SIKU zote ubuyu wa Zanzibar unahitaji mate mengi ili uumungunye sawia na uzuri wake ni kwamba haukinaishi! Muuza sura (video queen) ambaye hivi karibuni jina lake limekua kwa kasi baada ya kujiingiza kwenye Bongo Fleva, Lulu Augen ‘Amber Lulu anadaiwa kuvutishwa madawa ya kulevya ‘unga’.
↧
MREMBO AMBER LULU ADAIWA KUVUTISHWA UNGA
↧
FAHAMU MAANA YA BRAND NA NAMNA UNAVYOWEZA KUJI-BRAND
Na Lewis Mbonde +255 658 194194
Kama unataka kuanzisha biashara, au umekwisha anzisha, basi hii mada inakuhusu. Na hata unataka kuajiriwa au unatafuta kazi bora zaidi uliyonayo, ni jambo la msingi kujua namna ya kuwa na Brand inayouzika.
Maana ya Brand
Branding ni namna ya kutengeneza HISIA chanya mbele za hadhira. Ni namna unavyotaka wafikirie na waitambue bidhaa husika au asasi.
Mfano ukisikia Dr Cheni unapata picha kuwa ni msanii mkongwe katika kiwanda cha filamu ambaye anaelimisha na kuburudisha jamii. Ndio kusudio lake kuu.
Kuna mengi ya kufanya ili kujenga hisia hizo- jinsi unavyowasiliana na hadhira , huduma kwa wateja, aina ya bidhaa zako, uwajibikaji wako kiutendaji n.k
Hii sio maana ya Brand
Brand sio rangi , sio logo(nembo), sio jina la bidhaa. , bali ni nini vitu kama hivyo vina leta hisia na vinasadia kufanikisha lengo la uwepo wa bidhaa/asasi au mtu husika.
Kwanini unahitaji kuwa na Brand
Kama tulivyoona katika maana ya Brand, lengo kuu la Brand ni kufanikisha kukubaliwa mbele ya wale unaowalenga, hivyo basi unahitaji Brand ili kujiwezesha kupata kazi bora unayoihitaji kwani kwa picha nzuri utakayoijenga kwa jamii , unaweza kupata watu watakaotaka kufanya nawe kazi.
Pia Brand inakusaidia pale unapotaka kuanzisha biashara , au kama tayari unayo biashara basi inakurahisishia kuuza bidhaa zako nyingine mpya.
Brand inakufanya ujenge mtandao na watu wa muhimu katika fani yako, ajira na biashara.
Je unatengeneza Brand yako ?
Kwanza kabisa inabidi ujijue unapenda kufanya nini na nini utakachotoa kwa jamii kama bidhaa. Mfano kama lengo lako ni kutoa huduma za michezo mfano mpira wa miguu, basi utajikita katika kujifunza kwa undani kuhusu mambo ya mpira wa miguu, kushiriki katika michezo na kushare habari za kina kuhusu mpira wa miguu.
Hata hivyo haitoshi tuu kuonekana upo fiti katika hicho bidhaa yako , bali pia uwafanye watu wengine wapende kuwa karibu nawe. Hapa ndipo kazi ya ziada inahitaji katika namna yako ya kufanya mawasiliano.
Kumbuka mawasiliano ni zaidi ya unachozungumza, hata namna ya mavazi yako, lugha yako, umakini wako, tafakari zako, jinsi ulivyo wa msaada, mtandao wako n.k vyote vitakusaidia kujitengeneza kama BRAND.
Jitokeze ufahamike
Kujifunza na kuwa na kitu cha maana cha kutoa kwa jamii hakutoshi kama haujafahamika na kuanza kujenga Brand. Tafuta nafasi ya kuzungumza na makundi ya watu unaowalenga.
Tumia mitandao ya kijamii kwa faida ili kuifanya jamii ikutambue kwa namna unavyolenga kuja kutoa bidhaa yako.
Hitimisho
Fikiria na amua leo, je wewe unataka kutambulika kama mtu wa namna gani? Anza kujijenga kama BRAND !
Kumbuka tunatengeneza BRANDS ili kunufaika hususani kifedha na kimaendeleo. Haijalishi muda gani utachukua kabla ya kuweka BRAND imara, ila kumbuka INALIPA kufanya hivyo.
Waweza jibrand kama MTU MAKINI, MWAMINIFU, MCHAPAKAZI halafu uone matokeo yake. Ila inahitaji kazi na mikakati kufikia huko.
