↧
MAGAZETI YA LEO TANZANIA JUMAPILI JULY 9,2017
↧
Mbunge wa Mikumi Prof Jay auaga ukapera afunga ndoa kanisa la St Joseph Dar

↧
↧
Jeshi La Polisi Laua Watu 6 Jijijini Mwanza.......Ni Majambazi Hatari Yaliyokuwa Yametoroka Kibiti Na Kuingia Mwanza
Majambazi sita wameuawa kwa kupigwa risasi sehemu mbalimbali za miili yao na Jeshi la Polisi baada ya kutokea majibizano ya risasi kati ya polisi na majambazi hao na kupatikana silaha moja aina ya AK 47 na nyingine nne zilizotengenezwa kienyeji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea usiku wa Julai 8, 2017, katika mtaa wa Fumagila mashariki kata ya Igoma wilaya ya Ngamagana mkoani Mwanza baada ya kupokea taarifa kwa kwamba baadhi ya watu wanaofanya uhalifu katika mkoa wa Pwani wilaya ya Kibiti na Rufiji wamekimbilia mkoani humo wakijipanga kutengeneza vikundi vya kufanya uhalifu.
Kamanda Msangi amesema katika ufuatiliaji walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye katika mahojiano alikiri kuhusika na tukio la unyang'anyi kwa kutumia silaha, kisha alitoa ushirikiano kwa askari ambapo aliwapeleka hadi eneo la Fumagila ambapo alidai wenzake wamejificha eneo hilo, ghafla majambazi hao walikurupuka na kuanza kuwarushia askari polisi risasi.
Aidha, kutokana na umahiri wa askari hao waliweza kujibu mashambulizi na kufanikiwa kuwauwa majambazi sita huku wengine wawili wakifanikiwa kutoroka eneo la tukio lakini polisi walifanikiwa kukamata silaha kadhaa na vitu vingine.
Pamoja na hayo, DCP Msangi amesema hakuna askari aliyejeruhiwa kwa risasi wala kupoteza maisha katika tukio hilo huku akisisitiza kuwa ufuatiliaji wa kusaka na kuwatia nguvuni waliotoroka bado unaendelea.
Shuhuda wa tukio hilo, ambaye ni diwani wa Kata ya Kishili iliyo jirani na kata hiyo, Sospeter Ndumi amesema kurushiana risasi baina ya watu hao na polisi kulianza usiku wa manane hadi majira ya jana asubuhi.
Amesema katika majibizano hayo polisi walifanikiwa kuwaua watu hao na kukamata silaha mbalimbali za kivita walizokuwa wanazitumia.
Katika mtaa huo huo ndipo lilipotokea tukio la Desemba 3 mwaka jana ambapo polisi waliwakamata watoto 11 wenye umri unaokadiriwa kuwa na miaka sita hadi 14 baada ya kuizingira nyumba moja kwa lengo la kuwakamata watu waliowahisi kuwa majambazi.
Mmoja kati ya watu watatu waliokutwa kwenye nyumba hiyo alikimbia baada ya kuwarushia polisi bumu la mkono, kabla ya polisi kuwadhibiti waliosalia kwa kushirikiana na wananchi wa mtaa huo.
Kadhalika katika tukio hilo, watu watatu waliosadikiwa kuwa ni majambazi waliuawa na bunduki mbili aina ya SMG na AK47, magazine saba, bastola moja na risasi 183 vilikamatwa na polisi.
Baada ya polisi kuondoka katika eneo hilo, wananchi waliiteketeza nyumba hiyo kwa moto.
↧
BODI YA MIKOPO KUTANGAZA SIFA NA VIGEZO VITAKAVYOTUMIKA KUWAPANGIA WANAFUNZI MIKOPO 2017/2018

