Quantcast
Channel: LEWIS MBONDE BLOG
Viewing all 7853 articles
Browse latest View live

Lowassa Ampa Big Up Rais Magufuli Juu ya Hatua Alizochukua Katika Sakata la Mvhanga wa Madini

$
0
0

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa hatua anazozichukua kuhusu madini ya nchi yetu. 
Lowassa  aliyayasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la mchanga wa madini (makinikia) ambalo limeonyesha kuwa Tanzania impoteza zaidi ya trilioni 100 tangu mwaka 1998 hadi Machi mwaka 2017.
“Nimpongeze sana Mhe Rais John Pombe Magufuli kwa uamuzi na hatua ambazo amechukua kuhusu jambo hili, na hasa pale anapowashirikisha wananchi, ni jambo muhimu sana." Alisema Lowassa
Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alisema anampongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza maamuzi ambayo ni ya UKAWA kwani kipindi anazunguka kuomba kura kwa wananchi alipopita maeneo yenye madini aliyazungumza haya yanayotekelezwa leo.
“Nampongeza kwa kutekeleza yale maamuzi ambayo ni ya UKAWA. Nilipokuwa kwenye kampeni ya kuomba kura, hata pale Geita, nilieleza jambo hilo, nikasema hivyo hivyo alivyosema yeye kwamba nikiingia madarakani nitaunda tume ya kuchunguza jambo hili ili mtanzania awe ndiye anapata sehemu kubwa ya faida kuliko mgeni.”
Aidha, Lowassa amesema kuwa, ni kweli mikataba ya madini ina matatizo na hata yeye alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu aliwaita wawekezaji hao wakakaa na kuzungumza, lakini jambo gumu lilikuwa ni kwamba, mikataba ukishaiweka saini inakuwa migumu sana kubadilisha.
Lowassa alieleza kwamba baada ya kuongea nao kwa muda walikubali na kuongeza kidogo mirahaba lakini haikutosha.
“Matumaini yangu ‘figure’ (namba) hizo ni za kweli, kama ni za kweli, tumeliwa kweli kweli,” alisema Lowassa alipokuwa akizungumzia mahesabu yaliyowasilishwa katika ripoti za uchunguzi kuhusu kiasi cha fedha ambazo Tanzania imepoteza.
 Aidha, Lowassa alisema kuwa sera za Chama cha Mapinduzi (CCM) ndiyo zimefikisha nchi hapa kwani wakati wabunge wa CCM wanapiga kura kukubali mikataba hiyo walikuwa wakitimiza sera za chama hicho. kwahiyo vyama pinzani havina tatizo.
Hivyo alieleza kuwa kikubwa kinachohitajika ni kupatikana kwa katiba mpya ambayo itazingatia mambo hayo ya msingi na haki za raia.

