Quantcast
Channel: LEWIS MBONDE BLOG
Viewing all 7853 articles
Browse latest View live

Tambua:Wanaume Wengi Hupenda Wanawake Wenye Tabia Hizi

$
0
0

Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.


Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.

Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.

MWEYE MAPENZI YA KWELI

Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake. Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingi utamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.

Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.

Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.

WENYE TABIA NZURI

Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja suala na kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya. Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.
Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.

WENYE UCHU NA MAENDELEO

Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani 'golikipa'. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini. Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.

WASIOPENDA MAKUU

Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi dear?" Akimuona rafiki yake kanunua simu ya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia, "mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.


Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.’

Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leo amemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.

Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitaji upo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulani wakati inawezekana uwezekano haupo.

WAVUMILIVU

Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?

Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.

Licha ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu, wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo kimsingi havikubaliki katka jamii.Tabia hizo ni kama wambea, wasio wakweli na wawazi, wasioridhika, wagumu kusamehe na wapesi wa kuchukia, wagomvi na wenye roho ya kwanini.

Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume ambao wanatarajia kuoa wanawake ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali jijini Dar-es-Salaam. Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.

WAKONGWE 15 BONGO FLEVA WAPIGIWA ‘MIZINGA YA HESHIMA’ DAR LIVE

$
0
0
Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes, akiwasikilizisha nyimbo zake mashabiki waliofurika katika Ukumbi wa Dar Live usiku wa kuamikia leo katika shoo ya kuwapa heshima waanzilishi wa Muziki wa Bongo Flava nchini ambapo 'mizinga' mitano ya kuheshimu kazi yao hiyo ilipigwa.[/caption] Usiku wa kuamkia leo Jumapili ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar kulikuwa na shoo ya heshima kwa Bongo Flava waanzilishi wa muziki huo waliowahi kutamba enzi hizo walipigiwa mizinga mitano kabla kuanza mambo. Shoo hiyo iliyoandaliwa na kituo cha Redio na Runinga cha East Africa Television na Radio ya East Afrika kupitia kipindi chake cha Planet Bongo baada ya kupigwa mizinga hiyo umati uliofurika ukumbini hapo ulitulia dakika moja kuwakumbuka waanzilishi wa muziki huo waliotangulia mbele za haki. Baadhi ya wasanii waliotajwa majina yao wakiwa mbele za haki ni pamoja na Albert Mangwair, Mr Ebbo, Dogo Mfaume, Langa Kileo, Complex na Vivian ambao wote nyimbo zao zilizowahi kutikisa zilipigwa. ...Akiendelea kuwapagawisha mashabiki.[/caption] Tukio la kuwakumbuka waasisi hao lilipopita wasanii na makundi mbalimbali yaliyowahi kutikisa enzi hizo yalianza kuvamia jukwaa moja baada ya jingine na kupiga nyimbo zao zilizowahi kutamba. Mashabiki wa burudani walionekana kukunwa sana na burudani hiyo ambapo baadhi walisikika wakisema hiyo ndiyo ilikuwa Bongo Flava ya ukweli. Katika burudani hiyo alianza kuvamia jukwaa Z Anto, University Corner, LWP, Daz Nundaz Family chini ya Daz Baba, Wagosi wa Kaya, Solid Ground Family, Dully Sykes, Mandojo na Domokaya, Tid, Jaymoe, Dudu Baya, Manduli Boy, Mabaga Fresh, Afande Sele, Ispector Haruni ambapo mkali wa Temeke, Juma Nature ndiye aliyefunga kazi. [caption id="attachment_151489" align="aligncenter" width="800"] Mashabiki wakimshangilia Dully Sykes.[/caption] Katika burudani hiyo kila msanii aliyepanda jukwaani alitaka kujidhihirisha kama bado yuko vizuri kwenye gemu maana makamuziki hayakuwa ya chini, ambapo Kundi la Mabaga Fresh lilionekana kuupagawisha ukumbi huo hasa waliposhusha kibao chao kilichowawahi kutamba cha Tunataabika.
Kibao hicho kiliufanya ukumbi huo ulipuke kwa mayowe ya kushangilia huku DJ Snox naye akiwachagiza kwa swaga za kiulemavu huku akiinadi tafsiri ya Mabaga Fresh kuwa Ulemavu fresh tu. [caption id="attachment_151493" align="aligncenter" width="800"] Msanii mkongwe Khalid Mohammed aka TID Mnyama akifanya makamuzi. ...TID akiendelea kufanya makamuzi 
Msanii mkongwe mwengine, Dudu Baya, akiongea na mashabiki wakati wa shoo hiyo. ...Akipiga shoo. Kundi la Mabaga Freshi wakikumbushia enzi zao. ...Makamuzi yakiendelea Msanii mkonge, Afande Sele, akiwapagawisha mashabiki wa Bongo Fleva. Inspekta Haroun akikumbushia enzi zake kwa mashabiki. Juma Nature (kushoto) na Dollo wakifanya makamuzi. Inspekta (kushoto) akiimba na Juma Nature. Jay Moe akiwapa burudani mashabiki. Wagosi wa Kaya wakiwapa burudani mashabiki kwa nyimbo za tangu enzi zao mpaka sasa.[/caption]
(Picha/Habari na Richard Bukos/GPL)

Magazeti ya Leo Tanzania Jumapili ya July 2,207

Hizi hapa Kanuni Kumi '10' za Kuwa Mke Mwema

$
0
0
UHALISI WA MAISHA:
Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke/ mke tayari hii ni kumaanisha kuwa wanawake mashujaa tunapaswa kuishi maisha ambayo yanatutambulisha kama mfano wa kuigwa ili tunapozungumza na kufundisha mabadiliko tuwe tunazungumza uhalisia wa maisha yetu ambao unajengwa na haya yafuatayo;

UVUMILIVU:
Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbali mbali yasiyotuvutia katika mahusiano yetu, mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi kama vile; chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko, manung’uniko, machafuko, kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako. Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo.

