↧
Magazeti ya Leo Jumapili ya July 16,2017
↧
TANZIA: Mke wa Waziri Mwakyembe Afariki Dunia
↧
↧
Haya hapa Magazeti ya Leo Jumatatu ya July 17,2017
↧
Rais Magufuli Ampa Pole Mwakyembe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe kufuatia kifo cha mkewe Bi. Linah George Mwakyembe kilichotokea usiku wa tarehe 15 Julai, 2017.
Bi. Linah George Mwakyembe amefariki dunia katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katika salamu hizo, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na kusikitishwa na kifo hicho, na amesema yeye na familia yake wanaungana na familia ya Dkt. Mwakyembe katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
“Nakupa pole sana Dkt. Mwakyembe kwa kuondokewa na mkeo mpendwa Bi. Linah, natambua hisia za maumivu ulizonazo wewe na familia nzima, nyote nawaombea Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
"Namuombea Marehemu Linah George Mwakyembe apumzishwe mahali pema peponi, Amina” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
↧
Rais Magufuli Alivyoshiriki Ibada na kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa Chato
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli jana alisali Ibada ya Jumapili ya 15 ya mwaka wa Kanisa iliyofanyika katika Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita na kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.
Katika harambee hiyo Mhe. Rais Magufuli ambaye aliongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli alifanikiwa kuchangisha fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni 13, ahadi Shilingi 920,000/=, mifuko ya saruji 33 na malori 2 ya mchanga.
Mhe. Rais Magufuli aliwapongeza waumini wa Parokia ya Chato kwa hatua kubwa waliyopiga katika ujenzi wa kanisa kuu la Parokia hiyo na amewataka kuendelea kujitolea kukamilisha hatua za mwisho za ujenzi huo.
↧
↧
JE Wewe ni Mpenzi wa Kuvaa Mitumba? Basi Hili Hapa Linakuhusu

Waziri Kassim Majaliwa amesema safari ya Watanzania kuachana na nguo za mitumba imewadia kutokana na uwepo wa viwanda vya kutengeneza nguo nchini.
Waziri Mkuu alisema hayo jana wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Namera kilichoko Gongo la Mboto na kiwanda cha nguo cha Nida kilichopo Ubungo Dar es Salaam ambapo alidai viwanda vya kutengeneza nguo nchini ni ushahidi tosha kwamba nchi iko njiani kuondokana na matumizi ya nguo za mitumba kwa kuwa nguo nyingi zitakuwa zinatengenezwa nchini, hivyo kupatikana kwa bei nafuu.
Mbali na hilo Waziri Mkuu aliwapa matumaini wakulima wa pamba na kusema hawana sababu ya kwenda kuuza nje ya nchi na badala yake wauze pamba hiyo katika viwanda vya ndani ili vizalishe nguo za kutosha zitakazouzwa nchini kwa gharama nafuu.
“Pamba yote inaweza kuchakatwa nchini, hivyo hakuna haja ya kuiuza nje ya nchi. Natoa wito kwa wakulima wetu wa pamba walime mazao ya kutosha kwa sababu soko la uhakika lipo na hii ndio safari ya mwisho ya mitumba Tanzania" alisema Waziri Mkuu
Mbali na hilo Waziri Mkuu alitoa wito kwa wamiliki wa viwanda vyote nchini kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi waishio katika maeneo ya karibu na viwanda hivyo sambamba na kulipa kodi kwa wakati na kwa viwango sahihi.
Kwa mujibu wa Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alisema kuwa Tanzania imeazimia kufikia mwaka 2018 kuachana na biashara ya kuingiza nguo za mitumba kutoka nje, makubaliano ambayo yalifikiwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
↧
Huyu ndiye Binti Aliyeongoza Matokeo ya Kidato cha Sita 2017

amesema amepania kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na kwamba kiu yake kubwa ni kuonana na Rais John Magufuli ili amshike mkono kwa nia ya kumpongeza.
Aidha, kinara wa masomo ya mchepuo wa Lugha na Sanaa, ambaye ni wa EGM (Uchumi, Jiografia na Hisabati), Francis Samkyi wa Shule ya Feza Boys ya jijini Dar es Salaam, alisema amefurahi kutimiza lengo la mtihani huo na kwamba sasa nia yake ni kutimiza ndoto yake ya kuwa mtaalamu wa masuala ya fedha.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana mjini Zanzibar na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk. Charles Musonde, Sophia alikuwa kinara wa masomo ya sayansi, akifuatiwa na Agatha Ninga wa Tabora Girls ya Tabora na Nathaniel Ndagiwe wa Mzumbe ya Morogoro.
Samkyi aliibuka kidedea katika masomo ya lugha na sanaa, akifuatiwa na Jophary Ernest na Andrea Nkondo, wote wa Ilboru ya Arusha.