Wema: Ustaa ni Mateso, Niacheni

$
0
0
“NAHITAJI kupumzika sasa, nimechoka kuhusishwa na mambo yasiyo na mashiko. Kwakweli nimechoshwa na ninaumizwa sana na hii hali,” ndivyo anavyosema msanii wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu.
https://www.sde.co.ke/sdemedia/sdeimages/friday/efqvidw0kte8wv58a67e9d5ebec.jpg
Wema ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2006, amezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya clip inayosikika sauti inayodaiwa ni yake akizungumza kimahaba na mtu anayedaiwa kuwa ni Freeman Mbowe, Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chadema, taifa.
Katika clip hiyo iliyoanza kusambaa kwa kasi tangu wikiendi iliyopita, sauti inayodaiwa kuwa ni ya Wema na ile inayoelezwa ni ya Mbowe, wanazungumza katika hali ya mahaba huku wakionekana kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Mwanamume kwenye clip hiyo (anayedaiwa kuwa ni Mbowe), anajaribu kumuomba msamaha mwanamke (anayedhaniwa kuwa ni Wema) na kumtaka aende Kilimanjaro kwa mazungumzo zaidi katika siku za mwisho wa wiki.
Tayari Mbowe ameshakanusha vikali kuwa sauti ile siyo yake, bila kufafanua zaidi, akitaka muda uachwe uzungumze kwa vile suala hilo linafanyiwa kazi kwa upande wao.
Wema ameibuka na kueleza masikito yake kwa kuhusishwa katika clip hiyo akidai kuwa anaumizwa na namna watu wanavyomfuatafuata na kumchafulia jina lake.
Wema ameliambia Swaggaz kuwa, amekuwa akijitahidi sana kukaa mbali na vyombo vya habari ili asiripotiwe vibaya lakini anaona haisaidii.
“Nimeamua nikae mbali na mitandao, nitulie nifanye mambo yangu lakini naona haisadiii. Siyo siri nimechoshwa na hii hali, natamani atokee staa mwingine abebe huu mzigo nami nipumzike ili niweze kufanya majukumu yangu niliyonayo.
“Nafahamu Watanzania wana shida nyingi, nami nimejipanga kuwa mtetezi wao hasa wanawake na wasichana kwa ujumla.
“Nimejitahidi kukaa kimya kwa muda mrefu na kupotea  kwenye mitandao ni  na sehemu za starehe kwa kujichimbia nikifanya mambo yangu na kutafakari namna ambayo nitakitumikia chama changu (Chadema) lakini binadamu bado wameendelea kuniandama ili wapate cha kuniongelea,” anasema Wema na kuongeza:
“Kweli kabisa… huu ustaa sasa naona ni mzigo kwangu. Natamani atokee msichana mwingine awe staa kunizidi ili na yeye aandikwe sasa. Kila siku Wema, why? Nakwazika sana kwa kweli.”
KINACHOMKERA ZAIDI
Wema anasema anachukizwa sana na tabia ya kuzushiwa mambo, kwani anaweza kuwa karibu hata na ndugu yake, akazushiwa ni mpenzi wake.
“Nakerwa mno ninapokuwa na mwanamume karibu hata kikazi nasingiziwa kuwa ni mpenzi wangu, hii ni kero. Naomba nisionekane mwanamke wa kila mtu, sasa niheshimiwe kama wengine wanavyoheshimiwa.
“Ninapokuwa karibu na mtu wa jinsia nyingine nisifikiriwe kutoka naye kimapenzi, kwa kuwa kuna watu ninawaheshimu kama Mwenyekiti…
“Hii imeniumiza hadi nilitamani kuachana na siasa ila mama yangu, ndugu zangu na Mwenyekiti mwenyewe wamenipa moyo na hapo ndipo nimepata nguvu za kufanya kazi kwa nguvu kuliko hapo awali,” anasema Wema.
AFAFANUA KUHUSU CLIP
“Sina uhakika kama ni sauti yangu kwa kuwa sikumbuki siku wala saa niliyoongea maneno hayo, hivyo kazi hiyo naiacha chini ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ‘TCRA’ ili kubaini ukweli wa jambo hili.
“Kwa sasa sihitaji kuhusika wala kuliongelea kwa kina, nina uhakika ukweli utajulikana na sheria itachukua mkondo wake,” anasema Wema.
MIKAKATI YAKE
“Kwa sasa mikakati yangu ni kukitumikia chama changu kwa kuleta wanachama wengi zaidi kuhakikisha uchaguzi ujao kinafanya vizuri na kushinda ushindi wa kishindo.
“Hilo wapinzani wangu wanalijua na ndiyo maana wanatafuta skendo zisizo na maana ili kunirudisha nyuma ila ndiyo wamenipa nguvu ya kufanya kazi kwa kasi na kuniweka katika nafasi ya kujua siasa ni mchezo wa aina gani,” anasema.
MALENGO YAKE
“Malengo yangu ni kuwa kiongozi na hilo linajulikana kwa sababu uwezo ninao, nia ninayo na nguvu za kuwatumikia wananchi ninazo hivyo siasa zao za majitaka kwangu hazitakuwa na nafasi.
“Kama walikuwa wanajua Wema ni yule wa zamani, wa kukwazwa na vitu visivyo na msingi hilo wamenoa. Wema huyu ni kamanda ambaye anajiamini na kujitambua na nitasimama kutetea haki za wanyonge kama ilivyo sera ya chama changu,” anasema.
Mtanzania

Breaking Newzz:Rais Magufuli Akutana na Acacia Ikulu leo, wakubali kulipa fedha wanazodaiwa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

Prof. John L. Thornton ambaye amesafiri kwa ndege binafsi kutoka nchini Canada hadi Tanzania amekutana na Mhe. Rais Magufuli leo Juni 14, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam na mazungumzo yao yamehudhuriwa na Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini maslahi ya pande zote mbili.

Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa Prof. John L. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu (smelter) hapa nchini.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amevionya vyombo vya habari vinavyowataja Marais wastaafu Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kuwahusisha na taarifa za kamati mbili za uchunguzi wa madini yaliyo katika makontena yenye mchanga wa madini (Makinikia) ambao ripoti zimekabidhiwa kwake na kamati hizo.

“Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Mzee Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, viwaache wapumzike” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Juni, 2017

Hatimaye 'Pedeshee Ndama' huru kwa dhamana

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

Baada ya kufanikiwa kulipa faini ya milioni 200 hatimae leo mfanyabiashara , Ndama Shabani Hussein, maarufu kama Pedeshee Ndama mtoto ya Ng'ombe amepata dhamana.
Ndama amepata dhamana baada ya kuwa na wadhamink wawili na kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 600.
Wiki iliyopita Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimtia hatiani Ndama na kumuhukumu kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya milioni 200 baada ya kukiri shtaka la kutakatisha USD 540,000.
Aidha mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa ilimsomea masharti ya dhamana mshtakiwa huyo iwapo angefanikiwa kulipa kiasi hicho cha milioni 200 ili awe huru katika mashtaka matano yanayoendelea kumkabili mahakamani hapo ambayo upelelezi wake bado haujakamilika.

Katika masharti hayo, Ndama alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika na atoe fedha taslimu kiasi cha USD 270,200 ambacho ni sawa na zaidi ya milioni 600 mahakamani hapo ama mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha
Licha ya kupata dhamana, Ndama amerudishwa gerezani kukamilisha taratibu kabla ya kuachiwa huru. 

Hukumu hiyo ya shtaka la sita la kutakatisha fedha ilitolewa baada ya Wakili wa Serikali, Christopher Msigwa kumsomea maelezo ya awali (PH) Ndama na kuyakubali maelezo ya awali na maelezo yote yanayounda shtaka hilo la kutakatisha fedha, akapatikana na hatiani na kupewa adhabu hiyo.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili Msigwa aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa amekubali shtaka la sita la kutakatisha fedha na maelezo yanayounda shtaka hilo, hawana kumbukumbu za nyuma za makosa dhidi ya Ndama ila ni rai ya upande wa mashtaka kuwa wakati mahakama ikitoa adhabu izingatie matakwa ya kifungu cha 13(a) cha sheria ya kuzuia utakatishaji fedha.
Pia mahakama ibebe dhana ya sheria hiyo ambayo lengo lake ni kuzuia makosa ambayo yanalenga kudidimiza uchumi wa nchi na uzito wa kosa ambalo mshtakiwa amelifanya.
Kwa upande wa Wakili Wabeya Kung’e anayemtetea mshtakiwa huyo kwa kushirikiana na Jeremiah Mtobesya, Kung’e aliiambia mahakama kuwa ni wazi mshtakiwa amekiri kosa baadaya kusomewa maelezo ya awali ni rai yetu mahakama isitoe adhabu kali kwa mshtakiwa .

Aliiomba mahakama izingatie maombi yao kwa sababu mshtakiwa huyo hilo ndiyo kosa lake la kwanza, kitendo chake cha kukiri kosa kinaonesha kusikitikia kosa alilolitenda na kwamba anayo familia ambayo inamtegemea ambao kwa kipindi cha mwaka mmoja ambacho amekaa ndani imepata shida kwa kukosa huduma yake.
“Kwa kuzingatia kifungu cha 13(a) cha sheria ya kutakatisha fedha ni rai yetu mahakama tukufu isitoe adhabu kali kwa mshtakiwa kwa sababu amejutia kosa alilolitenda”Alisisitiza kueleza Kung’e. Hivyo amehukumiwa kulipa faini ya Sh 200 milioni ama akishindwa kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.
Juni 6,2017 Ndama aliiomba mahakama akumbushwe shtaka, akakumbushwa na Wakili wa Serikali, Esterzia Wilson na akalikubali shtaka hilo.
Akisomewa maelezo ya awali mahakamani hapo, Ndama alikubali maelezo ya awali aliyosomewa ikiwamo nyaraka zilizotumika kufungua akaunti iliyotumika kuingizwa hizo fedha, hundi 18 zilizotumika kutolea hizo fedha, maelezo ya benki ‘bank statement’ na Swift massage.

Amekubali kuwa Mei 14,2013 wakurugenzi ambao pia ni wanahisa wa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited wanaotambulika Brela, Bushoboka Mutamura na Mujibu Hamis Taratibu waliisajili kampuni hiyo Brela na kupata hati ya usajili namba 99249 kwa ajili ya kushughulikia biashara ya madini.

Aliendelea kukubali kuwa Septemba 16,2013 alifungua akaunti benki ya Stanbic katika tawi la Viwandani kwa kuwasilisha nyaraka mbalimbali ikiwamo TIN namba ya kampuni hiyo, leseni ya biashara na hati yake ya kusafiria nakwamba wakati akiifungua alijitambulisha kuwa yeye ndiyo Mwenyekiti wa kampuni hiyo na mtia saini pekee.

Pia alikubali kuwa kampuni ya kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliingia mkataba na kampuni ya Trade TJL DTYL Limited ya Australia na kwamba aliwagaia wabia wenzake fedha hizo taslimu kwa lengo la kuficha chanzo chake.