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema hivi karibuni itatangaza sifa na vigezo vitakavyotumika kuwapangia wanafunzi mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 unaotarajia kuanza miezi michache ijayo.
Ufafanuzi huo umetolewa jana (Ijumaa, Julai 7, 2017) jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Dk Cosmas Mwaisobwa wakati akijibu maswali ya baadhi ya wateja waliotembelea Banda la HESLB katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere ambako HESLB inashiriki katika Maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara.
“Tunakamilisha mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka ujao wa masomo na tumepanga kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Julai tuwe tumeutangaza na tumefungua mtandao wetu ili waombaji wenye sifa waombe,” alisema Dk Mwaisobwa.
Dk Mwaisobwa amewataka waombaji wa mikopo watarajiwa wawe watulivu na kufuatilia kwa karibu vyombo vya habari na tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) ambayo huwa na kiunganishi (link) cha mfumo wa kuombea mkopo.
Awali, katika maonesho hayo, baadhi ya wananchi wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu wamepata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali yakiwemo tarehe ambayo Bodi itaanza kupokea maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
Maswali mengine yaliyoulizwa ni kama utaratibu wa udahili kupitia vyuoni moja kwa moja utaathiri upatikanaji mikopo, wengine walitaka kupata elimu zaidi kuhusu taratibu za urejeshaji wa mikopo.
Akifafanua kuhusu maswali hayo, Dkt. Mwaisobwa alisema Sheria iliyoanzisha HESLB, pamoja na mambo mengine, inamtaka mnufaika kuanza kurejesha mkopo wake miezi 24 baada ya kuhitimu masomo.
Mkurugenzi huyo wa HESLB alisema kuwa sheria hiyo inamtaka mwajiri yeyote kuwasilisha kwa HESLB majina ya waajiriwa wake wote ambao ni wahitimu wa taasisi za elimu ya juu ndani ya siku 28 baada ya kuwaajiri na Bodi itamjulisha kama ni wanufaika au hapana pamoja na utaratibu na kiwango cha kumkata mnufaika.
Dk Mwaisobwa aliwataka wananchi kutembelea banda la HESLB kwa kuwa Bodi ya Mikopo itaendelea kuonyesha shughuli zake kwenye banda lake lililopo ndani, Banda la Benjamin Mkapa (Namba 19&20) hadi mwisho wa maonyesho hayo, tarehe 13 Julai, 2017.
↧
LULU AWEKA REKODI SERIKALI YA JPM

Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’
IMEVUJA! Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’, anatajwa kuwa ndiye staa pekee wa kike Bongo aliyeweka rekodi katika utawala wa Serikali ya Rais Dk.John Pombe Magufuli ‘JPM’ baada ya hivi karibuni kumfanyia kufuru ya fedha msanii mwenzake, Muhsein Awadh ‘Dk. Cheni’.
Chanzo kilichokuwa eneo la tukio kililieleza Risasi Jumamosi kuwa, Lulu alifanya kufuru hiyo miezi kadhaa iliyopita katika harusi ya shemeji wa Dk. Cheni iliyofanyika Msasani Tower jijini Dar ambapo Lulu alimtuza Dk. Cheni fedha nyingi, yaani noti za elfu kumikumi zisizo na idadi hali iliyomsababisha jamaa huyo na mkewe kushindwa kuzishika mikononi na kuziweka kwenye bahasha kubwa ya kaki.
Dk. Cheni
“Pamoja na Magufuli kukaba kila kona na mastaa wenzake kufulia, lakini Lizy (Lulu) ana jeuri kama kawa. “Kiukweli kwa fedha alizommwagia Dk. Cheni, inaonekana yupo vizuri sana kifedha kuliko wasanii wengine maana siyo kwa kufuru aliyomfanyia Dk. Cheni mpaka wageni waalikwa wakabaki wamepigwa na butwaa. Watu walibaki wakijiuliza anapata wapi fedha kiasi hicho ukizingatia hali ya maisha ni ngumu sana katika utawala huu wa JPM,” kilidai chanzo.
Baada ya kupata ubuyu huo na kunasa video inayomuonesha Lulu akimtuza minoti mingi Dk. Cheni na mkewe, Risasi Jumamosi lilimtafuta Dk. Cheni ili kumsikia kauli yake kwamba alijisikiaje ambapo alisema alijisikia furaha sana.
“Ile ilikuwa ni harusi ya shemeji yangu ambayo ilifanyika pale Msasani Tower, kwa kweli nilifurahi sana Lulu kututuza mahela yale maana mtu ukipewa zawadi siku zote lazima ufurahi,” alisema Dk. Cheni.
Uchunguzi wa Risasi Jumamosi ulionesha kuwa, Lulu, tofauti na wasanii wengine wanaolia maisha magumu, amekuwa akifurukuta kwenye utawala huu kwa kufanya kufuru kwani licha ya kuonekana akimtuza Dk. Chenipia amekuwa akipigilia pamba za gharama kiasi cha kuwafanya watu kuhoji, anazichota wapi pesa za kufanyia kufuru?
↧
↧
Hii hapa Orodha ya wagombea wa TFF waliyochujwa katika usahili.......Jamal Malinzi Kaondolewa
Jumamosi ya July 8 2017 kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka Tanzania TFF ilikutana kwa mara ya kwanza baada ya kuvunjwa na kuundwa upya na kikao cha kamati ya utendaji ya TFF.
Baada ya kikao kumalizika na kufanya usahili wa wagombea wa nafasi zote na kuchuja, orodha ya wagombea waliyochujwa nafasi ya Urais ni pamoja na Rais wa sasa wa TFF Jamal Malinzi ambaye ameondolewa kwa sababu yuko Rumande
↧
Prof Jay Ameyasema Haya Baada ya Kufunga Ndoa
Msanii wa muziki, Professor Jay amefunga ndoa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph la Posta jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 08, 2017 na mpenzi wake wa siku nyingi Grace Mgonjo.
Cherekochereko za tukio kubwa la Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule almaarufu Profesa Jay limetikisa Jiji La Dar baada ya kufuatiliwa na watu wengi. Ndoa ya Profesa Jay na mpenzi wake wa muda mrefu.
Kabla ya ndoa hiyo iliyoibua shangwe kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofurika kanisani hapo, msafara wa kuelekea kanisani ulianzia nyumbani kwa Profesa Jay, Kimara-Temboni jijini Dar.
Ndoa hiyo ilifuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo waalikwa walipata nafasi ya kula, kunywa hadi kusaza huku shughuli nzima ikipambwa na mahudhurio ya mastaa kibao wa Bongo.
Cherekochereko za tukio kubwa la Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule almaarufu Profesa Jay limetikisa Jiji La Dar baada ya kufuatiliwa na watu wengi. Ndoa ya Profesa Jay na mpenzi wake wa muda mrefu.
Kabla ya ndoa hiyo iliyoibua shangwe kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofurika kanisani hapo, msafara wa kuelekea kanisani ulianzia nyumbani kwa Profesa Jay, Kimara-Temboni jijini Dar.
Ndoa hiyo ilifuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo waalikwa walipata nafasi ya kula, kunywa hadi kusaza huku shughuli nzima ikipambwa na mahudhurio ya mastaa kibao wa Bongo.
“Namshukuru Mungu nimetimiza ahadi ya ndoa kwa mchumba wangu ambaye tumepitia mabonde na milima,” alisema Profesa Jay baada ya kutoka kanisani hapo.
↧
HUYU NDIYE MREMBO ALIYEUTIKISA MTANDAO LEO HUKO INSTAGRAM

↧
DR WA VICHAA NI MTAALAMU BINGWA WA TIBA ASILIA.ANAPATIKANA MOROGORO MJINI,MTAA WA MKUNDI SHELI
+255 712 528 623
HUDUMA ANAZOZITOA
1.KUTOA MAJINI MWILINI NA KUTOA VITU MAJUMBANI
2.KUSAFISHA NYOTA NA KUPANDISHA
3.KUPATA KAZI KWA HARAKA NA KUPANDISHWA CHEO
4.KESI SUGU ZISIZOISHA
5.KUTIBU KIZAZI(KUPATA MTOTO)
6.KUTOA VIFUNGO MWILINI NA KINGA YA MWILI
7.KUTIBU KICHAA
8.KUMRUDISHA ALIYEPOTEA
9.NGUVU ZA KIUME KUKOSEKANA
10.VIDONDA VYA TUMBO
11.KUTIBU SUKARI
12.KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA KWA MUME AU MKE
13.DAWA ZA BIASHARA NA ZINDIKO LA NYUMBA
MENGINEYO UTAYAJUA UTAKAPOFIKA OFISINI KWETU
KARIBUNI SANA WATEJA
KARIBUNI SANA WATEJA
↧
↧
TANZIA:MKE WA MC ELLY NGWALA TAUSI AMEFARIKI DUNIA