Katika orodha hiyo ya wanafunzi waliong’ara kwa kila mchepuo, Rajabu Ali Mabaranga wa shile ya Kibaha mkoani Pwani aliongoza katika msomo ya biashara, akifuatiwa na Gasto Theobalo Kimaro wa Umbwe ya Kilimanjaro na Rashid Abdallah wa Tusiime ya jijini Dar es Salaam.
SOPHIA ALIVYOMTAJA JPM
Sophia amehitimu shule ya sekondari St. Mary’s Mazinde Juu iliyopo Lushoto mkoani Tanga, akisomea mchepuo wa PCB (Fizikia, Kemia na Bailojia).
Pia ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wanne wa familia ya Richard Tadeo na Joyce Ezra, wakazi wa Pasiansi wilayani Ilemela, mkoa wa Mwanza ambao shughuli zao kuu ni uvuvi.
Kabla ya kwenda kwenye mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Kambi ya Msange mkoani Tabora, ambako kwa sasa ndipo alipo, Sophia aliwaahidi wazazi wake, kwamba mwaka huu atatenda maajabu yatakayompa fursa ya kushikana mkono na rais Magufuli.
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, mama wa Sophia, Joyce Ezra, alisema licha ya kumsomesha mtoto wao kwa shida ikiwamo kukopa fedha kila mara ili wamlipie ada, matokeo hayo yaliyotangazwa na NECTA na mwanawe (Sophia) kuongoza kitaifa katika masomo ya sayansi, wanaona wazi kwamba amewatendea haki na pia kutimiza kile alichowaahidi.
“Kila tulipokuwa tunaenda kukopa fedha, tulimuonyesha na kumwambia tumekopa fedha, tusije tukafungwa bure… jitahidi maana tulijinyima na hata wakati mwingine kulala njaa ili mtoto wetu asome,” alisema Joyce.
“Mara kwa mara amekuwa akituambia kwamba anataka kuwa daktari bingwa wa moyo ili aweze kutibu watu. Lakini kikubwa zaidi ni kwamba mwaka huu alijitabiria kuwa mwanafunzi bora na kwamba naamini kwa kufanya hivyo atapata fursa ya kuonana na kupeana mkono na Rais John Magufuli,” alisema mama huyo wa Sophia jana.
Kwa kawaida, wanafunzi wanaofanya vizuri katika mitihani ya taifa hupata nafasi ya kwenda bungeni na kupongezwa huku pia wakitunukiwa zawadi mbalimbali.
Akimuelezea Sophia, mama huyo alisema kuwa alisoma katika Shule ya Msingi Mwenge iliyopo Mwanza, kisha kusoma sekondari shule ya wasichana Visitation iliyopo Moshi mkoa wa Kilimanjaro.
Baba wa Sophia, Richard, alisema kumsomesha mtoto wa kike kuna manufaa makubwa na siri nyingine ni kwamba, ni rahisi kwao kutimiza malengo wanaposimamiwa kwa karibu kwa sababu mara nyingi huwa wasikivu.
“Wazazi wawekeze katika elimu, hasa kwa mtoto wa kike. Sikubaliani na usemi wa baadhi ya watu wanaosema kuwa kusomesha mtoto wa kike ni hasara.
Mtoto wa kike ni msaada na huwezi kupoteza. “Tena ni wasikivu sana. Kwakweli tunamshukuru Mungu mwanetu kupata matokeo mazuri kwa kiwango tusichotarajia,” alisema Richard, ambaye aliongeza kuwa amekuwa akijihusisha na uvuvi kwa zaidi ya miaka 20.
Alisema hivi sasa wanamsubiri kwa hamu Sophia ili wampokee kwa furaha wakati atakaporejea nyumbani akitokea kwenye mafunzo ya JKT, Agosti 8 mwaka huu.
ALICHOSEMA SAMKYI
Akizungumza na Nipashe jana, Samkyi alisema ndoto zake siku zote ni kuwa mtaalamu aliyebobea wa masuala ya fedha. Kwa sababu hiyo, Samkyi alisema kuwa alitenga muda wake mwingi kila siku akiwa likizo nyumbani au shuleni akijisomea na pia alimtanguliza Mungu kwa maombi ili amuongoze katika kile anachokipigania.
“Sikutarajia kushika nafasi hii kitaifa, kwa kuwa katika darasani tulikuwa wanafunzi 35 na wote hao kwakweli wako vizuri sana.
Hivyo ushindani ulikuwa mkubwa , haikuwa kazi rahisi,” alisema Samkyi. Baba na mama wa Samkyi, Thomas na Victoria, walisema kuwa walitarajia mtoto wao kufanya vizuri kwa kuwa siku zote, tangu akiwa shule ya msingi alikuwa akishika nafasi ya kwanza.