Katika shtaka hilo la sita la kutakatisha fedha Ndama anadaiwa kuwa kati ya Februari 26 na Machi 2014, Dar es Salaam, akiwa mwenyekiti na mtia saini pekee wa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Limited na akaunti ya benki ya kampuni hiyo iliyoko kwenye benki ya Stanbic alijihusisha moja kwa moja kwenye uhamishaji wa dola za Marekani 540,000 na kuzitoa huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la uhalifu la kujiapatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Ndama alilikubali shtaka hilo na kukana makosa mengine yakiwemo ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Miongoni mwa mashtaka yanayoendelea kumkabili, Ndama anadaiwa Februari 20, 2014 Dar es Salaam, alighushi nyaraka ya kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha maboxi manne ya dhahabu yenye kilogramu 207 yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000.00 kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.
Pia anadaiwa Machi 6, 2014, Dar es Salaam, alighushi kwa kutengeneza hati ya kibali ya Umoja wa Mataifa ofisi ya Dar es Salaam akijaribu kuonesha kilogramu 207 za dhahabu kutoka nchini Congo zinatarajiwa kusafirishwa na kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited, zimesafirishwa bila jinai yoyote wakati akijua si kweli.
Aidha anadaiwa Februari 20, 2014, alighushi fomu ya forodha yenye namba za usajili R.28092 akionesha kampuni ya Muru imeilipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) dola za Marekani 331,200 kama kodi ya uingizaji wa bidhaa ambazo zina uzito wa kilogramu 207 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000 kutoka Congo.
Shtaka lingine anadaiwa Februari 20, 2014, alighushi nyaraka ya bima kutoka Phoenix of Tanzania Assurance Company Ltd akionesha kampuni ya Muru imeyawekea bima maboxi manne yaliyokuwa na dhahabu hizo.
Anadaiwa kati ya Februari 26 na Machi 3, 2014, Dar es Salaam kwa njia ya udanganyifu alijipatia kutoka kwa kampuni ya nchini Australia ya Trade TJL DTYL Limited Dola za Marekani 540,000 baada ya kudanganya atawapa na kusafirisha dhahabu hizo. Kesi hiyo itatajwa Juni 16,2017.

Urusi Yaionya Marekani.....Yasema Itatungua Ndege Yoyote ya Muungano Unaoongozwa na Marekani

$
0
0
Urusi imeonya kuwa itashambulia ndege za muungano unaoongozwa na Marekani nchini Syria iwapo ndege hizo zitapaa katika maeneo ambayo jeshi lake linahudumu.

Hii ni baada ya ndege ya kivita ya Marekani kutungua ndege ya kivita ya serikali ya Syria.

Muungano huo unaoongozwa na Marekani ulisema ndege yake moja  ilitungua ndege ya Syria aina ya Su-22 baada ya ndege hiyo kuwaangushia mabomu wapiganaji  waasi wanaoungwa mkono na Marekani katika mkoa wa Raqqa, Jumapili.

Urusi, mshirika mkuu wa serikali ya Syria, imesema pia kwamba itakatiza mawasiliano yote na Marekani ambayo lengo lake huwa kuzuia ajali angani.

Syria imeshutumu shambulio hilo la Marekani na kusema litasababisha "matokeo mabaya sana".

"Ndege yoyote, ikiwa ni pamoja na ndege za kawaida na ndege zisizokuwa na rubani ambazo ni za muungano wa kimataifa unaohudumu magharibi mwa mto Euphrates, zitafuatiliwa na majeshi ya kukabiliana na ndege angani na ardhini na zitachukuliwa kama kitu kinachofaa kushambuliwa," wizara ya ulinzi ya Urusi  imesema.

Urusi imekanusha madai kwamba Marekani ilikuwa imewasiliana na maafisa wa urusi kabla ya ndege hiyo aina ya Su-22 kutunguliwa.

Maafikiano kati ya Urusi na majeshi ya muungano unaoongozwa na Marekani ya kushirikiana kuzuia ajali angani na pia kuhakikisha usalama yalifika kikomo Jumatatu, wizara hiyo iliongeza.

Hii si mara ya kwanza mawasiliano kusitishwa kati ya pande hizo mbili.

Aprili, mawasiliano yalisitishwa baada ya Marekani kurusha makombora aina ya 59 Tomahawk katika kambi ya ndege za kijeshi ya Shayrat, nchini Syria.

Marekani ilishambulia baada ya Syria kudaiwa kutekeleza shambulio la kemikali katika maeneo yaliyoshikiliwa na waasi katika mkoa wa Idlib.

