
July 16 2016 ilikuwa ni zamu ya wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa klabu ya Dar es Salaam Young Africans kucheza mchezo wao wa tatu wa Kundi A wa Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya klabu ya Medeama SC ya Ghana.

Kabla ya mchezo wa leo July 16 dhidi ya Medeama Yanga walikuwa nafasi ya mwisho kutokana na kukubali vipigo viwili mfululizo vya michezo yao miwili ya mwanzo, mchezo wa kwanza Yanga walicheza Algeria na MO Bejaia na kukubali kipigo cha goli 1-0 na baadae kipigo tena cha goli 1-0 kutoka TP Mazembe ya Congo, mchezo ambao ulichezwa Taifa Dar es Salaam.

Mchezo wa July 16 Yanga wanaofundishwa na kocha wao muholanzi Hans van der Pluijm, walikuwa wanahitaji ushindi wa aina yoyote ili waweze kuwa katika nafasi nzuri ya kuwania kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, hata hivyo Yanga wamelazimishwa sare ya goli 1-1.

Kikosi cha Yanga ambacho kilionekana kuwa na morali ya kuondoka na point tatu na kusahaulisha mashabiki wake vipigo viwili vya mwanzo, Yanga walianza kupata goli dakika ya 2 kupitia kwa Donald Ngoma ambaye alitumia vyema pasi ya mzimbabwe mwenzake Thabani Kamusoko, furaha ya Yanga ilizimwa dakika ya 17 baada ya Benard Danso kuisawazishia Medeama, Yanga bado inaendelea kuwa nafasi ya mwisho katika msimamo wa Kundi A.

GOLI LA MECHI YA YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1