“Lakini haijawahi kutokea katika familia mtoto kuongoza kitaifa, labda kimkoa… tunamshukuru Mungu kwa matokeo haya,” alisema baba wa Samkyi, akiungwa mkono na mkewe.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Feza, Simon Albert, alisema shule yao imempatia Samkyi ufadhili wa masomo ya Chuo Kikuu nje ya nchi na zawadi ya iPad.
“Kwa kawaida wanafunzi 10 bora hupewa scholarship (ufadhili wa masomo) pamoja na kompyuta. Lakini zaidi wanakuwa wanatamani kwenda bungeni.. wanajua wakishinda, wataitwa bungeni,” alisema Mwalimu Albert.Nipashe
↧
Inasikitisha Sanaa:Muuguzi Amchoma Binti Sindano ya Usingizi na Kisha Kumbaka huko Igunga
Muuguzi anayefanya kazi Kituo cha Afya Kata ya Igurubi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Damian Mgaya (26) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kumbaka binti wa miaka 18 mkazi wa kitongoji cha Mwagala B, Kijiji cha Mwagala.
Mtendaji wa Kata ya Igurubi, Ntemi James alisema uhalifu huo umefanyika Julai 14, mwaka huu saa 8 hadi alfajiri wakati binti huyo akimuuguza mama yake, Tatu Simbi ambaye amelazwa katika kituo hicho cha afya baada ya kushambuliwa kwa kipigo na mume wake.
James alidai mtuhumiwa alimpokea mama wa binti huyo akiwa hoi na ndipo alimpatia matibabu kisha kumlaza katika kituo hicho cha afya huku akimchoma sindano ya usingizi ambayo ilisababisha mama huyo kupitiwa na usingizi.
Mtendaji huyo alidai kuwa muuguzi Damian alipoona mama wa binti huyo amelala, alimwambia waende wote chumba kingine ili akachukue dawa ya mama yake; lakini hata hivyo hakumpa dawa na badala yake alimwambia amchome sindano ili asipate maradhi kwa kuwa mazingira ya hospitali sio mazuri.
Baada ya kuambiwa hivyo, binti huyo alikubali kuchomwa sindano mbili na alipochomwa sindano ya kwanza aliishiwa nguvu na alipochomwa sindano ya pili alianguka na kupitiwa na usingizi hadi asubuhi.
Alisema baada ya kuona amelala pasipokuwa na fahamu, muuguzi huyo alianza kumbaka hadi alfajiri alipoamshwa na mama yake huku yeye akiwa hajitambui kutokana na maumivu aliyokuwa akiyasikia sehemu zake za siri na mwili wote.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bonaventura Kalumbete alithibitisha kubakwa kwa binti huyo na muuguzi huyo na kueleza kuwa baada ya kupata taarifa hiyo, alituma timu ya wataalamu ambayo ilibaini binti huyo kubakwa na amelazwa kwenye kituo hicho na hali yake ni mbaya kwani hawezi kutembea.
Aidha, Dk Kalumbete alisema uchunguzi wa awali unaonesha binti huyo alichomwa sindano wakati alikuwa hata haumwi na hizo dawa nazo zimechangia kumsababishia kushindwa kutembea huku akiahidi kuwa baada ya uchunguzi, muuguzi huyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mkuu wa Wilaya ya Igunga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, John Mwaipopo alikiri kukamatwa kwa muuguzi baada ya kupokea taarifa ya kubakwa kwa binti huyo, alimwagiza Mkuu wa Polisi Igunga kumkamata muuguzi huyo Damian Mgaya ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
↧
PICHA HIZI MPYA ZA HAMISA MABETO ZAWA GUMZO MTANDAONI
↧
↧
KIMENUKA....Aliyetobolewa Macho na Scorpion Aanza Kugawana Mali na Mkewe
WAKATI lile sakata Linalomuhusu kijana Said Mrisho aliyetobolewa macho na mtu aitwaye, Salum Njwete ‘Scorpion’ kumtelekeza mkewe, Stara Sudi ‘Mama D’ na watoto wanne, likiwa bado bichi, jipya jingine limeibuka ambapo wawili hao wameanza kugawana mali.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Maji-Chumvi, Tabata-Kimanga jijini Dar, zikiwa zimekatika siku chache tangu Stara apangishiwe nyumba na Said kisha jamaa huyo kwenda kuishi na mwanamke mwingine mwenye asili ya Kiarabu.
Akizungumza na Wikienda, Stara alisema kuwa amefi kia uamuzi huo wa kuchukua kilicho chake baada ya kutelekezwa kwenye nyumba hiyo.
Ujue mwanzoni tulikubaliana na Said na akamuomba mwenye nyumba kuwa atakuwa akilipia kodi miezi mitatu-mitatu, lakini mama yangu akakataa, akasema muongo huyo, atakukimbia na kwamba kwa nini kwangu alipie miezi mitatu na kule (kwa mke mwingine) alipie miezi tisa? Said akadhani nitajua amesafi ri ili awe anakuja kwa siri kuchukua vitu kidogokidogo,” alisema Stara.