Lakini mataifa hayo mawili yalifufua mawasiliano yao mwezi uliopita.

Ndege hiyo ya kivita ya Syria aina ya Su-22 ilitunguliwa na F/A-18E Super Hornet karibu na mji wa Tabqa mkoa wa Raqqa Jumapili alasiri, wizara ya ulinzi ya Marekani imesema.

Inaaminika kwamba ndicho kisa cha kwanza kabisa cha ndege yenye rubani ya Marekani kutungua ndege nyingine ya kivita yenye rubani tangu vita vya Kosovo mwaka 1999.

Waasi wa Syrian Democratic Forces (SDF) wanaoungwa mkono na Marekani, wamekuwa wakihudumu eneo la Tabqa.

Credit: BBC

Magazeti ya Leo Tanzania Jumanne June 20,2017

Vigogo wa Escrow (James Rugemarila na Harbinder Sethi ) wafikishwa mahakamani Jana

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) aimewafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wafanyabiashara James Rugemarila na Harbinder Sethi kwa tuhuma za uhujumu uchumi na makosa mengine yanayofanana na hao.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa muda mrefu wamekuwa wakiulizwa kuhusu kesi ya Escrow hivyo sasa anaamini ni wakati muafaka wa kuwafikisha watuhumiwa hao wawili mahakamani.

Mlowola alisema kuwa taasisi hiyo imefanya uchunguzi wa kutosha kwa muda wote ambao ilikuwa kimya, na hivyo wamefikishwa mahakamani kisutu na baada ya hapo mahakama itafanya taratibu za kuhamishia kesi hiyo katika Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Kabla ya vigogo hawa wawili kufikishwa mahakamani leo, baadhi ya watumishi wa TANESCO tayari walishtakiwa kufuatia tuhuma za kupokea fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engeneering & Marketing ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), James Rugemalira.

Huu Hapa Uamuzi ya Mahakama kuhusu James Rugemalira na Harbinde Seth wa ESCROW

$
0
0
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia na Rushwa (TAKUKURU) jana Juni 19, 2017 iliwafikisha mahakamani wafanyabiashara wawili James Rugemalira na Harbinde Seth watuhumiwa wawili wa kesi za ESCROW na IPTL.

Watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ambapo wamesomewa mashtaka sita yanayowakabili likiwemo la uhujumu uchumi.

Akiwasomea mashtaka yao, Wakili wa Serikali, Paul Kadushi alidai Mahakamani hapo kuwa kosa la kwanza la kula njama linawakabili washtakiwa wote wawili ambapo inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Octoba 18, 2011 na March 19, 2014 katika maeneo tofauti ya DSM, Kenya, Afrika Kusini na India walikula njama kwa ajili ya kutenda kosa, ambapo walijipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Katika kosa la pili, la kujihusisha na mtandao wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida huku shtaka la tatu ni kughushi ambalo wakili Kadushi alieleza kuwa linamkabili Seth ambapo inadaiwa October 10, 2011 katika mtaa wa Ohio, Ilala DSM akiwa na nia ya ulaghai alighushi cheti cha usajili wa makampuni  na kuonesha yeye ni Mtanzania.

Aidha katika shtaka la kutoa nyaraka za kughushi ambalo pia linamkabili Seth ambapo anadaiwa alitoa nyaraka za kughushi katika Ofisi ya Msajili wa makampuni kwa nia ya udanganyifu akiwasilisha fomu namba 14 ya usajili wa makampuni ikionesha ni Mtanzania na mkazi wa mtaa wa Mrikau, Masaki Dar.

Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, wakili Kadushi alidai linawakabili washtakiwa wote wawili ambapo kati ya November 28 na 29, 2011 na Januari 23, 2014 katika Makao Makuu ya Benki za Stanbic na Benki ya Mkombozi tawi St. Joseph Dar  inadaiwa kuwa, kwa ulaghai washtakiwa hao wote wawili walijipatia Dollar 22,198,544.60 sawa na Tsh. 309b.

Wakili Kadushi alidai kuwa, shtaka la sita ni kusababisha hasara ambapo washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya November 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la kati Kinondoni kwa vitendo vyao waliisababishia Serikali hasara ya Dollar za Kimarekani, 22, 198, 544.60 sawa na Tsh. 309, 461,358.27.

Baada ya kuwasomea makosa hayo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu kitu kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka, ambapo wakili Kadushi alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kesi kutajwa.

Mahakama hiyo ilisema upelelezi bado unaendelea na haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa watuhumiwa hivyo walirudishwa rumande.

