Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC ,CCM Makao Makuu Dodoma akiwa ameshikilia kitabu cha Kanuni za Kamati ya Wabunge Wote wa Chama Cha Mapinduzi.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika leo Novemba 15, 2015 mjini Dodoma imewateua wana-CCM watatu watakaopigiwa kura na wabunge wote wa CCM ili kumpata mgombea wa CCM katika nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Walioteuliwa kugombea nafasi hiyo na Kamati Kuu iliyofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni pamoja na