Tunategemea kuupumzisha mwili wa Mke wangu Tausi siku ya kesho Jumapili ktk Makaburi ya Ukonga Kinyerezi
Ratiba nzima ya Mazishi ni kuanzia saa 3;00 Asubuhi na tunategemea kufika Kanisani muda wa SAA 7:00 KANISA lipo Ukonga Majumbasita
Ukitokea Airport nenda mbele Kwa kuelekea Ukonga Banana,mbele kdg kwenye Mataa (Trafic Light)ni njia panda ya kuelekea SEGEREA.
Elekea kulia vuka reli elekea kushoto nenda na Lami kisha fuata njia ya vumbi pembeni ya reli utaliona Kanisa la Moravian.
Elekea kulia vuka reli elekea kushoto nenda na Lami kisha fuata njia ya vumbi pembeni ya reli utaliona Kanisa la Moravian.
Lakini ukitaka kufika Nyumbani kwenye Msiba Kabla hauja vuka reli,kata kulia fuata Barabarani ya vumbi pembeni ya reli utauona Msiba Nyumbani Kwa Wazazi wangu Kwa mzee Mwaifwani.
Barikiwa unapoianza Safari.
Elly Hezron Mwaifwani.
MC ELLY NGWALA.
0713404646/0767404647
MC ELLY NGWALA.
0713404646/0767404647
Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Amen.
Amen.

↧
BOOK NOW MC DR CHENI CALL +255 713 620 865 +255 754 222 201

Moja ya sherehe ambayo Dr cheni alikua MC
Mahsein Awadh Said Maarufu kwa jina la Dr cheni katika tasnia ya filamu ambaye kwa sasa pia ni MC Mshereheshaji wa sherehe kama harusi na matukio mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
Call now these numbers for booking
Mc Dr Cheni
+255 754 222 201Admin: Lewis Mbonde
Tigo: +255 658 194 194
↧
Magazeti ya Leo Tanzania Jumanne July 11,2017
↧
LADY JAY DEE KAYASEMA HAYA BAADA YA PROFESSOR JAY KUFUNGA NDOA

Kuhusu hilo Lady Jaydee amesema, “Kwanza nimpongeze Prof Jay kwa hatua aliyochukua, ni hatua nzuri katika maisha kwa sababu kwanza ni kuzaliwa, pili ni kuoa au kuolewa na ya tatu ni kufa, kwa hiyo hii ni harusi ya pili katika maisha yake nimpongeze sana kwa uamuzi alioufikia,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza.“Nimtakie kila la kheri katika maisha yake ya ndoa yenye furaha na mafanikio. Professor kama kaka yangu na kama rafiki yangu ni mambo mengi tumepitia pamoja, tumeweza kusapotiana katika kazi na mambo mengine, kwa hiyo ni furaha kwangu, si kama msanii mwenzake bali kama mwanafamilia,” ameeleza Lady Jaydee.
Professor Jay na Lady Jaydee wamesharikiana katika nyimbo nyingi kama vile Kikao cha Dharura, Bongo Dar es Salaam, Niamini na Joto Hasira.
↧
↧
Ngeleja arudisha fedha za mgao wa ESCROW Millioni 40.4 alizopokea Disemba 2, 2014.

