Quantcast
Channel: LEWIS MBONDE BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

VIDEO:Koffi Olomide ampiga dansa wake wa kike airport Nairobi baada ya kuwasili Kenya

$
0
0
http://omg.co.ke/wp-content/uploads/2016/03/4129894293_e64ddfb827_b.jpg
Katika hali ambayo imeonekana kuwashangaza watu wengi, msanii wa rumba kutoka Congo, Koffi ameonekana akimpiga mmoja wa madansa wake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) ambaye ameambatana nae katika onyesho ambalo amekwenda kutumbuiza Kenya.

Video hiyo imemwonyesha Koffi Olomide akimfata dansa huyo na kumpiga kwa mguu huku Polisi wa Kenya wakimuangalia na baada ya hapo walimtuliza na kumpeleka katika gari aliloandaliwa.

Chanzo kimoja cha karibu na Olomide kimesema kuwa sababu ya Koffi kumpiga dansa wake ni kuwa dansa huyo alikuwa akizungumza kuwa na ugomvi na mke wa Koffi, Cindy jambo ambalo lilimkasirikisha na kushindwa kujizuia na kwenda kumpiga.

Dansa huyo ni mmoja wa madansa sita ambao wameongozana na Koffi Olomide katika onyesho linalotaraji kufanyika katika kijiji cha kitalii cha Bomas litakalofanyika Jumamosi ya Julai, 23.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

Trending Articles