Waharifu wa kwenye mtandao “hacers” wanaonekana kuzidi kutawala dunia kwa kuiba akaunti za mitandaoni za watu mbalimbali lakini zaidi wakiwa ni watu maarufu ambao wanaonekana kuwa na watu wengi ambao wamewafata.
Mmoja wa mastaa ambao wanaonekana sasa hackers wamefanya akaunti yake ya Instagram kuwa nyumbani kwao ni rapa Joh Makini kwani akaunti yake ya Instagram imeibiwa na watu hao na hii inakuwa sio mara ya kwanza kwa kitendo hicho kujitokeza.
Baada ya kuiba akaunti hiyo, watu hao wameibadili jina na sasa inaitwa fashionswebtz ikiwa na picha tano, watu ambao wameifata Laki 977 na ikiwa haijamfata mtu yoyote.
Joh Makini Instagram Accunt
Mwonekano wa sasa wa akaunti ya Instagram ya  Joh Makini
Taarifa za akaunti hiyo kuibiwa zimetolewa na watu wa karibu na Joh Makini akwepo Vanessa Mdee na Jux.