UPENDO WA DHATI:
Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafki kwa jamii inayomzunguka. Tabia ya upendo wa halisi ina thamani kubwa sana kuliko mali nyingi, pesa, elimu ya juu n.k. wewe unaweza kabisa kuwa na elimu ya juu sana na pesa nyingi sana lakini pasipo upendo wa halisi ni sawa na kusema kopo zuri kwa nje na ndani hamna kitu. Nguzo kuu ya maisha ya mwanamke shujaa ni Upendo wa dhati na uhalisia.

UTII KWA KWA JAMII:
Maisha halisi ya utii katika jamii inayokuzunguka  ili kuweza kuyafanyia kazi yale yote uliyojifunza na pia kuyatenda kwa ufasaha pasipo kupita kona yoyote. Utii  kwa jamii ni ufunguo mmoja wapo utakaokusaidia kufanikisha mambo yako na malengo yako kama mwanamke shujaa.

UAMINIFU KATIKA JAMII:
Kuishi maisha ya uaminifu wa kweli na uhalisia katika jamii inayomzunguka. Uaminifu wa kweli huonekana nyakati zote na siyo tu wakati mtu anapokuwa mbele za watu wanaomjua bali hata wale wasiomjua na hata anapokuwa mahali peke yake aweze kutunza uaminifu wake kwa faida ya jamii nzima. Mwanamke shujaa hujitahidi sana kutunza uaminifu wake katika sekta zote.

UNYENYEKEVU WA KWELI:
Kuishi maisha halisi kabisa ya unyenyekevu kwa jamii inayomzunguka, unyenyekevu ni kinyume kabisa na kiburi, majivuno, kujigamba, kujikweza, kujiinua, kujiona,na hata kjitanguliza mbele kwa kila jambo. Mwanamke shujaa huwa ni mnyenyekevu wakati wote na hana makuu daima.

UWAJIBIKAJI WA DHATI:
Maisha halisi ya uwajibikaji akiangalia majukumu yake yote yanayomkabili na kuhakikisha anafanya kwa moyo bila kuwa na tabia ya kusaidiwa majukumu yake. Mwanamke shujaa ni mfano wa kuigwa kutokana na uwajibikaji wake.

USHIRIKIANO WA DHATI:
Ushirikiano katika jamii inayomzunguka. Sisi wanawake mashujaa yatupasa kujua dhahiri kuwa kazi ya kubadili tabia na kufanya wengine wabadilike kwa lengo la kupata familia bora ni lazima kuwa na ushirikiano wa kweli ambao utajenga tabia ya kuaminiana na kunai mamoja katika harakati hizi za kuandaa/ kujenga familia bora.

UTARATIBU WA KAZI/MPANGILIO:
Katika utaratibu wa maisha yake, pamoja na mpangilio mzuri wa mambo yanayomzunguka hii itakusaidia kuwa na muda mzuri wa kufanya shughuli zako na pia kutekeleza majukumu yako ya kila siku kama mwanamke shujaa. Hakuna njia yoyote ya kukuwezesha kukua na kuendelea katika maisha yako bila kuwa na utaratibu na mpangilio wa mambo yako.

KUFANYA TATHIMINI:
Kuweza kufanya tathimini ya yale yote anayoyafanya katika maisha yake ya kila siku, pengine ni mfanyabiashara, mfanyakazi, mkulima n.k kama mwanamke shujaa yakupasa kutathimini shughuli zako kama zina leta faida/hasara kwa familia na jamii yako inayokuzunguka. Ukiona faida ni kubwa unaendelea na hiyo shughuli lakini kama hasara ni kubwa unajiweka katika nafasi ya kubadilisha aina ya shughuli mara moja bila kupoteza wakati.

Mwanamke Ukiwa na Tabia hizi 7, Lazima Mwanaume Akukimbie

$
0
0
1. CHOKOCHOKO
Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa.

Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.

Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.

2. KUTORIDHIKA
Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua wapenzi wao kwamba hawawatimizii mahitaji. Mwanaume anajitoa kumpa zawadi mpenzi wake, haridhiki tu.

Anaanza kuikosoa. Anasema haifanani na yeye, eti si ya hadhi yake. Akipewa fedha anasema hazitoshi. Kila siku ni malalamiko. Hampi nafasi mpenzi wake ya kufurahia uhusiano wao.  Anamfanya kila anapokutana naye awaze atapigwa mzinga.

Bahati mbaya sasa kila atakachopewa haridhiki. Anatamani kikubwa zaidi. Wanaume wengi siku hizi wanaichukia tabia hiyo. Hawapendi kuwa na mwanamke ambaye haridhiki na kile kidogo walichojaliwa. Wanaume wengi wakiona hivyo huwa wanaanza kumuepuka mwanamke wa ‘sampuli’ hiyo.

Kwake kunakuwa hakuna jema. Badala ya kumshauri mpenzi wake mbinu za kujikwamua kiuchumi yeye ni lawama tu. Kila siku analalamika kwamba wanaume wengine wanawapa wapenzi wao mahitaji muhimu lakini wa kwake hamtimizii.