Mawasiliano +255 658 194 194
↧
↧
Magazeti ya Tanzania Leo Jumanne ya July 4,2017
↧
Hizi hapa nafasi za kazi 400 kutoka serikalini
↧
Picha:Mbunge wa CCM Alivyotaka Kupigana na Wabunge wa CHADEMA Jana Bungeni
MBUNGE wa Viti Maalum (CCM) Juliana Shonza, jana alizua timbwili nje ya viwanja vya bunge na kunusurika kupigwa na wabunge wa upinzani kutokana na kuwatambia kwamba atahakikisha Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye yuko kifungoni anaendelea kusota huko.
Wabunge hao wa Chadema waliitwa Polisi kuhojiwa usiku wa kuamkia leo
Hapo chini ni picha za tukio hilo
Wabunge hao wa Chadema waliitwa Polisi kuhojiwa usiku wa kuamkia leo
Hapo chini ni picha za tukio hilo
↧
↧
Korea Kaskazini yafyatua Kombora zito, latua eneo Muhimu Japan
Korea Kaskazini imeendelea na mpango wake wa majaribio ya silaha nzito ambapo jana usiku imeripotiwa kufyatua kombora lingine zito kutoka Magharibi mwa eneo lake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na maafisa wa Japan na Korea Kaskazini, kombora hilo lilifyatuliwa majira ya saa tatu na dakika arobaini usiku kwa saa za eneo hilo, na lilitua katika eneo muhimu la kiuchumi la bahari nchini Japan.
Shirika la habari la Yonhap limekariri tamko la jeshi la Japan kuwa kombora lililofyatuliwa lilisafiri umbali wa kilometa 930 na lilichukua dakika 40 kabla ya kutua, kitendo kilichozua taharuki.
Hili ni jaribio la 11 la makombora ya Korea Kaskazini kwa mwaka huu, ingawa majaribio ya hivi karibuni yanaonekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Jaribio la mwisho lilikuwa mwezi Mei mwaka huu, katika maeneo mawili tofauti ambayo yote yalielekezwa baharini nchini Japan.
Katibu Mkuu wa Baraza la Mawazili la Japan, Yoshihide Suga ameeleza kuwa uchokozi unaofanywa na Korea Kaskazini hauvumiliki. Ameongeza kuwa taifa hilo linalaani kwa nguvu zote vitendo hivyo na hatua stahiki zitachukuliwa.
Naye Rais wa Korea Kusini, Moon Jae ametoa wito wa kufanyika kwa kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili hatua za Korea Kaskazini, wito aliousisitiza pia wakati wa kikao chake na Rais wa Marekani, Donald Trump ndani ya Ikulu ya Marekani.
↧
Taarifa Muhimu Toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 3 Julai, 2017 amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mwanza.
Akiwa mkoani hapa Mhe. Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Sengerema leo tarehe 4 Julai, 2017.
Katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza Mhe. Rais Dkt. Magufuli alikutana na kamati ya amani ya viongozi wa dini na kuwashukuru viongozi hao kwa sala na dua zao na amewataka waendelee kuwahimiza waumini wao kuliombea Taifa ili liepukane na vitendo vya rushwa ambavyo ni adui wa maendeleo.
Akiwa njiani kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza katika eneo la Bwiru kuelekea Ikulu ndogo ya Mwanza, Mhe. Rais Magufuli msafara wake ulisimamishwa mara kwa mara na wananchi waliojaa barabarani na kuamua kuzungumza nao ambapo aliwahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imepania kupambana na ufisadi kwa lengo la kuwaletea maendeleo Watanzania bila kujali tofauti za dini au Siasa.
Aidha, aliwahakikishia wananchi hao kuwa Serikali yake imedhamiria kuondoa kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufuta baadhi ya kodi zenye kero na kuwapatia vitambulisho wafanyabishara wadogo wadogo, maarufu kama Wamachinga, ili waweze kufanya biashara zao bila kusumbuliwa.
Akiwa eneo la Nyamagana jijini Mwanza, Mheshimiwa Rais alitembea kwa miguu huku kuwasalimu wananchi waliokuwa wakimshangilia na kuzuia msafara wake.
Rais Magufuli pia alikwenda Uwanja wa Mpira wa Nyamagana na kuungana na baadhi ya wananchi waliokuwa wakiangalia mechi ya mpira wa miguu kati ya timu ya Buhongwe na Nyamwaga.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli pia amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa barabara ya kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza hadi katikakati ya jiji ambao gharama za ujenzi wake zilitokana na fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe za Muungano.
Jaffar Haniu Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Mwanza
↧
Rais Magufuli: Mwalimu Atakaye Mrudisha Mwanafunzi Aliyepata Mimba Ntamfukuza Kazi
Rais John Magufuli amesema mwalimu mkuu atakayeruhusu mwanafunzi aliyejifungua kurudi shuleni kuendelea na masomo katika shule za Serikali, atafukuzwa kazi.
