Quantcast
Channel: LEWIS MBONDE BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

BASATA Yatoa Siku 7 Kwa Wamiliki wa Blogs, sound cloud, U-Tube , ITunes, Radio na Tv Kufuta Nyimbo za Wasanii Zenye Kukiuka Maadili

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linawaagiza wasanii, wamiliki na waendeshaji wa wavuti, tovuti na vyombo vya habari hususan radio na runinga kuondoa na kuacha mara moja kurusha au kutangaza au kucheza nyimbo zote zenye maudhui ya kashfa, matusi, kejeli, udhalilishaji ambazo zinahatarisha kuigawa jamii ya kitanzania katika misingi yoyote hasa katika kipindi hiki Taifa linapoendelea na kampeni za kisiasa na kujiandaa na uchaguzi mkuu.

Kwa mujibu wa kifungu namba 118 (a-d) cha Sheria ya Bunge namba 9 ya Mawasiliano ya Mtandao ya mwaka 2010 ni marufuku kwa njia yoyote kwa mtu au chombo chochote kutengeneza, kuzalisha, kusambaza au kutangaza ujumbe ambao una mlengo wa matusi, dharau, uzushi au jinai kwa lengo la kutukana, kutisha, kusumbua au kushusha hadhi ya mtu mwingine.
 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

Trending Articles