Kwa upande wake, Said alisema kuwa, alikubaliana na hatua aliyoichukua Stara ya kuchukua vitu vyote ikiwemo friji, makochi na vingine vingi, jambo lililofanywa mbele ya mashahidi akiwemo mwenye nyumba.
Nashangaa kuambiwa kuwa nimetelekeza familia, hivyo ni visingizio ambavyo mwenzangu amewahi kwenda kwenye media na kuongea bila kusikiliza upande wangu,” alisema Said na kuongeza:
STORI: MWANDISHI WETU | IJUMAA WIKIENDA| DAR
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Maji-Chumvi, Tabata-Kimanga jijini Dar, zikiwa zimekatika siku chache tangu Stara apangishiwe nyumba na Said kisha jamaa huyo kwenda kuishi na mwanamke mwingine mwenye asili ya Kiarabu.
Akizungumza na Wikienda, Stara alisema kuwa amefi kia uamuzi huo wa kuchukua kilicho chake baada ya kutelekezwa kwenye nyumba hiyo.
“Amenitelekeza, nitakaa vipi hapa… nimeamua kuchukua vitu na kupeleka nyumbani kwetu. Nimekaa hapa kwa siku nne tu, nimekuja kuchukua malipo yangu ya miezi mitatu.
Ujue mwanzoni tulikubaliana na Said na akamuomba mwenye nyumba kuwa atakuwa akilipia kodi miezi mitatu-mitatu, lakini mama yangu akakataa, akasema muongo huyo, atakukimbia na kwamba kwa nini kwangu alipie miezi mitatu na kule (kwa mke mwingine) alipie miezi tisa? Said akadhani nitajua amesafi ri ili awe anakuja kwa siri kuchukua vitu kidogokidogo,” alisema Stara.
Kwa upande wake, Said alisema kuwa, alikubaliana na hatua aliyoichukua Stara ya kuchukua vitu vyote ikiwemo friji, makochi na vingine vingi, jambo lililofanywa mbele ya mashahidi akiwemo mwenye nyumba.
“Nilikuwa ninatoa pesa vizuri, ilifi ka kipindi nikamwambia akatafute nyumba ya laki moja, akaenda kutafuta ya shilingi laki moja na nusu, nikalipia kwani niliomba kulipia miezi mitatumitatu.
Nashangaa kuambiwa kuwa nimetelekeza familia, hivyo ni visingizio ambavyo mwenzangu amewahi kwenda kwenye media na kuongea bila kusikiliza upande wangu,” alisema Said na kuongeza:
“Nilipigiwa simu na mwenye nyumba kuwa amepaki kila kitu kwenye gari, anahama na ameshapeleka barua Ustawi wa Jamii (Ilala) kuwa ninahitajika siku ya Jumatatu (leo) na kwamba kiasi cha kodi kilichokuwa kimelipwa (laki nne na nusu) arudishiwe kwani ndiyo kwanza amekaa miezi minne.Nilifi ka na kufanya makabidhiano mbele ya mwenye nyumba.”
STORI: MWANDISHI WETU | IJUMAA WIKIENDA| DAR
↧
MFANYABIASHARA Maarufu Kenya Kuzikwa Katika Jeneza la Dhahabu na Lisilopitisha Risasi
Aliyekuwa mfanyabiashara na mwanasiasa Kenya, Marehemu Nicholas Biwott kuzikwa katika jeneza la dhahabu na lisilopitisha risasi...
Imefanyika hivyo kutokana na maagizo yake aliyotoa kabla ya kifo chake ambapo alidai ana maadui wengi ambao wanaweza kumwinda hata akiwa kaburini....
Former Powerful Minister, Nicholas Biwott, will be buried in a gold bullet proof coffin to protect him from enemies.
In a will, Biwott said even in death enemies would be all over him. He therefore demanded that he be buried inside a bullet proof coffin so as to scare away people aimed at him. He also told his beloved ones to bury him in a golden coffin, to symbolize his social status.
The tycoon’s coffin has been ordered from USA after it was established that a casket of this nature could not be found in Kenya. Anytime this week the coffin will arrive in the country under maximum security.
Biwott was a man who constantly feared everyone and anyone. He was afraid of death. A secretive man, the former Minister never allowed any person near his compound unless iit was a close family member. Even in death, it was his wish to be protected.
↧
MGAWO wa PESA za Escrow wa Kina Chenge ni Bajeti ya Wizara hii
MGAWO waliopata wabunge, maofisa wa serikali na viongozi wa dini kutoka kwa watuhumiwa wakuu wa kashfa ya uchotwaji wa mabilioni ya akaunti ya Tegeta Escrow unatosha bajeti ya mwaka mzima ya miradi ya maendeleo ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nipashe imegundua.