Mwanaume akiona kila analofanya kwa mpenzi au mkewe haridhiki, hatoi shukurani ni rahisi kupunguza mapenzi kwa mtu wake. Taratibu anaanza kujitoa na hata kuhamishia mapenzi kwa mtu mwingine ambaye atakuwa anaridhika kwa kidogo anachopewa. Ni muhimu kuridhika.

3. KULINGANISHA
Hii nayo ni tabia isiyopendwa na wanaume wengi. Wanaume wanapenda kuishi maisha yao. Wanapenda kuheshimiwa na wapenzi wao. Wanapenda kumsikia mwanamke akisema; ‘hakuna mwanaume mwingine wa kufanana na wewe.’

Mwanaume anapenda kuhakikishiwa kwamba hakuna mwanaume mwingine kama yeye. Yeye ndiye mzuri au bora kuliko wanaume wengine hivyo mwanamke anapoanza kuonesha tabia za kumlimnganisha na mwanaume mwingine linakuwa tatizo kubwa.

Mwanaume anakasirika. Anaona ni rahisi mwanamke wake kumtamani mtu mwingine baki kuliko yeye. Sifa anazozitoa kwa mwanaume mwingine ni nzuri hivyo zinamvutia. Kama zinamvutia siku yoyote anaweza kushawishika kumfuata yule anayemvutia.

Wanawake wanapaswa kuwa makini katika eneo hilo. Hata kama umeona kuna kitu kizuri kimekuvutia kutoka kwa mwanaume mwingine, kamwe usije kumwambia mwenzi wako. Baki nalo moyoni. Jipe moyo kwamba mwanaume uliyenaye ndiye bora kuliko wanaume wote duniani.

4. KUWA TEGEMEZI
Wakati mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa kutojionesha huna kitu. Jioneshe kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume wa sasa hawapendi kuwa na mwanamke ambaye kila kitu anategemea kutoka kwa mwanaume.

Hata kama huna kazi lakini ni vyema basi mwanamke akajaribu kufanya biashara ndogondogo ambazo zitampunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa fedha kila wakati. Wanaume wanapenda kuwapa wapenzi wao fedha lakini inapozidi kipimo inageuka kuwa kero.

Yani kuanzia mahitaji ya kila siku, saluni, mavazi, ada ya watoto na mengine mengi mwanamke anamtegemea mwanaume. Yeye hataki kujishughulisha hata kidogo. Anataka aletewe, kazi yake kubwa ni kulea familia nyumbani.

Mwanaume akigundua mwanamke ni tegemezi mkiwa katika hatua za mwanzoni, ni rahisi kumkimbia mwanamke na kwenda kwa mwanamke ambaye angalau atakuwa hamtegemei kwa kila kitu. Mwanamke anayejiongeza hata kwa kutoa wazo la kuanzishiwa biashara ambayo itamfanya asiwe tegemezi.

5. KUTOKUA MUELEWA
Mwanaume anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi. Anatamani kuwa na mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya pale mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha wazo la kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye.

Wanaume wanapenda wanawake wanaowaelewa. Kama mwanamke anakuwa si wa kumuelewa mpenzi wake, kumsaidia basi mara nyingi mwanaume humkimbia.

6. KUJITAPA KWA KUWA NACHO
Hakuna mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anataka mwanaume afanye kile ambacho yeye anataka. Fedha zinamvimbisha kichwa na kuona kwamba anaweza kuwa na mamlaka ya kumuamrisha mumewe.

Anatumia fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni vigumu sana wanaume kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi wanajiepusha naye. Kwa kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume mwingine lakini pia watashindwana katika suala la kumtawala.

7. KUWA BIZE SANA
Wanaume wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao wanachukia mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona mwenzi wake anakuwa bize na kazi au biashara zake kiasi ambacho kitamfanya hata akose muda na mwenzi wake.

Unachotakiwa kufanya hapo mwanamke ni kujigawa. Hakikisha unakuwa bize na kazi lakini si ya kupitiliza maana itamfanya mwanaume akose muda wa kuwa na wewe pale anapokuhitaji, badala yake anaweza kwenda kwa mwanamke mwingine ambaye hayupo bize.

NCHI 10 ZINAZOONGOZA KUWA NA WASICHANA WAREMBO AFRIKA

$
0
0


Afrika ni miongoni mwa Bara lililobarikiwa tamaduni, lugha na watu tofauti wenye tabia zinazoshabihiana ikiwamo ukarimu.
Miongoni mwa watu wa Bara hili wapo wasichana warembo wa kuvutia tofauti na wengine, katika hili kuna mjadala mpana huku baadhi wakikubali kuwa kuna watu wanaovutia kuliko wengine huku baadhi yao wakidai kuwa uzuri, urembo wa mtu unatafsiriwa kulingana na anayemtizama.



Lakini katika hili tukubali tukatae miongoni mwa wanawake wa Afrika bila kujali wanatizamwa na nani ni wazuri na warembo na wanavutia kuliko wengine.

Ifuatayo ni orodha ya nchi 10 zenye wanawake wenye mvuto barani Afrika, mwaka jana Tanzania ilishika nafasi ya 10 mwaka huu imepanda nafasi moja na inashika nafasi ya tisa.

10: Ghana

Nchi ya Ghana inashika namba 10 kwa kuwa na wanawake wazuri Barani Afrika kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Machi mwaka huu na tovuti mbalimbali za masuala ya urembo ikiwamo Afrojuju, Urbanviralmedia.

