
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba mwenyekiti wa Chama cha DP nchini Tanzania mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia asubuhi hii katika ajali katika Kijiji cha Msola mkoani Pwani

Marehemu Mchungaji Mtikila baada ya kupata ajali na kufariki dunia leo asubuhi
Picha hii tumeiziba kutokana na sababu za kimaadili

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Jafar Ibrahim amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wengine watatu waliokuwa katika gari hilo wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Taarifa kamili tunakuletea hivi punde hapa hapa Habarika Blog Endelea kuwa nasi
R.I.P Mchungaji Mtikila.