Katika miaka mitatu iliyopita ya bajeti (2014/15, 2015/16 na 2016/17), wizara hiyo ambayo kwa sasa iko chini ya Waziri Dk. Harrison Mwakyembe, ilitengewa bajeti ya Sh. bilioni tatu kila mwaka, ikiongoza wizara zote 18 kwa kuwa na bajeti ndogo zaidi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Wakati wizara hiyo ikiambulia Sh. bilioni moja (theluthi ya bajeti yake ya maendeleo) hadi inapofika robo tatu ya mwaka wa bajeti katika miaka hiyo mitatu, imebainika Sh. bilioni 4.77 zinazodaiwa zao la kashfa ya uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow walizopatiwa wabunge, maofisa wa serikali viongozi hao wa dini zingelitosha kugharamia kikamilifu miradi ya maendeleo ya wizara hiyo kwa mwaka mzima na 'chenji' ya Sh. bilioni 1.7 ikabaki.
Katika mwaka uliopita wa fedha, kwa mfano, kati ya Sh. bilioni tatu zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wizara hiyo, ni Sh. bilioni 1.19 tu (asilimia 40) ndizo zilizokuwa zimetolewa hadi Aprili 30, mwaka huu kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe.
Kiasi hicho cha fedha hakifikii hata mgawo waliopata Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani, Andrew Chenge na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa zamani, Prof. Anna Tibaijuka kwenye mgawo huo unatokana na uchotwaji wa fedha za akaunti ya Tegeta Escrow mwaka 2014. Wawili hao waliripotiwa kupata mgawo wa Sh. bilioni 1.6 kila mmoja.
Miradi ya maendeleo ambayo Wizara ya Habari ilipanga kutekeleza mwaka uliopita wa fedha ni Programu ya Urithi na Ukombozi wa Bara la Afrika ambayo hadi Aprili 30, mwaka huu, ulikuwa umepokea Sh. milioni 30.324 badala ya Sh. milioni 700 na mradi wa Ujenzi wa Ukumbi wa Wazi wa Maonyesho ya Sanaa ambao ulikuwa haujapokea hata senti licha ya kuidhinishiwa na Bunge Sh. milioni 800.
Miradi mingine ni Ukarabati wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo uliokuwa umeidhinishiwa Sh. milioni 300, lakini hadi Aprili 30, mwaka huu, ulikuwa umepokea Sh. milioni 100 na Ujenzi wa eneo la Changamani la Michezo uliopokea Sh. milioni 60 kati ya milioni 100 zilizoidhinishwa na Bunge.
Miradi mingine ya maendeleo ya wizara hiyo iliyopaswa kutekelezwa mwaka jana ni Habari kwa Umma ulioidhinishiwa Sh. milioni 100, lakini haukupatiwa hata senti na mradi wa Upanuzi wa Usikivu TBC ambao ulipatiwa fedha zote, Sh. bilioni moja zilizoidhinishwa.
ILIANIKA MAJINA
Mgawo wa fedha za akaunti hiyo pia ni karibu nusu ya fedha ambazo serikali imetumia kufanya ukarabati wa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Uwanja huo umekarabatiwa na Kampuni ya Beijing Construction ya China kwa gharama ya Sh. bilioni 10.
Katika ripoti yake iliyowasilishwa kwenye kikao cha 18 cha Bunge la 10, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilianika majina ya maofisa wa serikali, wabunge na viongozi wa dini waliopata mgawo wa fedha zinazohusishwa na kashfa hiyo.
Watu hao walipewa fedha hizo na Mkurugenzi wa VIP Engineering na mmiliki mwenza kwa kampuni ya IPTL, James Rugemalira.
Mkurugenzi huyo na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Power African Power (T) Limited (PAP), Seth Sigh wako mahabusu kwenye Gereza la Keko jijini baada ya kukosa dhamana walipofikishwa mahakamani na Takukuru mwanzoni mwa mwezi wakikabiliwa na mashtaka 12 ikiwamo ya kugushi, utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya dola za Marekani milioni 22.1 na Sh bilioni 309.4 kwa serikali.
Mbali na Chenge na Prof. Tibaijuka, wengine waliopata mgawo huo ni ofisa katika Ofisi ya Rais wakati huo, Shabani Ngurumo aliyepewa Sh. milioni 80, Jaji wa Mahakama Kuu aliyejiuzulu, Eudes Ruhangisa Sh. milioni 404.25, aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco), Dk. Enos Bukuku Sh. milioni 161.7 na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), ambaye Jumatatu iliyopita alirejesha serikalini Sh. milioni 40.4 alizopewa.