Jambo wanalolingana wanawake wa Ghana kuwa wana mvuto wa asili ambao huuongezea kwa kujiremba.

Mwaka jana Ghana ilishika namba nane, mwaka huu imeshuka nafasi mbili na kushika nafasi ya 10.

9: Tanzania

Nafasi ya tisa mwaka huu imeshikiliwa na Tanzania iliyokuwa inashikilia nafasi ya 10 mwaka jana hivyo imepanda nafasi moja.

Miongoni mwa sifa za wanawake wa Tanzania ukiachilia mbali uzuri wa asil ni ni pamoja na kutunza nyumba, ujuzi wa kukisafisha chumba na kukipamba. Katika orodha hii wametajwa kuwa wanawake bora wachapa kazi na wanaojali familia.

8: Kenya

Imepanda nafasi moja kwa kuwa mwaka jana ilishika nafasi ya tisa.

Sifa za wanawake wa nchi hiyo ni pamoja na kuwa wajuzi katika mapenzi, wachapa kazi na watuamiaji wa pombe, jambo linalowatofautisha na watu wengine ni rangi yao ya kuvutia.

7: Nigeria

Kwa miaka miwili mfululizo warembo wa Nigeria wanashikilia nafasi ya saba.

Wanawake wa Nigeria licha ya kuwa na rangi za kuvutia, pia wana maumbo ya yaliyojazia na wamejaaliwa kuwa na uwezo wa kuzaa watoto wengi, kati ya 1970 na 2011 Nigeria iliongezeka idadi ya watu mara tatu na kuifanya kuwa nchi yenye wakazi wengi barani Afrika. Kama unataka mwanamke mzuri na atakayekuzaliwa watoto wengi Nigeria inakuhusu.

Kwa wale wanaotaka mwanamke mwenye sifa za kuwa mke, wa nchi hiyo wanafaa. Sifa ya kipekee wanajua kupika na kutunza familia.

6: Ivory Coast

Mwaka huu namba sita imeshikiliwa na Ivory Coast ambayo mwaka jana haikuwepo kabisa, hivyo imeingia kwenye 10 bora kwa mara ya kwanza, nafasi hiyo mwaka jana ilishikwa na nchi ya Afrika Kusini.

5: Afrika Kusini

Nchi hii imewapa jina warembo wake “Upinde wa Mvua wa Taifa”. mwaka huu imepanda nafasi moja kutoka nafasi ya sita iliyoshika mwaka jana.

Ni miongoni mwa nchi zenye wasichana warembo wa kuvutia katika Bara la Afrika. Miji ya Cape Town, Johannesburg, Pretoria na Durban ndiyo yenye wanawake wenye mvuto. Wanawake wa Afrika Kusini wanang’aa na kuvutia kutokana na ngozi zao nyororor.

Unapofika nchini humo hasa katika Jiji la Pretoria kuwa makini kwa sababu unaweza kugongwa na gari kutokana na kuwashangaa warembo hao ambao kwa kawaida huvaa tofauti kidogo, nguo zao huwa fupi.

4: Rwanda

Wanaume wao hujivunia kwa kuwaita “Tufaa Lililojificha”, mwaka jana nchi hiyo ilishika nafasi ya kwanza kwa kuwa na wanawake warembo, mwaka huu imekamata nafasi ya nne.

Wanawake wa nchi hii sifa ya kipekee ikiwamo urefu unaopendeza, shepu ya Kiafrika kabisa, wasomi na wanaotaka kufahamu kila jambo.

Kitu kinachowafanya wawe juu licha ya kuwa warembo, ni wachapa kazi wanaojali muda na kupigania wanachokitaka bila kujali wanapambana na nani na ana nafasi gani ikiwamo kutoogopa mashindano na wanaume katika nyanja mbalimbali ikiwamo za kisiasa, kielimu au kiutendaji.

3: Somalia

Sifa yao maarufu na wanayopendwa kuitwa na wanaume wa nchi yao ni “Vita Aiharibu Urembo”, mwaka jana walishika nafasi ya pili. Licha ya urembo na kuwa karibu maeneo mengi katika Bara la Afrika bado wana utamaduni wa kuoana wao kwa wao. Wanatajwa pia kuwa miongoni mwa wanawake wanaoamini katika ndoa na kuitendea haki.

2: Eritrea

Ni miongoni mwa nchi zenye wanawake wenye mvuto barani Afrika, licha ya asilimia kubwa ya wanawake wake kujihifadhi kwa kuvaa ushungi na mavazi marefu bado asili ya urembo wao ipo pale pale.

1: Ethiopia

Wanawake wa nchi hii huitwa “Asili ya Ubinadamu”. Huo ni utambulisho wao mbele ya macho ya dunia.

Inaelezwa kuwa ustaarabu kwa wanawake ulianzia katika Ethiopia, hivyo inatajwa kuwa ni nchi yenye wanawake wenye mvuto zaidi barani Afrika.

Wengine wanasema matokeo ya mvuto wao yanatokana na mchanganyiko wa watu wa kale wa Yemen na Ethiopia. Wakati mwingine inakuwa ngumu kuwatofautisha kutokana na baadhi yao kufanana sana, maumbile, sura na uzungumzaji.