Rais ameyasema hayo leo (Jumanne, Julai 4) alipokuwa akihutubia wananchi wakati akizindua mradi wa maji Sengerema.
“Ni ukweli pia kuwa wanafunzi waliopata mimba hawarudishwi shuleni, kuna ujanja ujanja wa walimu, wanaandika cheti kuwa alikuwa amelazwa,” amesema na kuongeza:
“Nikimuona Headmaster, amerudisha mwanafunzi aliyepata mimba, kwenye shule za Serikali, yule mwalimu anaondoka.”
Rais amehoji: “Wote waliopata mimba wamebakwa?” Alihoji na kuendelea,“wanafanya mambo haya kwenye picha, wakipata mimba kwa namna hiyo arudi shule.”
↧
Rais Magufuli: Mnaotaka wenye Mimba Warudi Shule Muanzishe Shule Zenu
Rais John Magufuli amezitaka Asasi za Kiraia (NGO’s) kufungua shule kwa wanafunzi wanaopata mimba shuleni kama kweli zinawapenda wanafunzi hao.
Rais ameyasema hayo leo (Jumanne, Julai 4) alipokuwa akihutubia wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Sengerema.
“Si kwamba nawachukia wenye mimba, hata kwa bahati mbaya akapata mimba, kama hizo NGO zinawatetea sana, zifungue shule za wenye mimba, kwa sababu zinawapenda wenye mimba, wafungue shule zao,”amesema Rais leo.
Amesema hata hao wanaofanya makongamano ya kuhamasisha watu wapate mimba wafungue shule zao kwa ajili ya wanafunzi hao.
“ Haiwezekani fedha za walipa kodi, Sh 17 bilioni kila mwaka za kusomesha watoto wetu, kwenda kusomesha wakinamama, wazunguke, waimbe, waseme nini mimi ndiyo Rais, huo ndio ukweli,” amesema.
Amesema tatizo si wanaopata mimba, kwani wapo waliopata matatizo, kama kuugua kwa muda mrefu wakashindwa kwenda shule lakini ulianzishwa mpango maalum wa kuwasomesha katika mfumo usio rasmi.
↧
↧
Hongera Diamond Platnumz...Embu Sikia Hawa Wasomi Baada ya Kusikia Diamond Anauza Karanga
Niliwahi kuandika wakati fulani (2015) kuwa ukimwendea Bakhressa ukamwambia kuwa #mihogo ni biashara nzuri atakuita board room muongee vizuri apate kujua vizuri lakini ukimfata msomi mwenye labda masters ya biashara ukamwambia kitu kile kile anaweza kukuona huna idea kichwani.
Nilipoona video ya #DiamondPlutnumz akizindua biashara yake mpya ya #DiamondKaranga nikawaza tena. Nikamforwadia mdogo wangu mmoja anasoma "ELIMU YA JUU" kwa sasa. Alipoiangalia nikamuuliza maswali machache:
1. Hiyo ni video ya Diamond na karanga?
Akajibu #NDIYO BRO
2. Nikamuuliza: Diamond amechuja kimuziki ndo maana kakimbilia karanga?
Akajibu #HAPANA
3. Nikamuuliza: Diamond alisomea biashara Chuo?
Akajibu #HAPANA
4. Nikamuuliza: Ana akili ya kibiashara?
Akajibu #NDIYO
5. Nikamuuliza: Ana hela nzuri nzuri benki?
Akajibu #NDIYO
6. Nikamuuliza: Sasa haoni aibu kuuza karanga?
Akajibu #HAPANA
7. Nikamuuliza: Kwa nini haoni aibu? Akajibu nadhani sababu ya pale juu NAMBA 4
Nikajisemea: Good.
8. Nikamuuliza: Wewe umesoma kuliko Diamond?
Akajibu: #NDIYO KAKA.
9. Nikamuuliza: Unaweza kuuza karanga?
......... (KIMYA).......
10. Nikataka kuuliza tena
..nikaona "Typing......"
Jibu likaja: INATEGEMEA
Anyway mpaka hapo nikawa nimeelewa jibu sahihi ni lipi. Kwamba nikimpa huyu msomi option mbili baada ya masomo yake. Moja apate AJIRA pale Azikiwe CRDB, mshahara labda laki 9 kwa mwezi na mkopo nafuu wa kununua IST... halafu option nyingine iwe idea ya kuuza karanga kuanzia zero ipi atachagua?
Nadhani jibu wote tunalo.
