Quantcast
Channel: LEWIS MBONDE BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

Mrema Afunguka: Asema Rais Magufuli Anaishi Kwenye Maneno Yake Hana Longo Longo

$
0
0
Mwenyekiti wa TLP Dkt. Augustino Lyatonga Mrema amesema Rais Dkt. John Magufuli anaishi kwenye maneno yake kwa kuwa mwaka jana alipofika kwenye jimbo la Vunjo aliwaambia wananchi wamchague Mrema na wasipomchagua atampa kazi, jambo ambalo ametimiza

Mrema ameyasema hayo alipofanya mahojiano maalum na EATV kuhusu uwezo wake wa kusimamia Bodi ya Parole ambayo yeye ndiye mwenyekiti wake baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli.

''Nafasi ambayo amenipa Rais Dkt. Magufuli nina uzoefu nayo kwa kuwa mwaka 1994 njia tuliyokuwa tunaitumia ni kutembelea magereza na kuongea na wafungwa hasa wanaotumia vyombo vya moto na wengine walikuwa wanataja walipoficha silaha, na wengine walikuwa wanataja wahalifu ndani ya jamii na nilipata ushirikiano wa kutosha.''

Aidha Dkt. Mrema amesema anachokitafuta Rais Dkt. John Magufuli ni mtu mzalendo na hatua ya Rais kumteua ni kuonesha imani yake kwake na si kwamba ana nia ya kuua upinzani bali ana lengo jema la kuchukua mtu mwenye uzoefu ili atumikie watanzania kwa sababu lengo la upinzani siyo kutaka wananchi wateseke.

''Watanzania wategemee ufanisi na kazi iliyotukuka ya kupunguza wafungwa magerezani ili waweze kupewa adhabu nyingine ndani ya jamii na wapewe watu wa kuwasimamia, kwa kuwa tatizo kubwa tulilonalo sasa hivi ni mlundikano wa wafungwa na serikali haiwezi kujitika kutanua magereza kwa kuwa sasa hivi inajikita kuboresha huduma za afya na elimu mfano suala la madawati'' Amesema Dkt. Mrema

Kuhusu yeye kuwa mzee na kama ataweza kumudu nafasi hiyo Dkt. Mrema amesema yeye ana miaka 72 na hana uzee wowote ambao utamfanya akwame kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na hata kabla ya uteuzi Rais ana watu wa kumshauri na wameona anafaa nafasi hiyo

Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

Trending Articles