Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amechanganya mambo na kusoma hotuba ya zamani wakati wa ufunguzi wa kikao cha tatu cha bunge la nane la nchi hiyo.
Katika kioja hicho, rais Mugabe amejikuta akirudia kusoma hotuba aliyoitoa wakati akilihutubia taifa Agosti 25 mwaka huu, wakati akishinikizwa na wabunge wa upinzani kuhusu kudorora kwa uchumi.
Msemaji wake George Charamba amekaririwa akisema mkanganyiko huo umetokana na mchanganyiko uliopo katika ofifi ya rais ya nyaraka.
Matangazo ya moja kwa moja ya hotuba hiyo yalikatishwa kwenye radio na televisheni, baada ya kuwepo ripoti kuwa wabunge wa upinzani walipanga kumvuruga.
LAKINI HABARI ZA LEO HII
Takriban wabunge sita wa upinzani wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC), wanadaiwa kupokea ujumbe wa simu ya mkononi wa vitisho kutoka kwa mtu aliyejiita “Death” akiwataka wawe watulivu.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amewaita wabunge wa nchi hiyo kwa kikao maalum siku moja baadaye yake kuwasomea hotuba isiyofaa, kimakosa.
Anatarajiwa kusoma hotuba iliyo sahihi wakati wa kikao hicho leo.Haijaeleweka ni vipi Bw Mugabe aliishia kusoma hotuba isiyofaa wakati wa kufunguliwa kwa bunge, lakini msemaji wake alikuwa ameambia gazeti la serikali la Herald kwamba kosa hilo lilitokana na suitafahamu katika afisi ya kiongozi huyo.
Kiongozi huyo aliaibika sana baada yake kurudia hotuba hiyo aliyokuwa ameisoma awali Agosti 25 wakati wa kikao cha kufafanua kuhusu hali ya taifa.
Kituo cha utangazaji wa serikali nchini humo kimewataka wabunge kufika kuhudhuria kile kilichotajwa kuwa kikao kisicho cha kawaida cha bunge.