Quantcast
Channel: LEWIS MBONDE BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

MTANZANIA MPENDA SELFIE ASHTAKIWA KWA KUMTHALILISHA MHUDUMU WA NDEGE

$
0
0


Raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 42 anashikiliwa na Mahakama Kuu ya makosa ya jinai ya jiji la Dubai, Falme za Kiarabu kwa tuhuma za kumdhalilisha mhudumu wa kike wa Shirika la Ndege la Emirates.

Raia huyo ambaye jina lake limeandikwa kwa herufi za mwanzo za MA, anasubiri kesi yake kusikilizwa Julai 24, mwaka huu.

Mtanzania huyo anadaiwa kumdhalilisha mhudumu huyo mwenye umri wa miaka 25  wakati wakiwa wanasafiri na ndege hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Dubai, Aprili 24 mwaka huu.

Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa juzi kwenye mtandao wa shirika hilo la ndege unaoitwa, Emirates 24/7, Mtanzania huyo alimwomba mhudumu huyo wapige picha ya pamoja kwa ajili ya ukumbusho.

Mhudumu huyo ambaye pia jina lake halikutajwa, alikubali.




“Wakati anapiga picha aliniwekea mkono kwenye bega. Kiongozi wangu aliona na kumuonya. Baada ya kuona hivyo, akaomba tupige selfie,” amesema mhudumu huyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

Trending Articles