Quantcast
Channel: LEWIS MBONDE BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

KIONGOZI WA UPINZANI UGANDA DR.KIZZA AKAMATWA BAADA YA KIJIAPISHA

$
0
0
:Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dr.Kizza Besigye amekamatwa na kikosi cha usalama baada kuamua kujiapisha kama Rais wa nchi hiyo hapo jana ikiwa taifa hilo likijiandaa kushuhudia kiapo cha Rais mteule wa taifa hilo Yoweri Museveni akiapishwa rasmi hii leo.
Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inaonesha Dr Besigye akila kiapo mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya jaji wa mahakama ya juu.Usalama umeimarishwa nchini humo huku mitandao ya kijamii ikizimwa kwa sababu za kiusalama.

Mpinzani mkuu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Dk. Kizza Besigye ambaye amekuwa akipinga ushindi wa Rais huyo, amekamatwa na polisi wa nchi hiyo baada ya jana kujiapisha kuwa Rais ikiwa ni siku moja tu (leo) kabla ya Museven kuapishwa.

Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa vizuizi  vya polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa taifa hilo''.

Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana ''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa mahakama ya juu''.

Video hiyo ilisambazwa kwa kasi  kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliopita akiwaacha kwa mbali wapinzani wake wakuu, Kizza Besigye na Amama Mbabazi.

Kadhalika, Mahakama Kuu nchini humo ilihalalisha ushindi wa Museveni baada ya kutupilia mbali shauri la pingamizi la ushindi huo lililowasilishwa na Amama Mbabazi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

Trending Articles