Katika ripoti hiyo Waziri wa Nishati na Madini wa serikali ya awamu ya tatu, Daniel Yona, Mbunge wa zamani wa Sumbawanga
Mjini, Paul Kimiti, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emmanuel Ole Naiko na aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Aloisius Mujulizi walitajwa kupatiwa Sh. milioni 40.4 kila mmoja.
Wengine ni ofisa wa TRA, Lucy Apollo Sh. milioni 80.8, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mkuu wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita), Philip Saliboko Sh. milioni 40.2, maaskofu Methodius Kilaini Sh. milioni 80.9 na Eusebius Nzingirwa Sh. milioni 40.4, Padri Alphonce Twimannye Sh. milioni 40.4, maofisa wa Rita Placidus Luoga Sh. milioni 121.2 na Theophil Rugozobwa Sh. milioni 323.4.
↧
HAWA NDIO WAREMBO WALIOUTIKISA LEO MTANDAO
↧
↧
Mwanza: Mwalimu Afumaniwa Akifanya Mapenzi na Mwanafunzi Wake Darasani
Mwalimu Abasi Hussein wa shule ya msingi Mwabomba iliyopo tarafa ya Ngula wilayani Kwimba mkoani Mwanza anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukutwa darasani akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 17.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo mkoani humo na kusema mpaka sasa mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 27 anashikiliwa na jeshi la polisi muda wowote upelelezi ukikamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
"Babu wa mwanafunzi alipoona mjukuu wake amechelewa kurudi nyumbani alianza kufanya msako, alikwenda kwenye shule ya sekondari lakini hakumuona ikabidi aendelee kumtafuta mjukuu wake, ilipofika kwenye muda wa saa sita na kitu alikwenda kwenye shule ya msingi ya Mabomba katika moja ya darasa wakakuta huyo mwanafunzi wa kike akifanya mapenzi na mwalimu wa shule hiyo ya msingi ya Mwabomba"alisema RPC Msangi
Msangi aliendelea kuelezea jinsi babu alivyoweza kuwakamata watu hao
"Yule babu alikuwa ameongozana na watu wengine hivyo walipowaona waliwakamata wakaita na watu wengine, baadaye taarifa zilifika kituo cha polisi na polisi walikwenda na kuwakuta watuhumiwa hao kwenye lile darasa hivyo wakawachukua na kuwafikisha kituoni, hivyo mtuhumiwa yupo kituo cha polisi tunaendelea na mahojiano na taratibu nyingine za kiupelelezi zinaendelea ili tuweze kukamilisha upelelezi tuweze kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo" alisisitiza Msangi
Mbali na hilo Kamanda Msangi ametoa onyo kwa watu wanaojihusisha na mapenzi na watoto chini ya miaka 17 na kusema huenda awe amekubali mwenyewe hilo ni kosa la ubakaji hivyo amewataka kuacha na kusema kufanya vitendo hivyo ni sawa na kuhitaji kwenda jela miaka 30.
↧
FLORA Mbasha: Mwanaume Kama Hakuridhishi Kiunyumba Haina Haja ya Kuendelea nae
↧
Mbunge Mlinga afafanua hoja ya Diamond kujengewa sanamu
Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Mh Goodluck Mlinga amezidi kutetea hoja yake ya kuwa wasanii waliofanya vizuri na kuiwakilisha nchi nje vizuri, kupewa heshima kama kujengewa sanamu na baadhi ya mitaa na barabara kupewa majina yao.

Kipindi cha nyuma Mbunge huyo alisimama Bungeni na kusema kwa namna msanii Diamond Platnumz anavyoiwakilisha nchi vizuri kimataifa anastahili kujengewa sanamu, na kupendekeza ikibidi sanamu la askari posta Dar es Salaam liondolewe na kuweka hilo la Diamond.
“Na sikumtaja Diamond pekee, niliwataja wasanii wengi kama wakina Mr Nice ambao wameiwakilisha Tanzania sana nje lakini mpaka leo hii wamepotea hawana alama, inakuwa hawawezi kuwahamasisha wasanii wengine, lakini tunapoweka alama kila msanii anapofanya vizuri tunahamasisha wengine na ndiyo utaratibu katika nchi za wenzetu,” ameiambia Habari Xtra ya Times Fm na kuongeza.
“Kuna mchezaji mmoja wa mpira alitoka Kenya (Victor Wanyama) kuja Tanzania siku ya pili alipewa mtaa, sasa vile vitu ndio tunatakiwa tuvifanye kwa wasanii wetu wanaoibeba nchi. Sasa wewe fikiri mtu katoka nje ambaye anawakilisha nchi nyingine tunampa mtaa, lakini kwetu ni msanii gani alishawahi kuacha alama hata akapewa Barabara, hakuna!!!,” amemaliza kwa kusema.