Kuna binti mwingine wa "Elimu ya Juu" alikuja kwangu akiomba msaada wa kutafutiwa mahali pa kufanya kazi kwa muda wakati wa likizo. Pamoja na hilo nilianza kumuuliza kama ana KIPAWA chochote ambacho anaweza kukitumia taratibu akijenge kije kumsaidia baadaye hata ajira zikija kugoma. Pamoja na binti huyo kukiri kuwa anacho kipawa (alinitajia) lakini hakuwa tayari kukifanyia kazi in any way hata kwa muda wa ziada. Anataka tu ajira.
Hili ni #JANGA.
Tuna wasomi wetu wengi ambao wanachotaka ni AJIRA TU. Serikali nayo inadhani itaweza kutatua tatizo la ajira kwa a one-sided view. Kwamba mtu asiye na ajira dawa yake kumpa ajira. Si kweli kwamba hiyo ndo dawa pekee. In fact tuendako hiyo ni wrong solution. Mfano mdogo ajira za madereva kwa dunia ya leo zinaondoka moja moja.
Fikiria: Siku jiji hili la Dar es Salaam kwa mfano hili likiwa na Mwendokasi kila Kona ya jiji na huko mbali na city centre kote kuanzia Bunju (au Bagamoyo) hadi Mbagala na hadi huko Chalinze.
Halafu treni za umeme ziko
Halafu self driving cars
Halafu drones za kudeliver mizigo kwa wateja (yani uko zako nyumbani labda Bunju unaagiza chakula KFC Posta unalipia kwa M-PESA kinaletwa na drone ndani ya robo saa tu hadi mlangoni kwako)
Hapo mtu aliyesomea udereva ataendesha nini?
Licha ya hayo mambo kukawia yatafika. Lakini hata kabla hayajafika ajira ngapi zipo na nani atapata nani akose.
Wasomi wetu ni lazima waanze kuwaza tofauti na wasomi wa mwaka 1970. Lazima kuwaza option ya kusurvive nje ya mfumo wa ajira.
Tatizo wengi wanachotaka ni MSHAHARA tu. Ndo maana wakikutana na wewe utasikia: "BRO NIUNGANISHE BASI HATA KWA RAFIKI ZAKO NIPATE KAZI". Ndo lugha yao. NIUNGANISHE. Yaani utadhani wewe umekuwa fundi welding...
Ukimpa idea nyingine HATAKI.
Ndo maana watu wasio na shule ndeefu ndo wanakuwa matajiri. Si bure. Katika matajiri wote 2000+ kwenye Forbes wenye MBA unaweza kuta hata 10 hawafiki. Na hao wenye hiyo MBA siyo kuwa ndo imewafanya wa excel in bness.
Lazima kuwaza kwa mapana. Wasomi hawataki kuumiza kichwa wanataka ready made things. Hii si njema kwa afya ya uchumi wa taifa letu.
Ukitazama #DiamondPlutnumz na karanga unashangaa kwa nini msomi akikuona unaanzisha biashara yako anataka umpe tu AJIRA hataki umfundishe afanye. Makanisani nako wasomi wanaombewa tu wapate AJIRA. Basi. Kweli? Ina maana hakuna MAONO mengine kwa wasomi wetu isipokuwa ajira?
Elimu ya juu kwa vijana wengi imepeleka creativity yao na uthubutu wao CHINI!
So sad!
Sikiliza kijana msomi:
Ni muhimu kuyatazama maisha yako kwa mapana na kwa upya kabisa pasipo kuyahusisha na elimu yako ya darasani kabisa.
Mungu awabariki sana.
Hongera tena #DiamondKaranga
↧
Ni rahisi sana Sana Kwa Mwanandoa Aliyeajiriwa Hapa Mjini Kuchepuka, Hivi Ndivyo Wanavyofanya
Nina uzoefu kidogo na mambo ya kazi za ajira maofisini, nimefanya hivi kwa muda mrefu. Wakati flani nilifanya kazi katika ofisi zilizo katikati ya jiji, kule mitaa ya Posta jijini Dar es Salaam.
Ofisi nyingi za serikali na watu binafsi zinapatikana mitaa ile. Kutokana na sababu hiyo, kuna idadi kubwa pia ya migahawa, hoteli, mama ntilie, pub na kadhalika.
Kuna mambo mawili makubwa yenye ushawishi mkubwa wa usaliti. Ofa za chakula au vinywaji na usafiri. Kwa kawaida, wafanyakazi wa ofisi moja hupenda kutoka pamoja wakati wa chakula cha mchana, wenyewe tunapendelea zaidi kusema lunch!