VIDEO QUEEN MOSOGANGE AWA GUMZO MTANDAONI

$
0
0
Tanzanian socialite, Agnes Masogange has continued showing her beauty on Social Media after her pics she shared on her account, Agnes Masogange always hoping taking pics flaunting her hot body can increase her popularity, Men also are the one who feel crazy In her photos as she shared on social Media, See her more pics;
 
 

TAZAMA JINSI DIAMOND PLATINUMS ALIVYO COPY NA KUPASTE VIDEO YA JASON

$
0
0
SOKO la nyimbo katika dunia ya sasa linakuzwa na video za muziki, ubora wa video umekuwa ukichangia kuufanya wimbo kuwa mkubwa hata kama ni wa kawaida.
Kuna vitu vingi vinavyochangia video kuwa bora, baadhi ni ubora wa picha, ubora wa mandhari na ubora wa ubunifu wa kile kinachoonekana katika video husika.
Msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz anajulikana kwa kuwekeza nguvu kubwa kwenye kutengeneza video zenye kiwango cha juu, hilo halina ubishi.
Pamoja na sifa hizo, imekuwa ni kawaida kuona Diamond akiiga matukio kadhaa ya video za wasanii wa Marekani na kuziingiza kwenye video za nyimbo zake.
Mfanano wa video au jambo lolote ni kitu cha kawaida lakini kuna mazingira ambayo yanaweza kumfanya mpaka shabiki au mtazamaji wa video akaelewa kuwa hakuna mfanano wa bahati mbaya bali ni makusudi.

Watanzania 18 watekwa na waasi wa Congo

$
0
0
Waasi wanaodaiwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamewateka madereva 21, wakiwamo Watanzania 18 wanaofanya kazi kwenye kampuni ya malori ya mizigo ya Alistair ya nchini.

Meneja usimamizi wa Tanzania na DRC wa kampuni ya Alistair , Anna Joyce Mbise aliliambia gazaeti la Mwananchi  jana kuwa  madereva hao walitekwa asubuhi ya Juni 29, baada ya mapambano kati ya askari wa Serikali ya Congo na waasi hao.

“Kwa mujibu wa maelezo ya madereva hao ni kwamba askari wa Serikali waliokuwa wanawasindikiza kabla ya msafara kuvamiwa, walizidiwa kwenye mashambulizi hayo ndipo wakatekwa,” alisema Mbise na kuongeza:

“Wametueleza kuwa hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo, waasi wamekuwa wakizungumza nao vyema, lakini gari zetu tatu zimeharibika kwa risasi kutokana na mashambulizi hayo,” alisema.

Alisema kampuni hiyo imewasiliana na viongozi husika wa Serikali kwa kuandika barua Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ili wasaidie madereva hao kuachiwa huru wakiwa salama.

“Tumejawa na hofu kuhusu usalama wao, kwani tunaamini kwamba askari wa jeshi la Serikali lazima wanajipanga kurejea kupambana ili kulikomboa eneo hilo, hapo tuna wasiwasi na usalama wa madereva hao ,” alisema.

Mratibu wa Shirikisho la Wasafirishaji Afrika Mashariki (FEARTA), Emmanuel Kakuyu alisema taarifa walizonazo ni kwamba madereva hao wamekumbwa na mkasa huo katika eneo la kijiji cha Lulimba kilichopo kati ya Ziwa Tanganyika na Kindu Manyema.

Alisema waasi hawa hawajawadhuru madereva hao, lakini alifafanua kuwa madereva watatu kati ya 21 wanatoka Uganda.

“Watekaji wamekuwa wakizungumza nao vizuri ikiwamo kuwahakikishia usalama wao wakidai kwamba hawana ugomvi nao, bali wana ugomvi na Serikali ya Congo,” alisema.

Umbali kati ya Lulimba na Kigoma ni kilomita 448, lakini ili ufike Lulimba ni lazima ulizunguke Ziwa Tanganyika upande wa mashariki mwa DRC.

Kaimu Mkurugenzi wa dawati la Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suleiman Saleh alijibu kwa kifupi kwamba wamepokea taarifa za utekaji huo na tayari wameanza kushughulikia.

IGP SIRRO ATEUA MSEMAJI MPYA WA JESHI LA POLISI

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro.
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amemteua Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Barnabas Mwakalukwa kuwa msemaji mpya wa jeshi hilo, akichukua nafasi ya Kamishina Msaidizi, Advera John Bulimba ambaye atapangiwa kazi nyingine.



Kamishina Msaidizi, Advera John Bulimba.
Uteuzi wa Mwakalukwa unatajwa kuwa moja ya harakati za IGP Siro kulifanyia mabadiliko jeshi hilo, katika kuboresha utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kujizatiti na mapambano ya uhalifu.
Kabla ya uteuzi huo, Kamishina Msaidizi Mwakalukwa amelitumikia Jeshi la Polisi kwa nafasi na nyadhifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Kamanda wa Oparesheni wa mikoa mbalimbali pamoja na ngazi zingine za utumishi wa juu.

BINTI AMUUA MPENZI WAKE KWA MZAHA KATIKA YOU TUBE ILI KUPATA UMAARUFU

$
0
0
Mwanamke mmoja mjini Minesesotta nchini Marekani amehukumiwa kwa kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake katika kile kinachosemekana ni mgogoro wa mtandaoni.Monalisa Perez mwenye umri wa miaka 19 aliwekwa kizuizini baada ya kumpiga risasi Pedro Ruiz alipokuwa akshikilia kitabu katika kifua chake akidhani kitazuia risasi hiyo.Wawili hao wana mtoto wa miaka mitatu na takriban watu 30 walikuwa wakiangalia video hiyo ya YuTube alipompiga risasi mpenziwe.Shangazie Ruiz anasema kuwa walifanya kitendo hicho ili kuimarisha ufuasi wao katika katika mitandao ya kijamii.Claudia Ruiz aliambia runinga ya WDAY-TV kwamba binamu yake alimwambia kwamba alitaka kufanya kitendo hicho '' kwa sababu walihitaji kupata wafuasi zaidi''. ''tunataka kuwa maarufu''.
''Aliniambia kuhusu wazo hilo na nikamwambia'',''Musafanye hivyo''.
''Kwa nini utumie bunduki? Kwa nini?'', Claudia Ruiz aliambia chombo hicho cha habari.
''Walikuwa wakipendana sana'',alisema.''ulikuwa mzaha uliofanyika kimakosa''.

