph lililopo Posta jijini Dar na sherehe kufanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, ameibuka na kufunguka suala la Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu kuikacha harusi yake.


Taarifa za awali kutoka kwa chanzo makini zilieleza kuwa, Profesa Jay na Wema ambaye alihamia Chadema miezi kadhaa iliyopita wana bifu kali japokuwa haijulikani chanzo ni nini, ndiyo maana mwanadada huyo hakuhudhuria kwenye harusi hiyo.

“Unajua Wema na Jay hawana uhusiano mzuri tangu ahamie kwenye chama hicho yaani wana bifu ndiyo sababu hata Wema hakuhudhuria kwenye sherehe ya harusi ya Jay maana wangekuwa sawa ungeona mbwembwe zake ukumbini lakini hakutokea,” kilidai chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Profesa Jay kwa njia ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp akiwa honeymoon ambapo mahojiano yalikuwa hivi;

Risasi Jumamosi: Hongera kwa kuoa na kuachana na ubachela Jay. Profesa
Jay: Asante sana, karibu.
Risasi Jumamosi: Kuna habari kuwa wewe na Wema mna bifu ndiyo maana hakuhudhuria hata kwenye harusi yako, hili likoje?
Profesa Jay: Jamani watu hawaishiwi maneno! Wema ni kamanda wangu tena tunahesh
imiana kwelikweli nisizuliwe bifu zisizokuwa na kichwa wala miguu.
Risasi Jumamosi: Kwa nini sasa hakuwepo au hukumwalika?
Profesa Jay: Mbona kuna watu wengi tu hawakuhudhuria kwa nini Wema? Mwacheni dada yangu apumzike, acha hizo stori. Profesa Jay kwa upande mwingine alieleza kuwa kesho Jumapili anatarajia kufanya sherehe kubwa kuliko ya mwanzo huko jimboni kwake Mikumi ambayo kila mwananchi atahudhuria kwani hakutakuwa na kadi na itafanyika uwanjani ikiwa ni shukrani kwao kwa kumchagua kuwatumikia

HAWA NDIO WAREMBO WALIOUTIKISA LEO MTANDAO

“Naomba Serikali ilegeze Kidogo ili Mashabiki Wangu Wafurahi Kwa Viuno na Chura Yangu” – Snura

$
0
0


Kama utakumbuka mwimbaji wa Bongofleva Snura aliwahi kuingia kwenye headlines baada ya video ya wimbo wake wa Chura kufungiwa na Serikali…sasa new stori ni kwamba ameiomba Serikali kulegeza kidogo baada ya video ya pili ya wimbo huo kupata mapokezi yasiyoridhisha.

Ayo TV na millardayo.com zimekaa na Snura na kusema:
”Video yangu ya Chura ya mara ya kwanza na video yangu ya pili niliyoifanya kimaadili kibishara, kiukweli imekwenda tofauti kwa sababu video yangu ya kwanza ilikuwa na kasi sana. Wengi tuliona walipost wakiwemo Don Jazzy mpaka meneja wa Lil Wayne.

“Kwa hiyo, ukiangalia video ya kwanza ilikuwa na kasi kuliko niliyoifanya ya pili. Naomba Serikali walegeze kidogo ili mashabiki zangu wafurahi kwani mashabiki wanapenda muziki wangu pia ukiangalia asilimia kubwa ya muziki ninaoufanya ni wa Kiswahili na lazima nioneshe viuno vyenyewe. Kwa hiyo Serikai watufikirie hilo.” – Snura.

Jike Shupa, Mamisa wa Young Dee Katika Bifu zito la Kugombania Bwana

$
0
0
MUUZA nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ na mzazi mwenza wa msanii wa Bongo Fleva, David Genz ‘Young D’, Mamisa Amir, wanadaiwa kuwa kwenye bifu zito kwa madai ya kuibiana mwanaume.


Chanzo makini kilidai kuwa, Mamisa ambaye awali alipojifungua alihifadhiwa na Jike Shupa, kwa sasa ni kama paka na panya, chanzo kikielezwa ni Mamisa kumpindua mwenzake kwa mwanaume wake japokuwa wenyewe wamekuwa wakifanya siri.


