Quantcast
Channel: LEWIS MBONDE BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

Haya hapa Matokeo ya Mtibwa Sugar Vs Yanga Jamhuri Morogoro Jana

$
0
0

Bado Ligi Kuu soka Tanzania bara inaendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti, September 30 Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara Dar Es Salaam Young African wamesafiri kuifuata Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
DSC_0469
Kikosi cha Mtibwa Sugar
Hii ni moja kati ya michezo ya kuvutia kwa wapenzi na mashabiki wa soka Tanzania, kwani timu itakayoibuka mshindi wa mechi hii, itapata nafasi ya kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2015/2016, Mtibwa Sugar ambayo ni timu mwenyeji wa mchezo huu imeshinda mechi zake nne za mwanzo kama ilivyo kwa Yanga.
DSC_0465
Kikosi cha Yanga
Mchezo ambao ulikuwa wa kukamiana hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika kila timu haikubahatika kuona nyavu za mwenzake, kipindi cha pili Yanga walionekana kubadilika na kuja na mbinu mbadala, Malimi Busungu akapachika goli la kwanza dakika ya 53 ya mchezo, Donald Ngoma ambaye awali alionekana kudhibitiwa na mabeki wa Mtibwa Sugar, alibahatika kuitumia nafasi aliyoipata dakika ya 89 ya mchezo na kuufanya mchezo kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
DSC_0615
Wachezaji wa Yanga na Mtibwa Sugar wakizozana na refa
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa September 30
Simba 1-0 Stand United
Azam FC 2-0 Coastal Union
Prisons 0-0 Mwadui FC
Maji maji 1-1 Ndanda FC
African Sports0-1 Mgambo Shooting
Kagera Sugar0-0 JKT Ruvu
DSC_0571
Simon Msuva akitafuta njia za kumtoka Issa Rashid wa Mtibwa Sugar
DSC_0077
Juma Abdul akijaribu kutaka kumpokonya mpira beki wa Mtibwa Sugar
DSC_0068
Donald Ngoma akikabwa na mabeki wawili wa Mtibwa Sugar ili asipate nafasi ya kufunga
DSC_0107
Donald Ngoma akiugulia maumivu
DSC_0094
Donald Ngoma akijaribu kudhibiti mpira aliopokonywa na beki wa Mtibwa Sugar
DSC_0590
Andrew Vicent akipiga kichwa mbele ya Donald Ngoma wa Yanga
DSC_0598
Donald Ngoma akishangilia goli lake na Simon Msuva kwa staili ya kucheza muziki
DSC_0602
Donald Ngoma, Simon Msuva na Malimi Busungu wakishangilia goli kwa pamoja
DSC_0065
Ngoma akidhibitiwa na beki wa Mtibwa Sugar
DSC_0059
Amissi Tambwe akidhibitiwa na Andrew Vicent katika harakati za kuwania mpira wa kichwa
DSC_0064
Juma Abdul wa Yanga akijaribu kumtoka Vicent Barnabas
DSC_0084
Wachezaji wa Mtibwa wakiwania mpira na mchezaji wa Yanga

Viewing all articles
Browse latest Browse all 7853

Trending Articles