==>Hapo chini kuna hati ya mashtaka 6 yanayowakabiri

Wananchi Bukombe waomba Rais Magufuli aongezewe muda wa kukaa madarakani

$
0
0

Wananchi wa vijiji vya Bulangwa na Katente mkoani Geita,wameliomba Bunge la Tanzania kufanya marekebisho ya muda wa ukomo wa urais kutoka miaka kumi ya sasa hadi miaka ishirini ili kumuwezesha Rais Dk.John Pombe Magufuli kuendelea kubakia madarakani.

Wananchi hao walitoa ushauri huo jana katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mbunge wa jimbo la bukombe mh. Dotto biteko kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa namna alivyosimamia sekta ya madini,mkutano ambao ulihudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh.Costantine Kanyasu.

Akiwahutubia wananchi,Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini Mh. Dotto Biteko,alisema kazi ya kupigania rasilimali za taifa inayofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli si ya lelemama,huku Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh. Kanyasu akisema serikali ya awamu ya tano haiwachukii wawekezaji, bali inawachukia waporaji wa raslimali za nchi.

Ripoti ya kamati ya pili ya mchanga wa madini wa Makinikia,iliyowasilishwa Juni 12 mwaka huu kwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof.Nehemiah Ossoro ilibaini taifa kupoteza shilingi Trilioni 252 kupitia usafirishaji wa mchanga wa madini ya makinikia nje ya nchi kuanzia mwaka 1998 hadi kufikia mwaka huu,huku ikiwahusisha baadhi ya mawaziri wa zamani wa nishati na madini waliohusika kuingia mikataba mibovu iliyoisababishia serikali hasara.

JINAMIZI la Kudanganya Umri Miss Tanzania Bado Lamtesa SITTI MTEMVU...Afunguka Haya

$
0
0
Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amedai sakata la umri lililopelekea kuvuliwa taji la Miss Tanzania ni kitu ambacho kimebadili mfumo wa maisha yake kabisa huku akiwaahidi Watanzania siku moja kuweka wazi ukweli kuhusu umri wake.



Akiongea na Bongo5 wiki hii, Sitti amedai sakata hilo liliweza kubadili mfumo wake mzima wa maisha.

“Mamshukuru Mungu maisha yanaendelea vizuri kwa sababu lile sakata lilikuwa kubwa sana lakini baada ya kumalizika niliamua kurudi shule na namshukuru Mungu nimemaliza salama na sasa anaendelea na shughuli zangu za kawaida,” alisema Sitti. “Ishu ya umri wangu siwezi kuizungumzia kwa sasa tuombe Mungu siku moja nitaanika ukweli na kila mtu anatajua ni nini kilitokea,”

Mrembo huyo kwa sasa anaendelea kufanya bishara ya kitabu chache cha Chozi la Sitti ambacho alikiandika baada ya sakata hilo.

Sitti alisema kitabu hicho kitaweza kuwasaidia vijana wengi hasa wakike katika nyanja mbalimbali za maisha.

JE Wajua Uzuri wa Mwanamke na Utamu Kwenye Tendo la Ngono si Chochote?

$
0
0
HUU NDIO USHAURI WANGU KWAKO
“UZURI WA MWANAMKE UNAWEZA UKAMPELEKEA MWANAUME AKATHUBUTU KUMUOA, LAKINI TABIA YAKE NDIO ITAKAYO MUAMURU ADUMU KWA MUDA GANI NA HUYU MWANAMKE KATIKA NDOA”.

Kuna Mambo Mengine Pesa Haiwezi Kununua Vitu Kama Heshima, Busara Na Upendo
NDUGU YANGU, “KUWA MTAMU KWENYE TENDO LA NGONO INAWEZA IKAMFANYA MWANAMUME ALALE NA WEWE USIKU KUCHA, LAKINI ASUBUHI AKAONDOKA ZAKE, LAKINI KUWA MTAMU KWENYE TENDO LA TABIA, KUNAWEZA KUMFANYA MWANAMUME AKUOE NA ADUMU NA WEWE MPAKA KUFA.”

By Julius Peter Gontako

HIZI NDIO SABABU Zinazoweza Kupelekea Mwanamke Asiolewe Kabisa

$
0
0


Kuoa au kuoelwa ni jambo ambalo watu wengi hutamani kwani ni miongoni mwa hatua kubwa  katika maisha ya kila mmoja. Ukifanya utafiti kwa watu ambao hawajaoa wengi watakwambia wanatamani siku moja wawe na familia bora na yenye furaha, kwani kila mmoja anaamini hayo ni mafanikio kwenye maisha.