Baada ya kupata ubuyu huo, Risasi Jumamosi liliwatafuta wahusika ambapo lilianza na Mamisa ambaye alisema kuwa, hana tatizo na bishosti huyo na hata akikutana naye wanasalimiana.
Kwa upande wa Jike Shupa aligoma kuweka wazi huku akijiumauma na kusema: “Hata kama tuna bifu, ninyi kinawauma nini? Niacheni bwana.”

MASHABIKI WA SUNDERLAND BRADLEY LOWERY AZIKWA NA MAMIA YA WAINGEREZA

$
0
0
Mshabiki wa Sunderland Bradley Lowery (6) amezikwa leo na mamia ya mashabiki wa timu hiyo pamoja na wachezaji wa Sunderland wakionyesha masikitiko makubwa kwa kuondokewa na moja ya mashabiki wao wakubwa.Bradley alifariki Ijumaa wiki iliyopita baada ya kuugua saratani kwa muda.ambapo katika uhai wake alikuwa mshabiki mkubwa wa timu ya Sunderland na ilifikia kipindi baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakiongozwa na Jermain Defoe kwenda kumjulia hali katika hopsitali aliyokuwa amelazwa.Mchezaji Jermain Defoe, ambaye aliunda urafiki wa karibu sana na Bradley, aliungana na familia ya mvulana huyo kumuaga kwa mara ya mwisho.
Ibada ya wafu ilifanyika katika kanisa la Mtakatifu Yusufu kijijini mwao, wengi wakimsifu sana mvulana huyo kwa ukakamavu wake na sifa alizojilimbikizia.Bradley alikuwa anaugua ugonjwa ambao kwa Kiingereza hufahamika kama neuroblastoma - aina nadra ya saratani - tangu alipokuwa na umri wa miezi 18.Bradley alifanywa kuwa kibonzo-nembo wa klabu hiyo na akaunda urafiki wa karibu na mshambuliaji wa klabu hiyo Jermain Defoe.Aidha, aliongoza wachezaji wa England kuingia uwanjani Wembley wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania.
Bradley alipewa matibabu lakini saratani yake ikaibuka tena mwaka jana. Wahisani walichangisha zaidi ya £700,000 kulipia matibabu yake New York mwaka 2016, lakini madaktari waligundua kwamba saratani yake ilikuwa imeenea sana na haingeweza kutibiwa.
Wazazi wake Gemma na Carl, kutoka Blackhall Colliery, Durham, waliambia Desemba kwamba alikuwa amesalia na "miezi kadha tu ya kuishi".Miezi minne baadaye, walifahamishwa kwamba jaribio la mwisho kabisa la kumtibu lilikuwa limefeli.Bradley alipendwa na maelfu ya watu na alipokea kadi 250,000 za kumtakia heri wakati wa Krismasi mwaka jana, kutoka kwa watu mataifa ya mbali kama vile Australia na New Zealand.
Habari kwa hisani ya BBC Swahili.

Aliyekuwa Kocha wa Sunderland David Moyes katika msiba wa Bradley Lowery.
Ujumbe wa Bradley ukiwa umewekwa katika moja ya barabara

Shule 10 za Mwisho matokeo ya kidato cha sita

$
0
0
Ni kilio na kicheko. Hivyo ndivyo tutakavyoweza kusema, kwani matokeo ya kidato cha sita, yaliyotangazwa leo Jumamosi, Julai 15 yamezitaja shule kumi zilizofanya vibaya na kushika mkia kitaifa.

Shule hizo ni Kiembesamaki Unguja, Hagafilo (Njombe), Chasasa (Pemba), Mwenyeheri Anuarite (Dar es Salaam) na Ben Bella (Unguja).

Nyingine zilizotajwa kushika mkia ni Meta (Mbeya), Mlima Mbeya(Mbeya)

 Nyingine ni Shule ya Sekondari ya Al-Ihsan Girls (Unguja na St Vicent(Tabora).

Matokeo Kidato cha Sita : Wasichana Waongoza kwa Kufaulu

$
0
0
Matokeo ya kidato cha sita nchini  yalitolewa leo Jumamosi, Julai 15, yameonyesha kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo  kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21).

Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.

Kwa upande wa watahiniwa wavulana,  waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya  46,385.

