Quantcast
Channel: LEWIS MBONDE BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

MAJAMBAZI WATEKA MAGARI HUKO TABORA HUKU WAKIIMBA "HAPA KAZI TU"

$
0
0

Kundi la watu wanaoaminika kuwa ni majambazi wakiwa na silaha mbalimbali kama mapanga na marungu, juzi waliteka magari katika kijiji  cha Igogo,Wilaya ya Igunga huku wakiimba ‘hapa kazi tu’.

Baadhi ya madereva waliokumbwa na dhahama hiyo, walidai kuwa baada ya kusimamishwa na majambazi hao waliwashambulia kwa marungu na bapa la panga huku wakiwaamrisha watoe fedha na simu za mkononi huku wakitamka kila wakati kauli mbiu iliyotumika kwenye kampeni ya 'hapa kazi tu'.

Mmoja wa madereva hao alisimulia na kusema alikumbana na mkasa huo usiku wakati akitokea hospitali ya rufaa kupeleka wagonjwa.

“Wakati wakitushambulia kwa mapanga , majambazi hao walikuwa wakisema ‘hapa kazi tu, toeni pesa na simu'” alisema.
 
Chanzo:Dunia Kiganjani

Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

Trending Articles