Bob Marley Alikataa kuandika urithi kwa kuamini kuwa marastafari huwa hawafi

$
0
0
 
Alikataa kuandika urithi kwa kuamini kuwa marastafari huwa hawafi.
Robert Nesta Marley,ambaye baadaye alikuja kujulikana kama Bob Marley,alizaliwa Februari 6,1945 katika kijiji cha Nine Mile kwenye Parishi ys mtakatifu Ann huko Jamaica.
Baba yake Norval Sinclair Marley alikuwa mzungu na mama yake Cedelia Booker alikuwa Mjamaica mweusi.Historia ya maisha yake haitofautiani sana na wanamuziki wenzake wa reggae Peter Tosh aliyelelewa na shangazi yake na Bunny Wailer aliyelelewa na baba yake zaidi,ni historia ya huzuni iliyo muacha Bob Marley chini ya mzazi mmoja(mama yake) pale alipofiwa na baba yake akiwa na umri wa miaka kumi tu.
Norval Sinclair (baba yake Bob Marley) alikuwa nahodha wa meli na muangalizi wa mashamba,alikufa mwak 1955 akiwa safarini,wakati huo alikuwa na umri wa miaka 60.
Kifo hicho kilimfanya mama yake Bob Markey ahamishe makazi kwenye mji wa Kingston,huko Bob alikutana na Bunny Wailer wakawa marafiki na kujifunza muziki pamoja.Akiwa na umri wa miaka 14,
Bob Marley aliacha shule na kujiunga na chuo cha ufundi wa kuchomelea vyuma,muda wakewa kupumzika alikuwa na Bunny Wailer kwenye muziki,kipindi hiko mwalimu wao alikuwa Joe Higgs,

Muimbaji wa mtaani mwenye imani ya kirastafari.Chini ya Joe Higgs walikutana na Peter Tosh na kuungana naye.

Mwaka 1962 Bob Marley alirekodi nyimbo zake mbili za kwanza ambazo ni;"Usihukumu"(judge not) na "kikombe kimoja cha chai"(one cup of tea) chini ya muandaaji Leslie Kong,

lakini nyimbo hizo hazikukubalika sana.Mwaka 1963 akashirikiana na Bunny Wailer,Peter Macintosh(Peter Tosh),Junior Braithwaite,Beverly Kelso na cherry Smith n kuunda kundi la "The Teenagers" kundi hilo lilijibadili majina na kuwa "The wailing rude boys","The wailling wailers" na mwishowe "The wailers".

Mwaka 1964 na 1965 watoa vibao vikali kama "Usiwe na wasiwasi"(simmer down) na "Nafsi isiyokubali"(soul rebel)nyimbo hizi zilikonga nyoyo za Wajamaika wengi

Hata hivyo kufikia mwaka 1965 lilibakiwa na wakali watatu tu,yaani Bob Marley,Bunny Wailer n Peter Tosh,baada ya wengine kujiengua.

Mwaka 1966 Bob Marley alimuoa kimwana Rita Anderson na kwenda kuishi kwa muda na mama yake huko Wilmington,Delaware nchini Marekani..

Na kuibuka na imani kali ya kirastafari na kuja na mtindo wa kufuga nywele uitwao "dreadlocks".

Baada ya hapo Bob Marley na kundi lake la The wailers walitoa vibao kemkem vilivyoitikisa Dunia.

Kati ya vibao hivyo ni;Africa unit,Zimbabwe,Could oyu loved?,Iron lion zion,Is this love,Buffalo soldier na vingine vingi.

Huyo ni Bob Marley,mfalme wa reggae aliyepinga ubaguzi kwani hata yeye mwenyewe alisema "Wananiita chotara,lakini mimi siegamii upande wowote bali nipo upande wa Mungu aliye niumba kutoka kwa weusi na weupe".

Hiyo ni biograph ya mwanaharakati huyo wakupinga ubaguzi."REST IN PEACE RASTAFARAE"

JAMANI Naombeni Msinilaumu Kwa Uamuzi Huu Niliouchukua Kwa Mume Wangu

$
0
0

Mimi nimeolewa miaka 15 sasa na tumejaaliwa watoto 4. Ndoa yetu ilipofikisha miaka 4-5 mume wangu alicheat, nikamkamata through sms akapinga sn lakini baadae alikubali akakiri kosa na kuomba msamaha. nikamsamehe

