Quantcast
Channel: LEWIS MBONDE BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

TATHMINI YA SHERIA YA MTANDAO - RADIO ONE

$
0
0

http://1.bp.blogspot.com/-_c8kx3G6SnE/VUELrJfcqxI/AAAAAAAAD9g/YSma3Rf65cU/s1600/Sheria%2Bya%2BMakosa%2Bya%2BMtandao%2B%2B-%2B%2BMatondo.Blogspot.com.png

SERIKALI imeshauriwa kuutumia vema mwezi Oktoba, mwaka huu kukuza uelewa  kwa wananchi juu ya masuala ya mitandao ili kupunguza kama si kuondoa kabisa uhalifu mitandaoni.

Rai hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mtaalamu wa Usalama wa Mitandao na Uchunguzi wa Makosa ya Kidijitali, Yusuph Kileo wakati akizungumza na Majira.

"Nichukue nafasi hii kutambua na kuhamasisha tukio la kipekee katika anga ya usalama katika mitandao jambo ambalo limekuwa likiadhimishwa kila mwaka katika mwezi wa Oktoba, ambapo mataifa yanaadhimisha siku ya uelewa wa masuala ya usalama wa mitandao duniani kote," alisema Kileo.

Alisema, wakati mataifa mbalimbali duniani yakitarajiwa kuadhimisha tukio hilo anaamini Tanzania itauchukulia mwezi huo kinamna ya kipekee ili kuweza kukuza uelewa kwa watu wake.  Hilo ni tukio ambalo nategemea kampuni mbalimbali na maeneo mengine yataandaa programu mbalimbali za kukuza uelewa wa masuala ya usalama mitandaoni ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na wanausalama wote wa mitandao duniani kote," aliongeza mtaalamu huyo.

Aidha, alisema inaaminika kama ilivyo katika uhalifu mwingine wowote kuwa ni vigumu kumaliza kabisa tatizo ila kuna njia kadhaa ambazo kwa umoja wake zikifanyiwa kazi vizuri zinaweza kabisa kupunguza kwa kiasi kikubwa  tatizo la uhalifu kwenye mitandao. 

"Tatizo kubwa  ni kuwa njia hizi zimekuwa zikiishia katika maandishi baada ya kujadiliwa na wanausalama wa mitandao; mimi binafsi nilikuwa miongoni mwao," alifafanua Kileo.

Alisema, baadhi ya njia za kukabiliana  na tatizo hilo ni kupitia elimu ya uelewa wa uhalifu katika mtandao na namna ya kujilinda. 

"Elimu hii inatoa fursa kwa mwananchi wa kawaida kutambua aina mbalimbali za uhalifu kwenye mitandao, athari zake, njia ya kujilinda na namna ya kulinda wenzake," alisema Kileo.

KUPITIA KIPINDI CHA KUMEPAMBAZUKA CHA RADIO ONE NIMEPATA KUSHIRIKI KWA NJIA YA SIMU HOJA ILIYO HOJI ---- IKIWA NI TAKRIBANI MWEZI MMOJA BAADA YA KUANZA KUTUMIKA KWA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO HAPA NCHINI,WIZARA YA MAWASILIANO,SAYANSI NA TEKNOLOJIA PAMOJA NA WADAU WENGINE WANATOA TATHIMINI GANI.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

Latest Images

Trending Articles