Ulinzi wa polisi viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa leo kabla ya mtuhumiwa wa mauwaji kufikishwa.
Wananchi wakiwa foleni kukaguliwa kabla ya kuingia mahakamani leo.
Mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi akipakiwa kwenye gari za FFU
Msafala wa gari za FFU zilizomsindikiza askari mwenzao anayekutwa na kosa la kuua bila kukusudia leo
Askari wa FFU wakitoka mbio mahakamani hapo
Wananchi na wanahabari wakitoka mahakamani hapo
Wakili kutoka mtandao wa watetezi wa haki za binadamu ((THRDC), Benedict Ishabakaki akizungumza na wanahabari nje ya viwanja vya mahakamani leo
Askari hao wakimtoa mahakamani hapo leo mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi
Na MatukiodaimaBlog Iringa
MAHAKAMA kuu kanda ya Iringa imemtia hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia askari Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia ( FFU )Iringa G 58 Pacificius Cleophace Simon (27) anayetuhumiwa kuuua mwaahabari Daudi Mwangosi mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi.
Hata hivyo mahakamani hiyo imesema adhabu kwa mtuhumiwa huyo kutokana na kupatikana na kosa hilo la kuua bila kukusudia itatolewa Julai 27 majira ya saa 4 asubuhi mwaka huu.
Jaji Dkt Paul Kiwelo ambaye anayesikiliza kesi hiyo alisema mahakakamani hapo jana kuwa kati ya vielelezo vitano vyote vilivyoleta kama ushahidi mahakamani hapo kwa ajili ya kesi hiyo namba 54 ya mwaka 2013 ni kielelezo kimoja pekee cha ungamo kwa mlinzi wa amani ambacho ndicho hakukuwa na shaka na ungamo hilo ndilo lililomtia hatiani asikari huyo.
Alivitaja vielelezo vilivyopelekwa kama ushahidi kuwa ni Ramani ya eneo la tukio,ripoti ya tabibu ,ungamo la mlinzi wa amani ,silaha aliyoitumia na rejista ya silaha.