Tumeendelea kuishi na nilipopata mtoto wa tatu akanicheat tena, safari hii alikuwa nje ya nchi kimasomo, napo alikiri na kuomba msamaha, nikamsamehe

wakati niko mjamzito mimba ya mtoto wa nne alinicheat tena, kibaya zaidi alinicheat na house girl wng akampa ujauzito. kwa ivo wkt mimi nina mimba na House girl naye mjamzito(japo sikujua km house girl alikuwa mjamzito kwani aliondoka nyumbani) niligundua baadae kuwa mtt wa aliyekuwa house Girl wangu ni wa mume wangu

kama kawaida yake akaomba msamaha safari hii hadi kupiga goti na kulia ili nimsamehe...na mimi kwa kuwa bado nampenda na nimemvumilia kwa mengi nikaamua kumsamehe tena..ila tulikubailana masharti mengi na akakubali masharti yote niliyompa..mwanzoni alibehave vizuri sn akawa muwazi kwng hanifichi chochote kuhusu huyo mtt.. na tuliishi maisha ya furaha kwn alinijali mno na alionekana kweli amerigrate.
sasa cha kushangaza siku za karibuni amebadilika san, amekuwa msiri na hasemi chochote kuhusu huyo mtt wa nje..siku hizi anatuma hela kwa siri na pia anawasiliana na huyo mama wa mtoto kwa siri haniambii chochote..

nilipoona mabadiliko niliamua kumuuliza imekuwaje tena mbona siri tena wkt tulikubaliana kila kitu kiwe open? hakunijibu isipokuwa alikuwa mkali na kufoka na kusema hilo swala tumeshamalizana nalo sitaki kulisikiasikia tena..
nikajaribu tena siku nyingine kumuuliza na majibu ndio hayo hayo, kwa kifupi hataki na anakwepa kuzungumzia hilo suala kabisa...sasa najiuliza kwa nini anafanya siri? km hakuna jambo lolote baya basi anaficha nini? ina maana kuna kitu zaidi ya mtoto.

Sasa jamani mimi nimeamua km ifuatavyo
1. Na mimi nimeamua kuwa na mahusiano nje ya ndoa, jamani msinilaumu nami pia nahitaji kuliwazwa na kufarijiwa kwa kifupi nimechoka na mastress yasiykuwa na mwisho, sikuwahi kumcheat mume wng ktk maisha yote ya ndoa. ila sasa atanisamehe tu ht akijua wl sijali, nipo tayari kwa lolote..
2. Sina mpango wa kuondoka kwenye nyumba tuliyojenga pamoja nitaishi hapa hapa kwani sipendi wtt wng walelwe na mzazi mmoja..wtt hawajui kinachoendelea in fact hata ndugu na jamaa hawajui chochote kwani mimi sijawaambia na wala sijawahi kuwaeleza matatizo ya ndoa yng..kwa nje tunaonekana familia iliyobarikiwa na ina furaha lkn wenyewe ndio tunaojua ndani kukoje
3. Kwa sababu sisemagi matatizo yangu kwa ndugu na marafiki nimeamua kuweka hapa labda nitapunguza kitu fulani kichwani kwani sometime naona km nazidiwa mawazo vile

Magazeti ya Leo Tanzania Jumatatu July 3,2017

BONDIA MANNY PACQUIAO ADUNDWA NA MWALIMU

$
0
0
Manny Pacquiao anaonekana kuendelea kupokea vichapo, na sasa amepokea kipigo kutoka kwa Jeff Horn ambaye kabla ya kuwa bondia alikuwa ni mwalimu katika pambano la raundi 12 lililopigwa nchini Australia.Jeff Horn alionekana kumshambulia Manny Pacquiao kuanzia raundi ya kwanza ya mpambano huo, japokuwa mwanzo Pacquao alionekana kujaribu kujitetea.Pacquiao alionekana kuzidiwa zaidi kadri pambano lilivyokuwa likiendelea kwani ngumi alizokuwa akipigwa na Horn zilionekana kumchana pembeni ya jichoPamoja na kushambuliwa sana lakini ilipofika raundi ya 9 Horn alionekana kuanza kupata tabu kutokana na ngumi za kushtukiza na za haraka zilizokuwa zikirushwa na Pacquiao.
Baada ya mpambano huo kura za majaji watatu zilimpa ushindi Horn kwa alama 117-111, 115-113 na 115-113 na kumfanya Horn kuwa bingwa wa WBO WORLD WELTERWEIGHT.
Pacquiao 38 ambaye ni raia wa nchini Ufilipino kwa sasa anakuwa amepoteza mapambank manne kati ya tisa aliyocheza mara ya mwisho hii ikiwa ni rekodi mbaya sana kwake.

Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Wake Wanyimwa Dhamana na Kurudishwa Rumande

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa wamenyimwa dhamana kwa kesi inayowakabili, wamerudishwa rumande mpaka Julai 17 mwaka huu shtaka lao litakaposomwa tena.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri baada ya mabishano makali ya kisheria dhidi ya mawakili wa utetezi na mawakili upande wa jamhuri (serikali).

Malinzi na Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mnamo Juni 27 kwa kutuhumiwa matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao na kupandishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Juni 29 na kusomewa mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.

JAHAZI la Rugemalila na Seth Wa IPTL Lazidi Kuzama..Waongezewa Mashtaka Mapya 6

$
0
0


Mfanyabiashara  Harbinder  Singh Sethi na James  Rugemalira wamepandishwa kizimbani kwa mara nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 12, badala ya mashtaka sita waliyosomewa awali.

Miongoni mwa mashtaka hayo 12 ya  uhujumu uchumi yamo mashtaka matano ya kutakatisha fedha na kuisababisha hasara ya USD 22, 198, 544.60 na Sh 309,461,300,158. 27.

Akiwasomea hati mpya ya mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shedrack Kimaro kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alidai wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kighushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kuisababishia Serikali hasara na kutakatisha fedha.