Kila mmoja ana sehemu yake anayokula kulingana na kipato chake, wapo wanaokwenda Southern Sun kupata chakula cha mchana, na wapo wanaowafuata mama ntilie wanaojibanza kwenye vichochoro vingi vilivyopo mjini.
Huko ndiko tunakokutana na akina dada waliovalia vizuri na kupendeza, wakitokea katika maofisi mbalimbali, huwezi kujua yupi ni mhudumu wa chai, yupi ni bosi, wote wanang’ara. Na hapa ndipo ofa za misosi zinapoanza kushawishi ngono.
Kijana mmoja mwenye kipato kikubwa ofisini kwake, atavutiwa na msichana mrembo mwenye mshahara wa wastani. Ili kumsogeza karibu, atalipia chakula cha siku hiyo na kumualika kwa kesho yake. Kulipiwa chakula ni jambo dogo, lakini lenye thamani kubwa sana. Si rahisi mtu aliyekulipia chakula kwa nia njema, ukaacha kumshukuru na hata kumwelekeza unapofanya kazi.
“Mimi nipo pale Oj Traders,” msichana anaweza kujita mbulisha jina na kusema anapofanyia kazi huku mkaka akimweleza kuwa yeye ni mhasibu katika ofisi flani. Watakapo
kutana mara ya pili, wataachiana namba za simu.
Baada ya hapo, mkaka atafanya mbwembwe za kuhamahama maeneo ya lunch ili mradi tu mdada wa watu aingie kwenye laini.
Ukimaliza suala la lunch, kuna hii kitu foleni, hasa kwa wakazi wa Dar es Salaam. Raha ya kufanya kazi katikati ya jiji inaingia shubiri kadiri jioni inavyozidi kusogea. Kuanzia saa kumi, ni vurugu katika vituo vya daladala na hasa wakati kama huu ambao bodaboda zimezuiliwa kuingia mjini.
Wenye magari binafsi ndiyo wakati wao wa kujidai, ingawa foleni inawakumba wote. Lakini ni afadhali ukiwa kwenye foleni ndani ya gari dogo, mko wawili kuliko foleni, umeshika bomba kwenye daladala.
Siyo rahisi kwa mdada kukataa lifti ya kijana mwenye gari. Na katika foleni ndefu, ni wazi kwamba hadi mwisho wa safari, watakuwa wameshabadilishana namba. Kwa msichana, kuwa na uhakika wa usafiri kila siku ni ukombozi.
Tusidanganyane, hakuna msichana ambaye hatajua kuwa lunch au usafiri anaopewa unahitaji malipo maalum, ambayo ni penzi. Hali hii haiko Dar tu, bali nchi nzima na pengine duniani kote.
Mwanamke aliyeajiriwa anakuwa katika mitihani mikubwa zaidi ya kusaliti ndoa au uhusiano wake, kwa sababu hata kama haitakuwa kwenye chakula au usafiri, bado watu anaokutana nao katika utendaji wake, wanaweza kumghasi. Fikiria anakutana na mabosi, marafiki wa mabosi wake, wafanya biashara, atapona kweli?
Hata hivyo, simaanishi kama tabia hii inawakumba waajiriwa wote, isipokuwa nadhani ni sehemu kubwa wanahusika!
By Mike Tee
↧
Namshukuru Mungu sikufikia hatua ya kujiuza – Saida Karoli

Msanii wa muziki wa asili Bongo, Saida Karoli amesema licha ya yeye kushuka kimuziki hakufikia hatua ya kujiuza.
Saida ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Orugambo’, ameeleza licha ya kuepuka hilo hata unywaji wa pombe alisitisha.“Vitu vingi nilipitia ila namshukuru Mwenyenzi Mungu sikufikia hatua ya kusema najiuza, na mpaka mtu anafikia anaona yeye sio kitu anaenda kujiuza barabarani, kuuza mwili wake lakini mimi sikufanya hivyo,” Saida ameiambia Power Breakfast ya Clouds FM na kuongeza.
“Nilikuwa nakunywa pombe sana lakini kutokana na kushuka kwangu nikaona na pombe niache tangu mwaka 2006, situmii bia, situmii Sigara namshukuru Mwenyenzi Mungu amenipa ustahimilivu nimesimama wima hatimae nimerudi Saida yule yule,” amesistiza.
By Peter Akaro
↧
Magazeti ya Tanzania Leo Jumatano ya July 5,2017
↧
↧
Kiongozi wa Korea Kaskazini Amkejeli Rais wa Marekani........Ni Baada ya Kurusha Kombora la Masafa Marefu Linaloweza Kutua Hadi Marekani
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un amemkejeli Rais wa Marekani, Donald Trump saa chache baada ya kufyatua kombora zito ambalo linadaiwa kuwa na uwezo wa kufika Alaska Marekani na sehemu nyingine duniani.