By Peter Akaro
↧
MHENGA ANASWA JUU YA UNGO LIVE AKIWANGA MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMANNE JULY 18,2017
↧
↧
Ebitoke : Ben Pol Ananipenda Kama Nilivyo
Msanii wa vichekesho Anastazia Kisaveli alimaarufu kama Ebitoke ameweka wazi jambo ambalo anavutiwa zaidi na Ben Pol na kusema ni vile msanii huyo alivyompenda na kumkubali jinsi alivyo.
Ebitoke ambaye inadaiwa anatoka kimapenzi na Ben Pol amesema hayo kupitia kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio kinachoruka kila Jumamosi na kudai Ben Pol hakumtenga wala kumdharau kutokana na kazi yake hiyo bali alimkubali na kumuhakikishia kumpa support katika kazi yake hiyo ili afanikiwe zaidi na zaidi.
"Kuna watu wananitisha kweli wanakuja 'DM' wengine wananitukana, wengine hivi wewe Ebitoke unaweza kuwa na Ben Pol? Hivi mimi wananionaje hawa watu wasinichukulie poa poa.
"Tunachotarajia sasa Ben Pol kwanza lazima anipe 'support' kwa kila kitu nachokifanya na mimi lazima nihakikishe natimiza malengo yangu kwa sababu amesema atanisapoti kuanzia kazi yangu nayofanya mpaka mbeleni kwa hiyo huyo ni mwanaume wa kweli kwangu, ambaye amekubali kazi yangu nayofanya, amenikubali jinsi nilivyo hajanibagua nimefurahi sana aliposema kuwa lazima anipe nguvu kutumiza malengo yangu" alisema Ebitoke
Mbali na hilo Ebitoke anasema kuna mambo mengi yeye na Ben Pol wameyapanga na anaamini kuwa yatatimia mbele ya safari katika maisha yao ya kila siku, ila anasema kaka zake yeye walimjia juu kuona hizo stori za mahusiano na Ben Pol lakini baadaye walielewa kuwa anachofanya ni kutafuta maisha hivyo ilibidi wamuache na kazi yake hiyo ya uigizaji na kuendelea kumpa 'Support'
↧
TRA Yamkana Ngeleja Sakata la fedha za Escrow........Yadai Jukumu Lake ni Kupokea Kodi na Sio Fedha za Kashfa
Waziri wa Nishati na Madini wa zamani Ngeleja ni mmoja kati ya watu waliopokea mgawo wa fedha zinazodaiwa kuwa zao la kashfa ya Tegeta Escrow, lakini akatangaza kuzirejesha kwa TRA Jumatatu iliyopita.
Februari 2014, Ngeleja ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Sengerema (CCM) aligaiwa Sh. milioni 40.4 na mfanyabiashara maarufu James Rugemalira ambaye mwanzoni mwa mwezi alifikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka 12, yakiwamo ya kughushi na utakatishaji fedha.
Hata hivyo, wakati Ngeleja akithibitisha kwa risiti mbele ya waandishi wa habari kuziingiza fedha hizo katika akaunti ya TRA, mamlaka hiyo imesema haizitambui. TRA imesema haina mpango wowote wa kufuatilia fedha hizo kwa sababu shughuli yake ni kukusanya kodi.
Akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa TRA, Richard Kayombo alisema mamlaka hiyo inahusika na kuhakikisha serikali inakusanya kodi stahiki na siyo urejeshaji wa fedha za kashfa kama Escrow.
Kayombo alitoa ufafanuzi huo wakati alipoulizwa na Nipashe juu ya utaratibu rasmi uliopo wa urejeshaji wa fedha hizo endapo wanufaika zaidi wa mgawo wa Rugemalira watataka kufuata nyayo za Ngeleja.
Akifafanua zaidi juu ya suala hilo, Kayombo alisema TRA haihusiki na fedha zilizochotwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kwa kuwa hazikuwa mali yake.
Aidha, Kayombo alisema TRA haiwezi kuzizungumzia fedha hizo kwa kuwa hazijawahi kuwa mali yake na kuelekeza watafutwe wenye fedha hizo kwa ufafanuzi zaidi.
“Fedha za Escrow zinaihusu vipi TRA? Tunawezaje kukaa na kuzungumzia fedha ambazo si zetu?” Alisema Kayombo. “Mimi nashauri watafutwe wenyewe wazungumze kama wanataka kurejesha… siyo sisi.”
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu aliiambia Nipashe wiki iliyopita kuwa uamuzi wa Ngeleja kupeleka fedha za hizo TRA unazua maswali zaidi kwa kuwa alipewa na Rugemarila, na viongozi wa awamu ya nne ya serikali walisema siyo za umma bali mtu binafsi.
Lakini akizungumza jijini Jumatatu iliyopita Ngeleja alisema amerejesha mgawo huo kwa TRA kwa kuwa pamoja na sababu nyingine, ili kujiweka kando na kashfa.