Ngeleja amezungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu, Julai 10, na kueleza kuwa fedha hizo zipatazo Sh 40.4 milioni tayari ameshazikabidhi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Fedha hizo ni sehemu ya Sh 306 bilioni zilizochotwa kwenye akauti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kwa pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kampuni ya kufua umeme ya IPTL wakati wakisubiri mzozo wa kimkataba baina yao uliokuwa mahakamani umalizike.
Fedha hizo ziligawiwa kwa wanasiasa akiwamo Ngeleja ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, majaji, wabunge na viongozi wa dini.
Ngeleja amesema ameamua kuzirudisha fedha hizo baada ya Rugemalira kuhusishwa na kashfa ya akaunti hiyo ya Escrow.
"Nilipokea msaada huo kama wapokeavyo wabunge wengine, ilikuwa ni msaada ambao nilipewa kwa ajili ya jimbo langu bila kujua kwamba Rugemalira baadaye angekuja kuhusishwa na kashfa ya fedha, za akaunti ya Escrow."
"Nimepima na kutafakari na hatimaye nimeamua kwa hiari yangu kurejesha serikalini fedha zote nilizopewa kama msaada bila kujali nilishazilipia kodi ya mapato," amesema.
Amesema ameamua kurudisha fedha hizo hata kama aliyempa msaada bado ni mtuhumiwa.
"Ninarudisha fedha hizi ili kulinda heshima na maslahi mapana ya nchi, chama, Serikali, jimbo langu la Sengerema, familia yangu na heshima yangu mwenyewe,"amesema.
===>
↧
Mtangazaji wa E-FM ‘Bikira wa Kisukuma’ afariki dunia
Tasnia ya habari nchini imepata pigo kwa kumpoteza mtangazaji maarufu wa kituo cha redio cha E-FM, Seth Katende maarufu kama ‘Bikira wa kisukuma’ aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kituo hicho cha redio kimeeleza kuwa Katende alipoteza maisha baada ya kuugua kwa muda mfupi.
“Kwa masikitiko makubwa E FM inapenda kuwajulisha kuwa mwenzetu Seth Katende maarufu” Bikira wa kisukuma”amefariki dunia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi.Seth atakumbukwa sana kwa ucheshi wake kupitia kipindi cha Ubaoni alichokua akiendesha sambamba na Imma Kapanga na Mpoki au “mwarabu wa Dubai”.Msiba upo nyumbani kwa baba yake mzazi Changanyikeni Dar es salaam,” ilieleza taarifa ya E-FM.
Katende alianza kupata umaarufu kupitia mtandao wa Instagram akitumia jina la ‘Bikira wa Kisukuma’ akichambua mada mbalimbali za maisha zilizowagusa wengi hususan vijana.
Umaarufu wa marehemu uliongezeka mara dufu baada ya kuanza kusikika kupitia kipindi cha Ubaoni cha E-FM kutokana na ucheshi wake na jinsi alivyokuwa akiwasilisha mada mbalimbali.
↧
ZARI AOGA MATUSI BAADA YA KUPOST HIKI INSTAGRAM