Timu ya ujasusi ya Marekani ilieleza kuwa kombora hilo la Korea Kaskazini lililofyatuliwa wiki hii limeonesha kufanikiwa kwa kiasi kikubwa na kwamba lilienda umbali wa zaidi ya Kilometa 900 kabla halijatua baharini kwenye eneo muhimu la kiuchumi nchini Japan.
Kwa mujibu wa Sky News, Kim Jong-Un ameeleza kuwa kombora hilo lililofyatuliwa Julai 4, siku ya kuadhimisha uhuru wa Marekani, lilikuwa zawadi yake kwa Marekani na kiongozi wake.
“Lilikuwa lenye muonekano wenye mvuto kama mvulana mtanashati,” Sky News inamkariri Kim Jong-Un. “Ilikuwa zawadi nzuri kwa Marekani siku ya maadhimisho ya uhuru wao,” anadaiwa kuongeza.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani imeeleza kuwa Rais Trump na timu ya wana usalama inaendelea kuvifanyia usaili wa karibu vitendo vya Korea Kaskazini na kwamba nchi hiyo imefikia ukomo wa uvumilivu wake.
Imeeleza kuwa Marekani itaongeza vikwazo zaidi dhidi ya nchi hiyo wakati ambapo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kujadili hatua dhidi ya Korea Kaskazini.
Urusi na China, jana zilitoa tamko la kulaani majaribio ya makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini, ambayo ni tishio kwa dunia nzima.
Kombora hilo aina ya Hwasong -14 liliruka umbali wa kilomita 2,802 na kusafiri kwa umbali wa kilomita 933 kwa dakika 39 kabla ya kuanguka baharini.
Korea Kaskazini imesema kuwa ni taifa lililojihami kinyuklia ambalo linamiliki kombora la masafa marefu linaloweza kushambulia eneno lolote duniani
Korea Kaskazini imesema kuwa ni taifa lililojihami kinyuklia ambalo linamiliki kombora la masafa marefu linaloweza kushambulia eneno lolote duniani
↧
Wapiga Dili Wamzuia Rais Magufuli Kusafiri Nje ya Nchi
Rais John Magufuli amesema amepata mialiko zaidi ya 60 kwenda nje ya nchi baada ya kuwa Rais lakini ameikataa kwa sababu anataka kuishughulikia Tanzania kwanza.
Ameyasema hayo jana (Jumanne Julai 4) wakati akihutubia wakazi wa Sengerema katika uzinduzi wa mradi wa maji Sengerema.
Rais Magufuli amesema hana haja ya kwenda nje ya nchi kwa sababu bado ana mzigo mkubwa wa kumaliza ufisadi.
“Niende nje kufanya nini wakati ntaenda tu nikishastaafu, nataka nimalize kwanza haya ya hapa ndani,” alisema.
↧
SHERIA MPYA YAPITISHWA...SASA MARUFUKU MAKINIKIA KUCHENJULIWA NJE YA NCHI,TMAA TUPA KULE
Bunge limepitisha sheria mpya ambayo sasa itatambua haki na dhamana ya serikali katika makinikia ambayo itakuwa ni marufuku kuchenjuliwa nje ya nchi na serikali itashiriki kwa asilimia kuanzia 16 hadi 50 katika shughuli zote za uchimbaji, uchakataji na uchejuaji madini na ununuzi wa hisa katika kampuni ya uchimbaji madini.
Aidha, Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) umefutwa rasmi na sasa kunaanzishwa Kamisheni ya Madini, na kwamba kuanzia sasa umiliki wa leseni mbalimbali zinazotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Madini, hautahamishwa kabla haujafanyiwa uendelezaji katika kitalu husika.
Akielezea mapendekezo ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2017 katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi alisema asilimia hizo za hisa ni kwa kuangalia thamani ya gharama ambazo serikali inahamia katika vituo vya uwekezaji na kodi aliyopewa mwekezaji.
Profesa Kabudi alisema muswada huo pia unatambua haki na dhamana ya serikali juu ya makinikia na kuweka utaratibu wa kuyahifadhi sehemu maalumu migodini chini ya uangalizi wa serikali.
“Kupitia marekebisho hayo, makinikia yanayotolewa nchini bila kufanyiwa uchunguzi wa kupata thamani halisi kabla ya kuchenjuliwa na uchenjuaji utafanyika nchini. Kuanzia sasa makinikia hayatauzwa nje ya nchi, yatauzwa kwenda kwa wachenjuaji wa ndani ya nchi yakiwa ni bidhaa ambayo itatozwa kodi,” alifafanua.
