Msanii wa muziki kutoka Marekani, Ne-Yo ameandika historia ya muziki mkoani Mwanza baada ya kufanya show ya nguvu katika tamasha la Jembeka Festival 2016 lililofanyika Jumamosi hii katika viwanja vya CCM Kirumba Mwanza.
Ne-Yo akifanya yake

Muimbaji huyo alipanda jukwaani kwa shangwe na kuanza kuimba nyimbo zake moja hadi nyingine kwa hisia hali ambayo iliibua shangwe kubwa. Pia baada ya kuimba nyimbo zake kadhaa alimwita Diamond jukwaani na kuimba naye wimbo ambao ni kolabo yao inayokuja.
Wasanii wengine ambao waliwapagawisha mashabiki ni, Diamond, Stamina, Nay wa Mitego, Mr Blue, Maua Sama, Ruby, Mo Music, Barakah Da Prince na wasanii wengine. Tazama picha.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akibariki show ya Jembeka Festival 2016.







Nay wa Mitego




Stamina