Licha ya kuwa kuolewa au kuoa ni jambo jema, baadhi ya watu huwa hawaoi au hawaolewi. Kuto kuoa au kuolewa kunaweza kuelezewa na sababu nyingi sana. Leo tutazungumzia suala la mwanamke kuolewa, na tutaweka bayana baadhi ya tabia chache ambazo zinaweza (zinachangia kwa kiasi kikubwa) mwanamke kuto kuolewa.

Utumiaji mbaya wa mitandao ya kijamii- Hili najua si kwa wanawake tu, lakini kwa sababu leo wao ni walengwa wa mada, tutazungumzia upande wao tu. Baadhi ya wanawake hutumia vibaya mitandao  ya kijamii ambapo huchati tangu asubuhi hadi jioni, wakiinua macho basi wanaangalia Tv na akimaliza channel hii atahamia nyingine, akimaliza mtandao huu atahamia mwingine. Kutwa nzima unakuta anafuatilia staa huyu alifanya nini usiku, huyu alipiga picha gani, kikapanda kikashuka.

Mwisho wa siku mwanamke kama huyu atakuwa hana cha maana alichojifunza kwenye mitandao au kutazama Tv zaidi ya kuanza kuiga yale aliyoyaona. Na hakuna mwanaume muoaji anayetaka mwanamke ambaye akili yake imetawaliwa na mitandao ya kijamii hakumbuki hata kufanya usafi ndani.

Kutokupenda kufanya kazi za nyumbani- Wanawake wengi wa ki-Afrika kwa vile wamekwenda shule wakatambua mambo ya haki sawa kwa wote na wengine kuona kwenye filamu wanaume wakifanya kazi ambazo mara nyingi hufanywa na wanawake, basi na wao ndio wameweka nukta kufanya kazi za nyumbani.

Kuto kana na hali hii, wanawake wamekua wakujiremba tangu mawio hadi machweo, ukitazama kucha zao zilivyondefu unajiuliza hutu anafua kweli? wengine wame amua kuajiri watu wa kuwafulia hadi nguo za ndani. Kwa hali hii isitarajie mwanaume akuoe kwa sababu anajua ni matatizo anapeleka nyumbani.

Kujipara hadi sura yako ya asili inasahaulika- Ni kweli wanaume hupenda mwanamke mrembo na mwenye kupendeza. Lakini hii haimaanishi ndio ujipodoe hadi uchukize. Kila kitu  kwa kiasi chake kwa sababu kitu chochote kikizidi huwa ni sumu.

Jirembe kwa kiasi, hili litavutia watu walio-serious kutaka kukuoa, lakini ukiwa ni wa kujiremba hadi ukapindukia, hakuna muoaji atakaye kuta. Tena ikumbukwe kuna baadhi ya wanaume wao hupenda mwanamke asiyejiremba (wenyewe huita natural)

Hizi ni baadhi tu, na wewe unaweza kuongezea ili kuwakumbusha wasichana wanaotaka kuolewa.

HUYU NDIYE MREMBO ALIYEUTIKISA MTANDAO LEO

Magazeti ya Leo Tanzania Jumapili ya June 25,2017

Tangazo Rasmi La Eid El-fitri Kutoka Bakwata


Vigogo IPTL Waendelea Kukalia Kuti Kavu, Mali Zao Zakamatwa

$
0
0
Serikali  imekamata mali za wafanyabiashara Harbinder Singh Sethi na mwenzake James Rugemalira wanaohusishwa na uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 katika Akaunti ya Tegeta Escrow.

Mali hizo zimekamatwa siku chache baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) kuwafikisha watuhumiwa hao mahakamani.

Kwa mujibu wa gazeti la MTANZANIA Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga hakuweza kupatikana kutoa ufafanuzi wa kina wa hatua ya ofisi yake kushikilia mali za Sethi na Rugemalira.

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), iliiambia MTANZANIA jana kuwa Serikali imelazimika kukamata mali zote za wafanyabiashara hao kama hatua ya kuzuia kuuzwa au kuhamishwa umiliki wake wakati wakiendelea kusota rumande.

“Ni jambo la kawaida katika kesi kama hii, huwezi kuacha mali ambazo ndizo kielelezo katika suala hili. Hivyo hatua ya kwanza ni kumkamata mshtakiwa na kisha ni lazima udhibiti mali zake kwani ndiyo kielelezo muhimu kinachobishaniwa katika kesi husika.

“Unaweza ukaiacha mali halafu mshtakiwa huku akiwa yupo ndani bado akaendelea kutoa maelezo na mali kuhamishwa umiliki wake au hata kuuzwa, kwa hali hiyo ndiyo hulazimika kushikilia mali hizo,” alisema mtoa taarifa huyo ambaye hakupenda kutajwa jina lake .