↧
Haya ndio Makosa Makubwa Tunayofanya Wanaume Katika Mapenzi

Mimi ni mwanaume, nimeoa ila kwa sasa mke wangu na mtoto wako mkoa mwingine na mimi mkoa mwingine kikazi.
Familia yangu naipenda sana na huwa nawapatia kila aina ya mahitaji mara ninapoambiwa kuna upungufu fulani wa mahitaji, hata kama sina hela niko tayari kukopa mahali lakini siyo mke wangu kwenda kukopa kwa watu. Kuna sababu kuu mbili za kutokuruhusu mwanya wa mke wangu kukopa: Moja, ni kuruhusu mwanya wa kutongozwa na hao watakaomkopesha (kama ni wanaume). Pili, inatengeneza umbea, majungu na unafiki usio na msingi especially akina mama.
Hivi karibuni kuna jamaa yangu tunafahamiana naye, naye yuko mbali na mkewe japo huja walau mara moja kwa mwezi au miezi miwili hivi, then hurudi kwenye biashara na kazi zake. Mke wake amekuwa akinisumbua sana mara kwa mara, huniomba nimkopeshe pesa. Wakati fulani nilimpa, akanirudishia. Mara ya pili akanikopa tena, muda wa kulipa ulipofika akaniambia kuwa Mr. amempigia simu kuwa bado hajapata hela, hivyo afanye atakaloweza kurekebisha mambo nyumbani. Akaniomba nimkopeshe tena, basi nikawa mpole tuu, nikaipotezea maana haikuwa hela kubwa (30,000).
Baada ya muda, akanisihi tena nimsaidie mama yake anaumwa anatakiwa aende kwao (Nauli 40,000/-) akanisihi kuwa Mr. atatuma hela wiki ijayo. Nikampa akaenda, alipofika huko dada yake akafariki ikawa ni msiba huku mama akiwa mgonjwa. Nikampa pole. Aliporudi sikudai ile 40,000/- nikijua alipatwa na matatizo, acha iwe msaada.
Baada ya wiki ananiambia Mr. anasema kuna mtu alikuwa anamdai laki 4, ametokomea na simu haipatikani. Akawa ananiuliza kuwa nimshauri afanyeje maana hata matumizi hana. Kisaikolojia ni kwamba alitaka nimsaidie tena, nikampa 10,000/-. Hiyo hali ikaendelea kidogo kidogo hivyo hivyo.
Siku moja alinitumia msg kuwa nimpigie kuna kitu anataka kuniambia. Nilipompigia alinishukuru kwa yote niliyomsaidia. Kwenye mazungumzo baadaye akaniambia njoo tulale, nikashtuka. Akaanza kunisemesha kwa sauti ya mahaba. Mwishowe uvumilivu ukamwishia, akapasua jipu. Anahitaji kuwa na mimi. Ameniambia hawezi kuvumilia tena, na amedhamiria liwalo na liwe lazima awe na mimi anipe tunda nilifaidi kama shukrani. Nilikata simu na tangu hapo nimejikuta kama vile nimelewa mawazo nimekuwa na hali ya kuchanganyikiwa kimawazo. ananitumia message za mapenzi kibao, japo mimi nimeamua kutokujibu message hizo.
Najua fika, mke wa mtu ni sumu. Lakini hoja yangu ni kuwa haya yote yasingetokea kama huyu mumewe angekuwa responsible na familia yake. Inakuwaje mtu akae miezi miwili mbali na familia yake na hatumi hela kwa visingizio vya kubanwa au kukosa hela? Sijui wadau, naombeni comment zenu hatua za kuchukua haraka at least to rescue the situation. Sisemi kuwa mimi nina hela sana, maana katika maisha kuna wakati wa kupata na kuna wakati wa kukosa, na inapotokea umekosa, wewe mwanaume fanya juu chini, bora ukope wewe mwanaume mtajuana na mdeni wako, lakini hawa wanawake ni viumbe dhaifu, ni rahisi kuingia majaribuni. Mimi sijamtongoza huyu dada na sijawahi kumtamkia mambo ya mapenzi lakini mwenyewe kalianzisha. Sasa mambo yakiharibika nani alaumiwe?
↧
↧
PICHA:HARMONIZE AKIJIACHIA NA MPENZI WAKE WA KIZUNGU
↧
HALI YA SHUMIMILETA YADAIWA KUWA TETE UGHAIBUNI

Shumileta
MWIGIZAJI wa kitambo Bongo, Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’ au ‘Shumi’ anadaiwa kuwa na hali tete ya kimaisha nchini India kufuatia kile kilichotajwa kuachana na bwana’ke aliyekuwa akiishi naye, raia wa Nigeriahivyo kwa sasa anatafuta msaada wa kurejea nyumbani, Tanzania.
Akizungumza na Wikienda, mmoja wa marafiki wa karibu na Shumileta ambaye pia ni msanii wa filamu za Kibongo alisema kuwa, alipata taarifa za masaibu hayo ya Shumileta kutoka kwa mmoja wa wanafamilia yake na kwamba wako kwenye mipango ya kumsaidia arejee nyumbani kuendelea na maisha.
“Ndugu wako kwenye hatua za mwisho kuhakikisha wanamsaidia kurudi nyumbani,” alisema ‘kikulacho’ huyo.
Wikienda liko kwenye msako mkali wa kuwatafuta ndugu wa msanii huyo ili kujiridhisha juu ya madai hayo kuhusu ndugu yao na kila kitu kikikamilika, tutarejea hapa kukujuza kuhusu hali ya Shumi.
↧
HAYA NDIO MADHARA YA KUJICHUBUA
Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango,hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao.

Mtu anaeyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba,Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito,kutokwa na mabaka, pumu, kupata watoto wenye kasoro, kupata matatizo ya akili, kuharibika kwa ini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika krimu,Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa)Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na mengine hujitokeza kadri mtu anavyotumia ving´arisha ngozi.
↧