Washtakiwa hao katika shtaka la kwanza wanadaiwa, Rugemarila ambaye ni Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP wanadaiwa kuwa   kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19, 2014 jiji Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Kimaro alidai katika shtaka la pili la kujihusisha na mtandao, washtakiwa hao kati ya Oktoba 18, 2011na Machi 19, 2014 jijini Dar es Salaam wakiwa siyo watumishi wa umma na watumishi wa umma  walitekeleza mtandao huo wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.

Kwa upande shtaka la tatu, Sethi  anadaiwa  kuwa   Oktoba 10, 2011 katika mtaa wa Ohio Ilala Dar es Salaam akiwa na nia ya ulaghai alighushi fomu namba 14 ya usajili wa makampuni  na kuonyesha yeye ni mtanzania anayeishi Kitalu namba 887 Mtaa wa Mrikau Masaki wakati akijua ni uongo.

Seth katika shtaka la nne anadaiwa kutoa nyaraka ya kughushi ambayo ni fomu namba 14a ya usajili wa kampuni kwa ofisa msajili wa kampuni, Seka Kasera kwa njia ya kuonyesha kwamba yeye ni mtanzania na Mkazi wa Mtaa wa Mrikau.

Katika shtaka la tano, washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya  Novemba 28/29, 2011 na Januari 23, 2014 makao makuu Benki ya Stanbic Kinondoni  na Benki ya Mkombozi Tawi St Joseph kwa ulaghai washtakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), walijipatia USD 22,198,544.60 na Sh 309, 461,300,158.27. 

Katika shtaka sita la kusababisha hasara,  washtakiwa hao wanadaiwa kuwa   Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la  kati Kinondoni kwa vitendo vyao waliisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198, 544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Kimaro alidai katika la saba, kuwa kati ya Novemba 29, 2013 na Januari 23, 2014 maeneo tofauti Dar es Salaam kwa pamoja walitenda kosa la kutakatisha fedha kwa kuchukua fedha kutoka BoT USD 22,198,544.60 na Tsh 309,461,300, 158.27 wakati wakijua fedha hizo zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Shtaka la nane, Kimaro alidai kuwa Novemba 29, 2013 katika tawi la kati la Benji ya Stanbic Tanzania Wilaya ya Kinondoni Sethi alitakatisha fedha kwa kuchukua BoT USD 22,198,544.60 wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Kwa upande wa shtaka la tisa, Sethi anadaiwa kuwa kati ya Novemba 29, 2013 na Machi 14,2014 katika tawi la kati la Benji ya Stanbic Kinondoni Dar es Salaam alitakatisha fedha, Sh 309,461,300,158.27 kutoka BoT wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Shtaka ya kumi,  inadaiwa Januari 23, 2014 katika Benki ya Mkombozi tawi la St Joseph Cathedral, Rugemalila  alitakatisha fedha, Sh 73, 573, 500,000 kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Kwa upande wa shtaka la 11, Kimaro alidai kuwa Januari 23,2014 katika Benki ya Mkombozi tawi la St Joseph Cathedral, Rugemarila alitakatisha fedha USD 22,000,000 kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo ni zao la uhalifu.

Shtaka la 12, Seth anadaiwa kuwa Januari 28, 2014 katika tawi la kati la Benki ya Stanbic Wilaya ya Kinondoni alihamisha Rand (zar 1,305,800 kwenda kwenye akaunti namba 022655123 katika Standard bank Land Rover Sandton Johannesburg wakati akijua katika kipindi anahamisha fedha hizo zimetokana na zao la kujihusha na genge la uhalifu.

Washtakiwa hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hao.

Upande wa mashtaka ulidai upelelezi bado haujakamilika na washtakiwa wamepelekwa rumande hadi Julai 14, 2017.

Hata hivyo mashtaka ya kutakatisha fedha yanayowakabili washtakiwa hao hayana dhamana.

Hizi Hapa Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo

MZAZI MWENZA WA YOUNG D ABANWA KUHUSU KUMWACHA MTOTO UKWENI

$
0
0
Mamisa amir, mzazi mwenzake na Young D
BAADA ya kudaiwa kumuacha mwanaye mchanga mwenye umri wa miezi saba kwa bibi yake ambaye ni mama mzazi wa mwanamuziki David Genzi ‘Young D’, mwanamama, Mamisa Amir amebanwa juu ya ishu hiyo na kueleza sababu ya kufanya hivyo.


Kwa mujibu wa chanzo makini, kwa sasa mtoto huyo wa kike aitwaye Tamar yupo kwa bibi yake maeneo ya Tabata baada ya Young D kushindwa kuelewana na Mamisa hivyo mama mzazi wa Young D kuamua kumchukua mjukuu wake huyo.
David Genzi ‘Young D’
Akizungumza na Wikienda baada ya kubanwa kuhusu ishu hiyo, Mamisa alikiri Tamar kulelewa na mama wa Young D kufuatia makubaliano yaliyofanyika ambapo mama huyo alisema apewe amlee mjukuu wake.

“Mapenzi hakuna tena kati yangu na Young D, ndiyo maana familia yake iliamua kumchukua Tamar ili kumlea kwani nisingeweza kumlea kwa sababu ninafanya kazi. Nikitaka kwenda kumuona ninakwenda kama kawaida na hata nikitaka kulala huko wiki moja, ninalala,” alisema Mamisa.

KUTOKA BUNGENI DODOMA:YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 58 MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JULAI 3, 2017

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Tulia Ackson akiongoza kikao cha hamsini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 3, 2017.

Viewing all 7853 articles
Browse latest View live