Alisema aliyetoa mgawo huo ameshakamatwa na Takukuru na ana kesi inayoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Huku akionyesha stakabadhi ya malipo ya Benki ya CRDB tawi la Tower, Ngeleja alisema pia “nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa, kwa vile hajathibitika kupatikana na hatia, kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya kashfa au tuhuma hizo.”
“Nimesononeshwa na kufadhaika sana kuona kuwa msaada niliopewa sasa unahusishwa na tuhuma.”
Alisema alipokea mgawo huo Februari 12, 2014 na Januari 15, 2015 alilipa kodi kwa TRA kiasi cha Sh. 13,138,125 ikiwa ni sawa na asilimia 30 ya msaada huo aliopewa.
Hakusema ni kwa nini ulipita muda mrefu kati ya kupokea na malipo ya kodi.
Baada ya Ngeleja kurejesha fedha hizo palikuwa na wito kutoka kwa wanasiasa na wanaharakati waliotaka wote waliopata mgawo huo kurejesha fedha hizo kwa TRA kama alivyofanya waziri huyo wa zamani.
MASHTAKA 12
Rugemalira na mwenzake, mmiliki wa Kampuni ya Pan African Power (PAP), Harbinder Singh Sethi walisomewa mashtaka 12 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Julai 3.
Mashtaka hayo ni pamoja na ya kugushi, utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya dola zaMarekani milioni 22.1 na Sh. bilioni 309.4 kwa serikali.
Novemba 26, 2014, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliwasilisha mjini Dodoma ripoti ya uchunguzi wa kashfa Tegeta Escrow ambapo ilisema Sh. bilioni 306 zilichotwa kutoka Benki Kuu kinyume cha sheria.
Mwenyekiti wa kamati hiyo wakati huo, Zitto Kabwe alisoma ripoti na kulithibitishia Bunge kwamba viongozi na wafanyakazi wa Serikali, wafanyabiashara, viongozi na taasisi za dini, mabenki na watu binafsi walihusika katika ufisadi.
Ripoti ya PAC ilianika orodha ya waliopata mgawo huo kuwa mbali na Ngeleja ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani, Andrew Chenge ambao kila mmoja alipata Sh. bilioni 1.6.
Wengine ni ofisa katika Ofisi ya Rais wakati huo, Shabani Ngurumo aliyepewa Sh. milioni 80, Jaji wa Mahakama Kuu, Eudes Ruhangisa alipata Sh. milioni 404.25 na aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco), Dk. Enos Bukuku, aliyepewa Sh. milioni 161.7.
Katika ripoti hiyo Waziri wa Nishati na Madini wa serikali ya awamu ya tatu, Daniel Yona, Mbunge wa zamani wa Sumbawanga Mjini, Paul Kimiti, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emmanuel Ole Naiko na Jaji wa zamani wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Aloisius Mujulizi walitajwa kupatiwa Sh. milioni 40.4 kila mmoja.
Wengine ni ofisa wa TRA, Lucy Apollo Sh. milioni 80.8, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita), Philip Saliboko Sh. milioni 40.2, maaskofu Methodius Kilaini Sh. milioni 80.9 na Eusebius Nzingirwa Sh. milioni 40.4, Padri Alphonce Twimannye Sh. milioni 40.4, maofisa wa Rita Placidus Luoga Sh. milioni 121.2 na Theophil Rugozobwa Sh. milioni 323.4.
BAJETI WIZARA
Mgawo waliopata wabunge, maofisa wa serikali na viongozi wa dini kutoka kwa Rugemalira unatosha bajeti ya mwaka mzima ya miradi ya maendeleo ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nipashe imegundua.
Katika miaka mitatu iliyopita ya bajeti (2014/15, 2015/16 na 2016/17), wizara hiyo ambayo kwa sasa iko chini ya Waziri Dk. Harrison Mwakyembe, ilitengewa bajeti ya Sh. bilioni tatu kila mwaka, ikiongoza wizara zote 18 kwa kuwa na bajeti ndogo zaidi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Wakati wizara hiyo ikiambulia Sh. bilioni moja (theluthi ya bajeti yake ya maendeleo) hadi inapofika robo tatu ya mwaka wa bajeti katika miaka hiyo mitatu, imebainika Sh. bilioni 4.77 zinazodaiwa zao la kashfa ya uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow walizopatiwa waheshimiwa hao zingetosha kugharamia kikamilifu miradi ya maendeleo ya wizara hiyo kwa mwaka mzima na ‘chenji’
ya Sh. bilioni 1.7 ikabaki.
Katika mwaka uliopita wa fedha, kwa mfano, kati ya Sh. bilioni tatu zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wizara hiyo, ni Sh. bilioni 1.19 tu (asilimia 40) ndizo zilizokuwa zimetolewa hadi Aprili 30, mwaka huu kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe.
Chanzo: Nipashe
↧
NAFASI za Kazi Zilizotangazwa Leo
↧