Ofisi ya DPP inaelezwa imezuia mali zote za Sethi na Rugemalira kwa kuziweka chini ya ulinzi mkali pamoja na kufunga kwa muda akaunti zao za benki.

Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL)/Pan Africa Power (PAP) na Rugemalira wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam Juni 19.

Watuhumiwa hawa tayari wamesomewa mashtaka sita, yakiwamo ya uhujumu uchumi.

Mbali na hayo imeelezwa kuwa orodha ya waliopata mgawo wa fedha hizo za Escrow imezidi kuongezeka, wakiwamo vigogo kutoka wizara nyeti, taasisi, viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya kiserikali na tayari baadhi yao wameanza kuhojiwa na Takukuru mapema wiki hii.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa idadi ya waliohojiwa imefika zaidi ya watu 30 hadi sasa.

Miongoni mwa wanaotajwa kuhojiwa na Takukuru wamo baadhi ya mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne na mtoto wa kigogo wa Serikali, ambao inaelezwa kuwa huenda wakafikishwa mahakamani Jumatatu, huku wengine wakiendelea kuhojiwa zaidi.

Maneno ya Diamond baada ya Rayvanny kunyakua tuzo ya BET

$
0
0
Msanii wa Bongo Flava, Rayvanny kutoka Wasafi Classic Baby (WCB) ameshinda tuzo ya BET (Black Entertainment Television) kipengele cha ‘Viewers Choice Best New International Act Artist’.

Kufuatia ushindi huo msanii Diamond Platnumz ambaye anaiongoza WCB amepongeza ushindi huo wa Rayvanny, amesema kuwa zaidi ya miaka mitatu tunaenda na kurudi patupu lakini safari hii si patupu tena kufuatia ushindi huo.

“Hatimaye leo Unakuja nayo Tanzania Dah! ….Zaidi ya miaka mi 3 tunaenda na kurudi Patupu….Hakika Maisha Uvumilivu na kutokata tamaa…. BRING IT HOME BOSS!!! @babutale”

“WOOOOOOOOOYOOOOOOOO!!!!!!!….. Nikishindwa kwa Mkono wa Kulia, ntatumia hata Mkono wa Kushoto…..ila lazma ifike @Wcb_Wasafi TANZANIA!!!! Chkua hiyo #Wcb_Wasafi #WinningTeam!”

PICHA HIZI ZA WEMA SEPETU ZAWA GUMZO MTANDAONI

$
0
0
SUPASTAA wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu, ametupia picha mpya kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram, zikimuonesha akiwa na mwonekano
mpya ambapo muda mfupi baadaye, mashabiki zake walianza kutoa maoni yao, wengi wakionesha kufurahishwa na mwonekano wake mpya.
Mashabiki hao wamembatiza Wema kwa jina jipya, wakimuita Malkia wa Instagram Tanzania au mwenye insta yake kaja.


Makubwa:Amlazimisha Mme Wake Aoe Mke wa Pili Kisa Hiki Hapa

$
0
0
Habari wana jamvini kunadada mmoja huyo Pichani jirani yetu imekua kero kwa mme wake baada ya kumlazimisha mme wake aoe mke wa pili baada ya kuona kua yeye hawezi kumhimili kua jamaa anaweza kumgegeda kuanzia saa tatu usiku mpaka sasa kumi na bado mchana akitoka kazini anataka afikiee eko. Kwake yeye ameona ni karaha imefikia wakati ameenda kutoa malalamiko kwao na mume huku akiwashauri ndugu zake wa mshauri aoe mke wa pili baada ya mume wake kukataa swala la kuoa mke wa pili.

Hebu tuambizane anacho fanya uyn dada ni sahihi?

MREMBO MASOGANGE AFUNGUKA HAYA KUHUSU UKIMYA WAKE

$
0
0
VIDEO Queen mwenye figa bomba Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange’ amefunguka kuwa ukimya wake wa hivi karibuni na kutojichanganya kwa watu mbalimbali ni kwa sababu ya mpenzi ambaye amempata kwa sasa kwani anambana sana.

Akizungumza  Masogange alisema hivi sasa haendi sehemu yoyote ya starehe wala kujichanganya na watu wengi kwa sababu mpenzi wake huyo amempa masharti hayo na yeye ni lazima ayafuate kwani anaheshimu penzi lake.
“Unajua kipindi cha nyuma kilikuwa cha utoto zaidi kwa sasa nimejitambua vizuri zaidi na ukiwa na mtu ambaye anakusaidia akawa hataki vitu fulani ni lazima kuheshimu ndiyo maana sionekani ovyo kwa sasa,” alisema Masogange.
Viewing all 7853 articles
Browse latest View live