Quantcast
Channel: LEWIS MBONDE BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

Wachezaji wa Korea Kaskazini na Kusini wapiga picha ya pamoja katika Michezo ya Olimpiki Rio 2016

$
0
0
Wanamichezo wa mazoezi ya viungo kutoka Korea Kusini na Kaskazini, ambao wanashiriki Michezo ya Olimpiki Rio 2016, wameuonesha ulimwengu ishara ya umoja, kwa kupiga selfie pamoja.
_90720041_hi034380182Picha hii imesifiwa kama ishara ya moyo wa michezo ya Olimpiki
Lee Eun-ju wa Korea Kusini na Hong Un-jong wa Kaskazini walipiga picha wakiwa wametabasamu wakati wa mazoezi kabla ya kuanza kwa michezo hiyo.
Picha za wanawake hao wawili zimesifiwa sana kwa kuashiria moyo wa Olimpiki wa kuwaleta watu pamoja.
Korea Kaskazini na Kusini huwa na uhasama mkubwa.
Uhusiano baina ya nchi hizo mbili umedorora zaidi, kutokana na hatua ya karibuni ya Pyongyang kufanyia majaribio makombora.
_90720043_hi034437380Wanamichezo hao walikutana wakati wa raundi ya kufuzu kwa mashindano kamili tarehe 7 Agosti
_90720045_hi034437387Wanamichezo wote wawili hawakufanikiwa kufuzu, lakini bila shaka walibeba ‘dhahabu’ ya uanadiplomasia
“Hii ndiyo maana huwa twashiriki Olimpiki,” mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Ian Bremmer aliandika kwenye Twitter na kuweka picha hiyo.
Ujumbe wake ulisambazwa zaidi ya mara 18,000.
Wengine hata hivyo hawakufurahishwa na hilo.
“Anaruhusiwa kufanya urafiki na adui?”, mmoja wa watu mitandaoni waliuliza, na wengine wakaeleza wasiwasi kwamba huenda Hong akaadhibiwa akirejea nyumbani.
Lee, 17, na Hong, 27, wote walishiriki kama wachezaji wa kufuzu wakiwa binafsi. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Lee kushiriki michezo ya Olimpiki.
_90720049_hi034438658Lee akishiriki kwenye mashindano ya Olimpiki Rio
_90720047_hi034436686Hong akishiriki mashindano ya Rio tarehe 7 Agosti. Alikuwa mwanamichezo wa kwanza wa mazoezi ya viungo kushindia taifa lake nishani, aliposhinda Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2008.
Wengi walieleza tofauti iliyopo baina ya wanawake hao wawili na timu ya Olimpiki ya Lebanon iliyokataa kuabiri basi moja na wanamichezo wa Israel.
Source: BBC

Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

Trending Articles