Alisema pia muswada unaipa serikali haki na dhamana juu ya usimamizi wa bidhaa zote na maliasili, zinazotokana na uchimbaji, uchakataji na uchejuaji wa madini yakiwamo makinikia au kwa jina maarufu mchanga wa dhahabu.
Aidha, alisema muswada umelenga kutambua na kuweka chini ya uangalizi wa serikali maeneo yote ya uchimbaji na madini kwa lengo la kuweka ulinzi na usimamizi madhubuti wa madini kwa lengo la kuweka ulinzi na usimamizi madhubuti wa maeneo ya uchimbaji.
“Hii itasaidia kuwepo ulinzimahsusi wa maeneo yote ya uchimbaji wa madini, kuwepo kwa utaratibu wa serikali kufanya ukaguzi na udhibiti wa usambazaji wa madini, kuipa serikali uwezo wa kudhibiti na kutambua viwango vya madini yote yanayotolewa kwenye maeneo ya migodi na kupitia vyombo vya ulinzi na usalama vya serikali,” alieleza.
TMAA yazikwa rasmi
Alieleza kuwa kufutwa kwa TMAA kunatokana na majukumu yake, yaliyokuwa yakitekelezwa na wakala huyo kuhamishiwa kwa Kamisheni ya Madini ambayo itaanzishwa.
Akiwasilisha muswada huo, Profesa Kabudi alisema kutokana na kufanyiwa mapitio ya madaraka ya Waziri na Kamishna wa Madini kwa lengo la kuwapunguza baadhi ya majukumu na madaraka yatahamishiwa kwa Kamisheni ya Madini.
Alisema kamisheni inayopendekezwa kuanzishwa itakuwa na jumla ya makamishina tisa, na watu kati yao akiwamo Mwenyekiti watakuwa wa kudumu.
“Watashirikiana na watendaji wakuu kutekeleza majukumu yao ya Kamisheni ya kila siku, makamishna wengine watakuwa wa muda na watakutana katika vikao maalumu vya kamisheni kwa ajili ya kufanya maamuzi ya misingi na kufuatilia utekelezaji wake,” alifafanua na kuongeza kuwa makamishina wa muda watateuliwa kutokana na nafasi zao ambao ni Katibu Mkuu Hazina, Katibu Mkuu Tamisemi, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu wa Ulinzi na Katibu Mkuu Ardhi.
“Kamisheni inayopendekezwa kuundwa itachukua majukumu sehemu kubwa ya majukumu ya Kamishna wa Madini kwa sasa. Majukumu hayo ni pamoja na kutoa, kuhuisha au pale itakapolazimika kufuta leseni zote zinazotolewa kwa mujibu wa sheria ya madini, kusimamia shughuli za madini ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi maeneo ya migodi.
"Pia majukumu yote yaliyokuwa yakitekelezwa na TMAA yatahamishiwa na kuwekwa chini ya Kamishna. Na kwa msingi huu TMAA inafutwa,”alibainisha.
Umiliki wa leseni
Kuhusu kutohamisha leseni, alisema hatua hiyo ni katika kuzuia watu kufanya biashara ya udalali wa leseni.
Kuhusu kutohamisha leseni, alisema hatua hiyo ni katika kuzuia watu kufanya biashara ya udalali wa leseni.
“Katika kuweka masharti yanayokusudia kuzuia watu kufanya biashara ya udalali wa leseni mbalimbali zinazotolewa kwa mujibu wa sheria ya madini, mmiliki wa leseni hataruhusiwa kuhamisha umiliki wa leseni kabla ya uendelezaji katka kitalu husika,” alieleza.
Aliongeza, “baada ya kumalizika kwa muda wake, leseni itahuishwa kwa kipindi kimoja tu, na baada ya hapo umiliki wa kitalu husika utarejeshwa serikalini.”
↧
Huu hapa Uamuzi Wa Kikao Cha Kamati Ya Utendaji ya Shirikisho la soka nchini TFF
Kamati ya Utendaji (EXCOMM) ya Shirikisho la soka nchini TFF, ilikutana jana Jumanne Julai 4, 2017 katika kikao cha dharura ambako ilijadili mgawanyiko katika Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Kamati hiyo ya utendaji ilikutana kwa dharura kwa mujibu wa Ibara ya 35 (1) ya Katiba ya TFF inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6). Kikao cha Kamati hiyo kilianza saa 8.58 alasiri hadi saa 10.51 jioni.
