Quantcast
Channel: LEWIS MBONDE BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

ITV na Clouds Media vyatozwa faini ya Tsh 19M na TCRA

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia kitengo chake cha maudhui Jumanne hii kimevitoza faini ya jumla Sh19m vituo vya utangazaji, ITV, Clouds TV na Clouds FM kwa kukiuka kanuni za utangazaji.13925025_1190759717654687_5317016183424975708_n
TCRA wanasema Clouds Media imepigwa faini hiyo kutokana na kosa la kushabikia mapenzi ya mbuzi na binadamu kwenye chombo chao cha habari na kupiga wimbo wa mwanamuziki Mwana FA ambao unapaswa kupigwa muda maalumu ambao wameagizwa.
ITV wamepigwa faini hiyo kutokana na kipindi kutoka bungeni kilichokuwa kinaoongozwa moja kwa moja,ambapo Mbunge wa Iringa Mjini alisikika akisema “Naibu Spika amekuwa kama anavaa pampas,hataki kubanduka kwenye kiti kuongoza bunge”.
TCRA imewakumbusha wadau wote kufuata sheria na maadili ya utangazaji ili kuepuka adhabu na ukiukwaji wa maadili.
Source: Mwananchi/Jamii Forum

Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

Trending Articles