 Taarifa iliyotolea inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (asilimia 93.72) walipata daraja la kwanza hadi la tatu. Kati ya hao, wasichana ni 22, 909 na wavulana ni 35,647.

 “Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa walipata daraja la 1-11  umepanda  kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016 hadi 93.72 mwaka huu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza;

 “Pia, ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda ikilinganishwa na wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07 ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana.”

 Ufaulu wa masomo
Kadhalika taarifa hiyo imeonyesha kuwa ufaulu kwa watanikiwa wa shule kwa upande wa masomo, ya Sayansi, Biashara, Lugha na Sanaa, haukuonyesha tofauti kubwa ukilinganisha na mwaka jana.

Hata hivyo, ufaulu katika somo la General Studies umeshuka kwa asilimia 7.54 kutoka asilimia 71. 24 hadi 63.70.

Wanafunzi 10 Wafutiwa Matokeo Kidato cha Sita

$
0
0
Wakati matokeo ya mitihani ya kidato cha sita yakitolewa leo, Jumamosi Julai 15, imebainika kuwa watahiniwa 10 walifutiwa matokeo kwa makosa ya kufanya udanganyifu.

 Taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta),  Dk Charles Msonde imeeleza kuwa kati ya watahiniwa hao kumi, saba ni wa shule na watatu ni wa kujitegemea.

 Pamoja na hao kumi, matokeo ya watahiniwa wengine 15 yalizuiliwa kwa kuwa hawakufanya mitihani ya baadhi ya masomo.

 Watahiniwa hao walishindwa kufanya mitihani kutokana na matatizo mbalimbali ikiwamo ya kiafya na hivyo kushindwa kufanya baadhi ya mitihani hiyo.

‘Watahiniwa hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kidato cha sita, Mei 2018 kama wa watahiniwa wa shule,” imesema taarifa ya Dk Msonde.

Pia, wapo watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani hiyo, Mei 2018.

Shule 10 Bora Matokeo Kidato cha 6

$
0
0
Matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2017 yametoka leo Jumamosi, Julai 15 huku shule ya Wasichana ya Feza Girls ikiibuka kinara kwa watahiniwa wake 67 kufaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili.

Shule nyingine zilizoibuka kidedea katika matokeo hayo ni Marian Boys, iliyoshika nafasi ya pili, Kisimiri (Arusha) imeshika nafasi ya tatu na Ahmes (Pwani) imeshika nafasi ya nne.

 Shule nyingine  ni  Marian  Girls (Pwani) iliyoshika nafasi ya tano, Mzumbe (Morogoro) nafasi ya sita, St Marry Mazinde Juu (Tanga) nafasi ya saba, Tabora Boys (Tabora) nafasi ya nane, Feza BOYS (Dar es Salaam) nafasi ya tisa na Kibaha ya Pwani iliyoshika namba kumi.

TAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2017 YAMETOKA BOFYA HAPA KUYAONA

Jerry Muro Apigwa Chini Yanga

$
0
0

KATIBU Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, jana amemtambulisha rasmi, Dismas Ten kuwa Ofisa wa Habari wa klabu hiyo. Kabla ya utambulisho huo, Dismas alikuwa ofisa habari wa Mbeya City ya Mbeya ambayo pia inashiriki Ligi Kuu Bara kama Yanga.

Hii ina maana kuwa, Yanga haitakuwa tena na aliyekuwa ofisa wa habari wake, Jerry Muro ambaye hivi karibuni alimaliza kifungo chake cha kufungiwa mwaka mmoja alichopewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Jerry alifungiwa na Kamati ya Maadili ya TFF, chini ya mwenyekiti
wake, Wakili Wilson Ogunde kwa kosa la kudharau uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkwasa alisema amemtambulisha Dismas baada ya ofisa huyo kumaliza mkataba wake wa miaka minne Mbeya City. “Nichukue nafasi hii kumtangaza
Dismas kuwa ndiye ofisa wetu wa habari mpya atakayefanya kazi pamoja na Chicharito (Godlisten).

“Hiyo yote ni katika kukiboresha kitengo chetu cha habari cha Yanga ili kifanye kazi yake vizuri ndani ya klabu yetu,” alisema Mkwasa.
Viewing all 7853 articles
Browse latest View live