Katika kikao chake kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za shirikisho, Karume jijini Dar es Salaam Kamati iliamua kufanya mabadiliko madogo katika Kamati zake za Kisheria na Kamati za uchaguzi kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 44 (7) na Ibara ya 52 inayotoa mamlaka ya kufanya mabaduiliko hayo.
Katika Kamati ya Uchaguzi, EXCOMM imeteua Mawakili kuongoza kamati hiyo wakiongozwa na Msomi Wakili Revocatus Kuuli; Mheshimiwa Wakili Mohammed Mchengelwa; Msomi Wakili Malangwe Mchungahela; Msomi Wakili Kiomoni Kibamba na Msomi Wakili Thadeus Karua.
Katika Kamati ya Rufaa Uchaguzi, EXCOMM imeteua Msomi Wakili, Abdi Kagomba kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Msomi Wakili Kenneth Mwenda na wajumbe ni Msomi Wakili Rashid Sadalla, Mhe. Jabir Shekimweri na Mohammed Gombati.
Kadhalika katika kamati za kisheria za TFF, ikianzia Kamati ya Maadili, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Hamidu Mbwezeleni kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Msomi Wakili Steven Zangira na wajumbe ni Mhe. Glorius Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhressa.
Kamati ya Rufaa na Maadili, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Ebenezer Mshana kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Naibu Kamisha katika Jeshi la Polisi (DCP), Mohammed Mpinga na Wajumbe ni Msomi Wakili Benjamin Karume; Dk. Lisobine Kisongo na Mrakibu Msaidizi wa Polisi – ASP Benedict Nyagabona.
Kamati ya Nidhamu ya TFF, EXCOMM imeteua Tarimba Abbas kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Peter Hella huku Wajumbe wakiwa ni Boniface Lyamwike, Dk. Billy Haonga na Kassim Dau.
Kamati ya Rufaa ya Nidhamu, EXCOMM imeteua Wakili Msomi, Rahim Shaban kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Siza Chenja huku Wajumbe wakiwa ni Abbas Mtemvu; Amani Mulika, Amin Bakhressa na Stella Mwakingwe.
↧
↧
KIDOA SI WA MCHEZO MCHEZO ANAMILIKI MJENGO WA HATARI


Akipiga stori na Za Motomoto News, alisema tangu ajikite kwenye ishu hiyo amebadilisha maisha yake kwani sasa ameweza kumhamisha mama yake kutoka nyumba ya kupanga aliyokuwa anaishi maeneo ya Kinondoni Dar.
“Namshukuru Mungu, tamthiliya zinanilipa kwa kweli sikutarajia kwa umri huu mdogo wa miaka 22, ningeweza kumiliki mjengo tena kwa jasho langu, hatimaye nimemnusuru mama yangu na mabalaa ya nyumba za kupanga,” alisema Kidoa.
Stori: Mayasa Mariwata
↧
MREMBO HAMISSA MOBETO AMUANIKA BABA KIJACHO WAKE

Muuza nyago kwenye video za wasanii, Hamissa Mobeto.
Muuza nyago kwenye video za wasanii, Hamissa Mobeto anayehisiwa kuwa ni mama kijacho, kutokana na baadhi ya picha zake za hivi karibuni zikimuonyesha akiwa ameshiba yaani kitumbo ndiii!!!
Huku Wabongo wakiwa bado wanajiuliza swali la ni nani hasa baba kijacho wa kitumbo hicho, wengine wakienda mbali zaidi na kuhisi labda huenda hicho kibendi ni cha mmoja wa wasanii waliowahi kujivinjari naye au ni cha baba wa mtoto wake wa kwanza!
Sasa jana kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Mobeto kaliamsha dude baada ya kuposti picha yake na kuandika maelezo yafuatayo; Mama daa…Mama dee…Mama dii…Mama doo… Mama duu… ambapo mashabiki wakafananisha maelezo hayo na hisia zao za muda mrefu kuwa kibendi hicho ni cha yuleyule msanii wa bongo fleva aliyekuwa akihisiwa.
↧
Alichosema Haitham kuhusu wimbo wake na Wema Sepetu
Msanii wa Bongo Fleva, Haitham ameelezea jinsi alivyofanya kazi na mrembo Wema Sepetu.

Haitham ambaye amemshirikisha Wema Sepetu katika wimbo wake mpya ‘Play Boy’, ameiambia XXL ya Clouds FM kufanya kazi na Wema kumeongeza uzito wa jina lake.
“Toka nimetoa ngoma na Wema nimeona watu wamenipokea vizuri tena zaidi na zaidi lakini sio kwa sababu nimefanya na Wema pekee yake tu, kwa sababu ya muziki mzuri, watu pia wanasema muziki ni mzuri,” amesema Haitham.
By Peter Akaro
↧